Posts

Israel inasema inadhibiti eneo la mpaka wa Gaza na Misri

Image
  Jeshi la Israel linasema kuwa limechukua udhibiti wa eneo la kimkakati kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri, linalojulikana kama Philadelphi Msemaji wa Kikosi cha Ulinzi cha Israel (IDF) alisema kuwa takribani njia za chini kwa chini 20 zinazotumiwa na Hamas kuingiza silaha Gaza zimepatikana huko. Televisheni ya Misri ilinukuu vyanzo vinavyokanusha hilo, na kusema Israel ilikuwa inajaribu kuhalalisha operesheni yake ya kijeshi katika mji wa kusini wa Gaza wa Rafah. Tangazo hilo linakuja wakati wa mvutano mkali na Misri. "Katika siku za hivi karibuni, wanajeshi wa IDF walianzisha udhibiti wa operesheni kwenye Ukanda wa Philadelphi, kwenye mpaka kati ya Misri na Rafah," msemaji wa IDF Rear Admiral Daniel Hagari alisema Jumatano. Alielezea ukanda huo kama "uhai" kwa Hamas, ambapo kundi hilo "liliingiza silaha mara kwa mara katika Ukanda wa Gaza". Bw.Hagari baadaye alisema katika kikao na wanahabari kwamba hangeweza kuwa na uhakika kwamba njia zote zilivuka ha

Uchaguzi Afrika Kusini 2024: Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea

Image
  Kura zinahesabiwa baada ya uchaguzi wa hapo jana nchini Afrika Kusini. Mistari mirefu ilikuwa nje ya vituo vya kupigia kura kote nchini. Afisa mmoja wa uchaguzi mjini Johannesburg aliiambia BBC kuwa misururu hiyo inakumbusha uchaguzi wa kihistoria wa 1994, wakati watu weusi walipiga kura kwa mara ya kwanza, na ambao ulishuhudia Nelson Mandela kuwa rais. Watu wengi walikuwa bado wanangoja kupiga kura wakati kura zilipofungwa rasmi saa 2100 saa za ndani (1900 GMT) lakini tume ya uchaguzi ilisema kwamba wote wataruhusiwa kupiga kura zao. Matokeo ya kwanza yataanza kutangazwa Alhamisi asubuhi na matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwa juma. Chama cha ANC kimepoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira. Kura za maoni zinaonesha kuwa huenda ikapoteza wingi wake bungeni. Sifiso Buthelezi, ambaye alipiga kura katika Joubert Park mjini Johannesburg, kituo kikubwa zaidi cha kupigia kura nchini Afrika Kusini, aliiambia BBC

Saa 6 zilizopitaLondon: Polisi 3 wajeruhiwa huku watu 40 wakikamatwa katika maandamano ya wanaopendelea Palestina

Image
  Maafisa watatu wa polisi wamejeruhiwa wakati wa maandamano huko Westminster yaliyoandaliwa na Palestine Solidarity Campaign na makundi mengine. Afisa mmoja alipata jeraha baya usoni baada ya kupigwa na chupa iliyorushwa kutoka katikati ya umati, Polisi wa mji walisema. Mamlaka ilisema mshukiwa bado hajatambuliwa lakini polisi wanaendelea na uchunguzi. Watu 40 walikamatwa kuhusiana na shambulio dhidi ya wafanyikazi wa dharura, ghasia kwenye barabara kuu na ukiukwaji wa sheria za umma ulifanyika, polisi ilisema. Polisi walisema "wengi" wa waandamanaji - kati ya watu 8,000 na 10,000 - waliondoka kabla ya kuanza kwa maandamano huku kundi la watu wapatao 500 wakibaki na kuendelea kuandamana.

Sweden kutoa kifurushi kikubwa zaidi cha msaada wa kijeshi kwa Ukraine

Image
  Sweden imetangaza kifurushi cha 16 na kikubwa zaidi cha usaidizi wa kijeshi kwa Ukraine unaofikia euro bilioni 1.16. Msaada huo unajumuisha ndege ya kutambua rada ya ASC 890. Vyanzo vingi vya habari vya kijeshi vya kimataifa vimeandika kwamba ndege mbili aina hiyo zitakabidhiwa Ukraine. Kulingana na Waziri wa Ulinzi wa Uswidi Paul Johnson, ASC 890 itakuwa na "mchango mkubwa zaidi kwa ulinzi wa anga wa Ukraine" kwani itaongeza na kuimarisha ndege za kivita za F-16 za Marekani. "Zinaweza kutambua makombora ya kwenda umbali mrefu, ndege zisizo na rubani na kulenga za ardhini na baharini," aliambia mkutano wa wanahabari. Aidha, Uswidi itatoa AMRAAM - makombora ya masafa ya kati yanayorushwa angani. Katika ujumbe kutoka wizara ya ulinzi inasemekana kwamba zinaimarishwa kwa matumizi katika mifumo ya makombora ya kukinga ndege ya ardhini. Makombora hayo pia hutumiwa na ndege za kivita za F-16, ambazo Ukraine inatarajia kupokea kutoka nchi za Ulaya mwishoni mwa mwaka.

