Nigeria yakanusha kushirikiana na Ufaransa kuyumbisha Niger

 

.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kiongozi wa Niger, Abdourahmane Tchiani, alshutumu jirani yake Nigeria kwa kujaribu kuyumbisha nchi yake.

Nigeria imekanusha shutuma kutoka kwa kiongozi wa kijeshi wa Niger, Brig Jenerali Abdourahmane Tchiani, kwa kushirikiana na Ufaransa kulivuruga taifa hilo linaloongozwa na junta.

Katika mahojiano ya Siku ya Krismasi, Jenerali Tchiani aliishutumu Ufaransa kwa kushirikiana na makundi ya wanamgambo katika eneo la Ziwa Chad ili kudhoofisha usalama wa Niger, ikidaiwa kuwa Nigeria inafahamu.

"Mamlaka za Nigeria hazijui kuhusu hatua hii ya kizembe," Jenerali Tchiani alinukuliwa akisema na AFP.

kijibu, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Nigeria, Nuhu Ribadu, aliiambia BBC Hausa kwamba madai hayo "hayana msingi" na "uongo".

Bw Ribadu alisema Nigeria kamwe "haitahujumu Niger au kuruhusu maafa yoyote kuikumba".

Waziri wa Habari wa Nigeria, Mohammed Idris, alisema madai hayo hayana msingi na "mbinu ya kitofauti inayolenga kuficha kushindwa kwa utawala wake".