Chad yataka Marekani isitishe shughuli za kijeshi nchini humo

 

  • Chad yataka Marekani isitishe shughuli za kijeshi nchini humo

Chad imeitaka Marekani isitishe mara moja kwa shughuli za kijeshi katika kambi ya nchi hiyo iliyo kati ya kaskazini na kati mwa Afrika.

Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga la Chad amesema kuwa hajapokea nyaraka zozote kutoka kwa Wamarekani "zinazoonyesha sababu ya wao kuhatajia kuwepo kwao katika Uwanja wa Ndege za Kijeshi wa Adji Kosseï (BAK)" katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena.

Kulingana na Jenerali Idris Amin Ahmed, hakuna mfumo wa kisheria wa kuhalalisha uwepo wa jeshi la Marekani katika uwanja huo wa ndege za kijeshi.

Hapo awali vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwa Chad iliitishia Marekani kuwa itavunja makubaliano yao ya ulinzi sambamba na kuwataka wanajeshi wa Marekani kuondoka katika kambi ya Ufaransa katika mji mkuu huo. Uamuzi huo ulikuja baada ya nchi jirani ya Niger kusitisha makubaliano ya kijeshi na Marekani.

Kuna vituo vya kijeshi vya Ufaransa na Marekania nchini Chad. Hivi majuzi, nchi hiyo imeonyesha nia ya kupanua wigo wa washirika wake wa kijeshi.

Vyanzo vingine vya habari vinasema kuwa barua hiyo inaweza kuwa mbinu ya mazungumzo inayotumiwa na utawala wa Chad kutaka mkataba mpya ambao utazingatia maslahi ya nchi hiyo.

Idadi kamili ya wanajeshi wa Marekani katika taifa hilo haijulikani, ingawa afisa mmoja wa Marekani anadai kuwa ni chini ya 100

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China