“Vikwazo Vikubwa Dhidi ya Iran Vinarudi Jumamosi Usiku – Ushirikiano wa Nyuklia Ukiwekwa Hatua ya Hatua!”
“Iran imeonya itasimamisha ushirikiano na IAEA iwapo vikwazo vitarejeshwa, huku dunia ikisubiri hatua za kidiplomasia.”
Vikwazo vikubwa vya kiuchumi na kijeshi dhidi ya Iran, vilivyopunguzwa chini ya makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia miaka 10 iliyopita, vinatarajiwa kurejeshwa Jumamosi usiku.
Hii inajiri baada ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuishutumu Iran kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita.
Iran imepewa siku 30 kutafuta suluhu ya kidiplomasia ili kuepuka kurejeshwa kwa vikwazo, lakini imeitaja hatua hii kuwa kinyume cha sheria.
Nchi hiyo pia imeonya itasimamisha ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) iwapo vikwazo vitarejeshwa.
Hii ni hatua nyingine ya kuongezeka kwa mzozo wa nyuklia, baada ya Iran kuzidisha shughuli za nyuklia zilizopigwa marufuku baada ya Marekani kujiondoa makubaliano hayo mwaka 2016.