Real Madrid wanamtaka Van de Ven - Tetesi za Soka Ulaya Jumapili

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wanataka kumsajili Micky van de Ven kutoka Tottenham huku kukiwa na tatizo la majeraha kwenye safu ya ulinzi, wakati Barcelona ikiwa katika uwezekano wa kuondokewa na Dani Olmo na Frenkie de Jong mnamo mwezi Januari kipindi ambacho miamba hao wa La Liga wanakabiliwa na tatizo la kupunguza gharama.
Beki wa Tottenham na Uholanzi Micky van de Ven, 23, analengwa na Real Madrid Januari kufuatia msururu wa majeraha kwa wachezaji wa safu ya ulinzi wa klabu hiyo ya Uhispania. (Relevo - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini mchezaji huru na nahodha wa zamani Sergio Ramos, 38, anataka ndoto irejee Real Madrid kufuatia majeraha ya Mhispania mwenzake, Dani Carvajal, 32, David Alaba, 32, Mbrazil Eder Militao, 26. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Barcelona Dani Olmo, 26, yuko tayari kuhamia kwa mkopo katika Ligi ya Primia mwezi Januari ikiwa klabu yake haiwezi kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kwa kipindi cha pili cha msimu. (TBR Football)
Wakati huo huo, upande wa La Liga, wanajaribu kutoa pesa ili waweze kumsajili Olmo – ikiwa ni pamoja na kupunguza bei wanayotaka kumnunua kiungo wa kati Mholanzi Frenkie de Jong, 27. (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, hajaiambia Liverpool kwamba amechagua kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure msimu huu, licha ya ripoti kutoka Uhispania. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 30, hatafikiria kukatiza mkataba wake wa mkopo wa Arsenal kutoka Chelsea mwezi Januari, licha ya kutoanza mchezo wa ligi tangu Oktoba 19. (Athletic - subscription required)
Everton bado hawajaanza mazungumzo ya mkataba na beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 22, ambaye analengwa na Liverpool, Manchester United na Manchester City. (Daily Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanafuatilia hali ya beki wa kushoto wa Fulham Antonee Robinson, na uwezekano wa kumnunua beki huyo wa Marekani, 27, mwezi Januari. (Football Insider)
Mshambulizi wa Colombia Jhon Duran, 21, anaweza kuondoka Aston Villa katika dirisha la uhamisho, huku mshambuliaji wa Atalanta mwenye umri wa miaka 25 raia wa Italia Mateo Retegui akichukuliwa kama mbadala wake. (Caught Offside),
Real Madrid wanapanga kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 24, kuhusu mkataba mpya. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 33, anapendelea kuhamia Marekani na Ligi Kuu ya Marekani, ikiwa Mbelgiji huyo ataondoka mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Mshambulizi wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli, 34, anasakwa na klabu ya Mexico Cruz Azul - ambayo itakuwa klabu ya 13 katika taaluma ya Muitaliano huyo. (Gazzeta dello Sport - in Italian)