Israel inatabiri kuwa vita na Hamas vitaendelea hadi angalau mwisho wa mwaka

 .

 Maelezo ya picha, Vifaru vya Israel vilijikita kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza

Mshauri wa usalama wa taifa wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Tzachi Hanegbi, amesema anatarajia mapigano huko Gaza kuendelea hadi angalau mwisho wa mwaka huu.

Hanegbi pia amesema kuwa jeshi la Israel sasa linadhibiti asilimia sabini na tano ya kile kinachoitwa "Philadelphia Corridor," eneo la buffer kati ya Gaza na Misri.

Hanegbi, anayechukuliwa kuwa msiri wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, pia aliongeza kuwa Israel hivi karibuni itachukua udhibiti kamili wa ukanda wa kimkakati kwenye mpaka wa Gaza na Misri. Mpango huo, alisema, ni kufanya kazi na Wamisri kuzuia utoroshwaji wa silaha kwa makundi yenye silaha ya Palestina.

Maneno ya mshauri wa Netanyahu yanaweza kufasiriwa kuwa ni ishara kwamba Israel haiko tayari kutii wito wa kimataifa wa kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano na wanamgambo wa Hamas na kubadilishana mateka wanaoshikiliwa nao kwa wafungwa wa Kipalestina.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China