Zelensky aombwa kutodai yale "yasiowezekana" kutoka kwa NATO – Telegraph

Image
  Ukraine haitakaribia kujiunga na muungano wa NATO mwaka huu, kutokana na hofu kwamba hili litaingiza muungano huo katika vita na Urusi, gazeti la Telegraph limesema. Vyanzo vya habari vinadai kuwa wakati wa maandalizi ya mkutano wa kilele wa NATO, ambao utafanyika Washington mnamo Julai 9-11 na utakuwa maalum kwa maadhimisho ya miaka 75 ya muungano huo, Marekani na Ujerumani zilizungumzia suala la kuweka makataa ya wazi ya uwezekano wa Ukraine kuijiunga na muungano. "Wana mashaka sana juu ya kuendelea kwa Ukraine kutaka kuwa mwanachama kamili wa NATO mwaka huu," chanzo kinachoufahamu utawala wa Biden kililiambia gazeti hilo. "Marekani inaweza isiwe na wasiwasi kama Ujerumani, lakini ina wasiwasi juu ya tishio linalotokana na Urusi kwa muungano huo." Katika suala hili, Rais Zelensky ameombwa kutotaka yale "yasiowezekana" kutoka kwa muungano wa NATO, Telegraph imesema. Mwaka jana, Zelensky aliita hali hiyo kuwa "isiyo ya kawaida na ya kipuuzi" wa

Israel inatabiri kuwa vita na Hamas vitaendelea hadi angalau mwisho wa mwaka

Image
    Maelezo ya picha, Vifaru vya Israel vilijikita kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza Mshauri wa usalama wa taifa wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Tzachi Hanegbi, amesema anatarajia mapigano huko Gaza kuendelea hadi angalau mwisho wa mwaka huu. Hanegbi pia amesema kuwa jeshi la Israel sasa linadhibiti asilimia sabini na tano ya kile kinachoitwa "Philadelphia Corridor," eneo la buffer kati ya Gaza na Misri. Hanegbi, anayechukuliwa kuwa msiri wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, pia aliongeza kuwa Israel hivi karibuni itachukua udhibiti kamili wa ukanda wa kimkakati kwenye mpaka wa Gaza na Misri. Mpango huo, alisema, ni kufanya kazi na Wamisri kuzuia utoroshwaji wa silaha kwa makundi yenye silaha ya Palestina. Maneno ya mshauri wa Netanyahu yanaweza kufasiriwa kuwa ni ishara kwamba Israel haiko tayari kutii wito wa kimataifa wa kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano na wanamgambo wa Hamas na kubadilishana mateka wanaoshikiliwa nao kwa wafungwa wa Kipalestina.

Urusi: Kwanini maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi wanakamatwa?

Image
  Mkuu wa Kurugenzi Kuu ya Jeshi na Naibu Mkuu wa majenerali, Jenerali Vadym Shamarin, amekamatwa. Hii ni mara ya nne kukamatwa afisa wa ngazi ya juu wa Urusi ndani ya mwezi mmoja. Shamarin anashukiwa kupokea hongo, mashirika ya Urusi yakinukuu mahakama ya kijeshi, ambayo iliamua jenerali huyo awekwe kizuizini. Wa kwanza kukamatwa alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi Timur Ivanov, ambaye alisimamia ujenzi wa kambi za jeshi. Alikamatwa Aprili 24. Katikati ya Mei, ilifahamika kuwa mkuu wa Idara ya Wafanyakazi ya Wizara ya Ulinzi, Yuriy Kuznetsov alikuwa kizuizini. Mwezi Mei 17, kamanda wa zamani wa Kikosi cha 58 katika Wilaya ya Kijeshi ya Kusini, Ivan Popov, alikamatwa. Wote wanatuhumiwa kwa ufisadi au ubadhirifu. Vita dhidi ya Ufisadi "Bila shaka, mapambano dhidi ya rushwa yanaendelea katika idara zote," alisema msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmytro Peskov baada ya kukamatwa kwa Shamarin. Bbaada ya kuapishwa Vladimir Putin mwezi Mei, Serhiy Shoigu aliacha wadhifa wa waziri