Rais Yoon aliidhinisha jeshi kufyatua risasi Bungeni, yafichua Ofisi ya Mwendesha Mashtaka

 Nchini Korea Kusini, rais aliidhinisha jeshi kufyatua risasi kuingia Bungeni, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Korea Kusini. Mnamo Desemba 3, mkuu wa nchi, aliyesimamishwa kazi kwa sasa, alijaribu kuweka sheria ya kijeshi nchini humo. Wakati huo huo alipeleka jeshi katika Bunge la taifa. Sasa yamejulikana mengi zaidi kuhusu kile kilichotokea usiku huo.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wakati akitangaza sheria ya kijeshi kwenye televisheni, Desemba 4, 2024.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wakati akitangaza sheria ya kijeshi kwenye televisheni, Desemba 4, 2024. © Soo-hyeon Kim / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Seoul, Camille Ruiz

Haya ni maneno ya umwagaji damu. Yangetamkwa mnamo Desemba 3 mwaka jana. Katika maongezi ya simu akimpigia kamanda wa kijeshi ambaye alikuwa karibu na Bunge, rais Yoon Suk-yeol inadaiwa aliamuru: "kuharibu lango kwa shoka ikiwa ni lazima" au "kuwatoa watu nje, hata ikiwa itabidi kufyatua risasi."

Takriban mwezi mmoja uliopita, baada ya sheria ya kijeshi kutangazwa nchini Korea Kusini, wanajeshi walivamia Bunge. Walipanda ua, wakavunja madirisha. Helikopta za jeshi hata zilitua juu ya paa la jengo hilo. Wabunge walifanikiwa kupiga kura kuondoa sheria ya kijeshi.

Wakili wa rais anabaini kwamba maelezo kutoka kwa upande wa mashtaka yana upendeleo. Ripoti hiyo ya takriban kurasa kumi pia inabainisha kuwa rais alikuwa akijadili sheria ya kijeshi na maafisa wakuu wa kijeshi mwezi Machi mwaka jana. Yoon Suk Yeol sasa ndiye mlengwa wa uchunguzi wa "uasi" na "matumizi mabaya ya mamlaka". Bado anakataa kufika mbele ya wachunguzi.

Tangu wakati huo, nchi hiyo imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kiuchumi. Jana, Ijumaa, Desemba 27, Bunge la taifa lilimsimamisha kazi Waziri Mkuu na kaimu rais, wiki mbili baada ya kutimuliwa kwa Yoon Suk Yeol.