Serikali ya Al-Joulani yatoa agizo la siri: Picha zozote za mauaji na uporaji zisisambazwe
Kufuatia kusambazwa picha na video za mauaji na uporaji unaofanywa na wanachama wa Tahrir al-Sham nchini Syria, utawala mpya wa Al-Joulani umetoa agizo la siri la kupiga marufuku usambazaji wa picha na video hizo.
Maafisa walio chini ya Al-Joulani, mkuu wa kundi la
Hayat Tahrir al-Sham, wamepokea waraka wa siri, unaopiga marufuku
kurekodi video za aina yoyote za operesheni za ukamataji watu,
mapigano na mauaji ya hadharani yanayofanywa nchini Syria.
Waraka huo unajumuisha miji 30 ya nchi hiyo.
Inasemekana kuwa, kusambazwa video zinazohusiana na kuwatia nguvuni
watu, kuwaua na kuwanyonga hadharani na kuchoma moto maeneo matakatifu
nchini Syria kunakofanywa na wafuasi wa Al-Joulani kumezikasirisha fikra
za umma ndani ya nchi hiyo na hata katika nchi zingine.
Kwa mujibu wa ripoti, 95% ya vitendo vya kinyama vinavyofanywa na mawakala wa al-Joulani havirekodiwi na wala havisajiliwi.
Kuanzia Novemba 27, 2024, wapinzani wabeba silaha nchini Syria
walianzisha operesheni za kijeshi katika maeneo ya kaskazini-magharibi,
magharibi na kusini magharibi mwa mji wa Aleppo kwa lengo la kumuondoa
madarakani Bashar al-Assad na hatimaye baada ya siku 11, mnamo Desemba
8, walitangaza kulidhibiti jiji la Damascus na kuondoka Assad nchini
humo.../