Uchaguzi mpya unaweza kuchukua hadi miaka minne, kiongozi wa waasi wa Syria anasema

Chanzo cha picha, Reuters
Uchaguzi mpya nchini Syria unaweza kuchukua hadi miaka minne, kiongozi wa waasi Ahmed al-Sharaa amesema katika mahojiano ya matangazo.
Hii ni mara yake ya kwanza kutoa ratiba ya uchaguzi unaowezekana nchini Syria tangu kundi lake la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) liongoze mashambulizi ya waasi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa Rais Bashar al-Assad.
Katika mahojiano na shirika la utangazaji la serikali ya Saudi Al Arabiya siku ya Jumapili, alisema kuandaa katiba mpya kunaweza kuchukua hadi miaka mitatu.
Alisema pia inaweza kuchukua mwaka mmoja kabla ya Wasyria kuanza kuona mabadiliko makubwa na maboresho ya huduma za umma kufuatia kupinduliwa kwa utawala wa Assad.
Sharaa alisema Syria inahitaji kujenga upya mfumo wake wa sheria na italazimika kufanya sensa kamili ya watu ili kuendesha uchaguzi halali.