Shirika la ndege la Jeju Air laomba msamaha kwa ajali

 

.

Chanzo cha picha, EPA/Yonhap

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Jeju Air ameomba msamaha hadharani kwa waathiriwa wa ajali hiyo.

Katika mkutano mfupi wa wanahabari, Kim E-bae na wakuu wengine wa kampuni waliinamisha vichwa vyao na kusema kuwaunga mkono wafiwa ndio kipaumbele chao kwa sasa.

"Sisi Jeju Air tunainamisha vichwa vyetu kwa kuomba msamaha kwa kila mtu ambaye ameathirika katika tukio hili kwenye Uwanja wa Ndege wa Muan," inasema taarifa hiyo ambayo imetafsiriwa kwa Kiingereza.

"Tutafanya kila tuwezalo kujibu tukio hilo. Tunasikitika kwa mfadhaika."

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, lakini vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa huenda ilisababishwa na ndege kukamatwa kwenye mfumo wa ndege hiyo.

Ajali hii ya kwanza mbaya katika historia ya Jeju Air, mojawapo ya mashirika makubwa ya ndege ya bei ya chini ya Korea Kusini, ambayo ilianzishwa mwaka 2005