Putin aomba radhi kwa ajali ya ndege, bila kusema Urusi ina makosa
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameomba radhi kwa rais wa nchi jirani ya Azerbaijan kwa kudungua ndege ya kubeba raia katika anga ya Urusi, ambapo watu 38 waliuawa - lakini akaacha kusema Urusi ilihusika.
Katika maoni yake ya kwanza juu ya ajali ya siku ya Krismasi, Putin alisema "tukio la kusikitisha" lilitokea wakati mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi ilipokuwa ikifukuza ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Ilikuwa imeripotiwa kuwa ndege hiyo ilishambuliwa na mifumo ya ulinzi ya anga ya Urusi ilipojaribu kutua Chechnya - na kuilazimisha kuvuka bahari ya Caspian.
Ilianguka huko Kazakhstan, na kuua 38 kati ya 67 waliokuwemo.