UN kuanza kusambaza misaada ya chakula Sudan leo
Msafara mkubwa zaidi uliobeba chakula cha misaada umefika katikak mji mkuu wa Sudan, Khartoum tangu kuanza kwa mzozo mwezi Aprili 2023.
Msafara huo unajumuisha usaidizi wa chakula wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na misaada mingine ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na misaada kwa wadau wengine.
Msaada huo wa chakula kwa sasa unashushwa baada ya msafara unaoongozwa na WFP wa malori 28 umepanga kusambaza chakula siku ya Jumapili, 29 Desemba, na chakula hiki kinakusudiwa kwa takriban watu 78,000.
“Msafara huu pia ni wa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo ambapo msaada wa chakula wa WFP unafikishwa Mayo na Alingaz kusini mwa Khartoum. Maeneo yote mawili yako katika hatari ya njaa, kulingana na uainishaji wa viwango vya njaa (IPC).” Ameeleza Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
WFP imekuwa ikifanya kazi ya kufikia maeneo yote ya Khartoum ikitumia fursa ya utulivu mfupi katika mapigano kutoa msaada wa chakula wakati pia ikiunga mkono juhudi za jamii kutoa milo moto ya kila siku.
Mwezi Julai, msafara wa WFP ulipeleka msaada wa chakula na lishe kwa watu wa Bahri,
WFP pia inafanya kazi kupanua utoaji wa vyakula vya moto kupitia miradi inayoendeshwa na jamii huko Jebel Awlia. WFP tayari inasaidia jikoni za jamii huko Mayo na inafanya kazi kupanua utoaji milo moto hadi Alingaz pia.