Mkuu wa IRGC: Wayemeni hatimaye wataibuka washindi


  • Mkuu wa IRGC: Wayemeni hatimaye wataibuka washindi

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amelipongeza taifa la Yemen kwa kulitetea kwa ushujaa taifa la Palestina wakati huu wa hujuma ya umwagaji damu ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza na kueleza kuwa Wayemen hatimaye wataibuka washindi.

Meja Jenerali Hossein Salami aliyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya al-Masirah ya Yemen yenye lugha ya Kiarabu siku ya Jumamosi.

Ameongeza kuwa: "Wayemeni, kwa vile wamepinga kwa utu na heshima hadi leo, wataendeleza upinzani wao kwa neema ya Mwenyezi Mungu na hatimaye wataibuka washindi."

Aliongeza, “The Mrengo wa Muqawama haujadhoofika; na kila mtu anashuhudia jinsi Wayemen wanavyoilinda Palestina kwa umahiri na kufanya maandamano kila Ijumaa kuunga mkono Gaza."

Jeshi la Yemen lilitangaza siku ya Ijumaa kwamba lilirusha "kombora la balestiki la hypersonic" ambalo lililenga Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wa huko Tel Aviv, na kusisitiza kuwa lilikuwa limelenga shabaha yake.

Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Yahya Saree alisema katika taarifa yake kwa njia ya televisheni kwamba shambulio hilo lilisababisha hasara na kutatiza usafiri wa ndege katika uwanja huo.

Harakati ya muqawama ya Ansarullah ya Yemen pia imekuwa ikilenga meli zenye uhusiano na Israel, Marekani au Uingereza ili kulazimisha tawala hizo kusitisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Wanajeshi wa Yemen wamesema kuwa hawatasimamisha operesheni zao hadi mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza yatakapomalizika.

Tokea Oktoba 2023 hadi sasa, Israel imewauwa Wapalestina wasiopungua 45,3436, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine 108,038 huko Gaza.