Je, mvutano kati ya Israel na Iran umeisha (kwa sasa) baada ya mashambulizi ya pande zote mbili?

 


Saa chache baada ya vyombo vya habari vya Marekani kuripoti shambulio la moja kwa moja la Israel dhidi ya Iran, bado tunapokea taarifa zinazokinzana kutoka kwa vyanzo mbalimbali kuhusu madai ya shambulio hili.

Hadi kufikia Ijumaa, misimamo ya mamlaka ya kijeshi ya Iran na vyombo vya habari vinavyohusishwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wanadokeza kwamba, kwa mtazamo wa kipropaganda, msimamo wa Iran ni kwamba hakuna jambo la maana lililotokea na kwamba hakutakuwa na mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Abdolrahim Mousavi, kamanda mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alijibu maswali kuhusu hatua ya Iran hukusu shambulio la Israel kwa kusema: "Mmeona majibu ya Iran hapo awali," akimaanisha shambulio la makombora la Iran mnamo tarehe 13 mwezi wa Aprili.

Zaidi ya hayo, Makao makuu ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran yamesema: "Hakujatokea hujuma za kigeni dhidi ya nchi."

Ingawa vyombo vya habari vya Irani viliripoti shughuli fulani na maafisa walithibitisha kwamba mfumo wa ulinzi wa Iran ulikuwa umeandaliwa mapema kwa ajili ya kukabiliana na mashambulio Ijumaa, kulingana na maelezeo ya Irani ni mashambulio ya Israeli yalikuwa "duni na madogo tu ambapo quadcopter [droni] " zilizoonekana angani karibu na mji wa Isfahan, na zote ziliharibiwa angani.

Zaidi ya hayo, Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran limethibitisha kuwa hakuna kituo chochote cha nyuklia cha nchi hiyo kilichoshambuliwa.

Shirika hilo lilikariri kwamba vifaa vya nyuklia, kwa sababu ya unyeti unaohusishwa na vifaa vya mionzi, haipaswi kamwe kkulengwa kijeshi.

Bila kujali maelezo ya shambulio hili linalowezekana, kulingana na habari iliyotolewa, kilichotokea kinaweza kuwa jibu lililopangwa na sahihi ambalo linaafiki malengo ya Israeli.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wairan waliingia mitaani Ijumaa hii kuunga mkono hatua za nchi yao dhidi ya Israel.

Hata hivyo, ili kuelewa ukweli zaidi, habari zaidi zinahitajika, ambazo bado haijawekwa wazi.

Bado haijulikani ni wapi, ikiwa shambulio lilitokea, lengo lililofikiwa, ni aina gani ya silaha zilizotumiwa, na kiwango kamili cha uharibifu .

Maelezo muhimu zaidi kuhusu uwezekano wa shambulio la Israel yanatoka kwa maafisa wa kijeshi wa Marekani ambao hawakutajwa majina ambao waliviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba katika saa za mapema siku ya Ijumaa kombora la Israel lilirushwa kuelekea Iran na kufanikiwa kulenga shabaha yake.

Israel haijatoa maoni yoyote wala kutoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.

Hiki si kisa cha kwanza kwa Israel kufanya operesheni za kijeshi katika ardhi ya Iran.

Katika matukio ya awali, Israel haijakiri rasmi kuhusika kwake na shambulio lolote au hujuma yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran.

Wakati huu, hata hivyo, Israeli inatarajiwa kukiri shambulio hilo, hasa kwa vile Iran imekiri hadharani mashambulizi yake ya makombora dhidi ya Israeli, na kutaja kama ''utetezi halali wa haki zake za uhuru''.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kwa Israeli, maendeleo yanayohusiana na Wapalestina yanasalia kuwa kipaumbele cha juu sana na cha dharura.

Je, lengo la uwezekano wa Israel kushambulia Iran ni nini?

Hesabu ya Israeli katika kuijibu Iran inapaswa kuzingatia ushiriki wake wa sasa wa kijeshi katika mzozo wa Gaza.

Kwa Israel, ambayo imehusika katika vita hivyo kwa zaidi ya miezi sita na bado haijawaachilia mateka wote au kuwatenganisha na Hamas, masuala yanayohusiana na Wapalestina yanasalia kuwa kipaumbele cha juu na cha haraka kwa Israel.

Hata hivyo, kupanua mzozo huo kwa kuzingatia hisia za umma au matakwa ya watu wenye msimamo mkali katika nchi hii hakutafikia malengo haya.

Ikizingatiwa kuwa hii ni mara ya kwanza katika historia ya sasa kwa Iran kufanya mashambulizi katika ardhi ya Israel, Israel ina uhalali mkubwa ndani ya sheria za kimataifa kwa shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Iran.

Kwa mtazamo huu, Israel inalazimika kujibu uvamizi wa moja kwa moja wa kijeshi unaofanywa na nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Katika kiwango hiki, tukisisitiza kanuni za kimsingi kama vile haki ya kutetea mamlaka ya kitaifa, watoa maamuzi wengi nchini Israeli wanaelezea jibu hilo kama hatua ya lazima.

Hata hivyo, mwitikio huu nyeti, ingawa unaweza kuonekana kama hitaji la "halisi" ndani ya misingi ya kimuundo ya mahusiano ya sasa ya kimataifa, hauna lengo pekee la "kulipiza kisasi" au "adhabu kwa adui."

Moja ya malengo makuu ya Israeli katika kujibu ni kuzuia.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Israel haikukubali kuwa ilikuwa na jukumu la shambulio la Ijumaa asubuhi huko Isfahan.

Lengo ni kujizuia kujirudia kwa matukio sawa na mashambulizi ya makombora ya moja kwa moja ya IRGC, lengo ambalo pia lilitolewa baada ya shambulio la Israel kwenye ubalozi mdogo wa Damascus ili kuzuia mashambulizi kama hayo yajayo.

Eneo la uwezekano wa shambulio la kombora la Israel ndani ya Iran na kiwango cha uharibifu ni muhimu.

Iwapo shambulio hilo lililenga eneo la thamani kubwa ya kimkakati na kijeshi kwa Iran, hata shambulio dogo linaweza kutuma ujumbe mzito kwa kiongozi wa Iran Ali Khamenei na makamanda wa IRGC.

Kwa hakika, ikiwa Israel imeweza imesababisha pigo kubwa kwa kile kinachoonekana kuwa ni mashambulizi machache, imedhihirisha uwezo wake wa hali ya juu wa kijeshi kwa Tehran na ikiwezekana hata kuwaonyesha makamanda wa IRGC kiwango cha kupenya kwake kiintelijensia na uwezo wake wa kushambulia.

Kama ilivyoripotiwa na vyanzo vya Marekani, kuna uwezekano kwamba kombora moja tu lilirushwa, ambalo, ikiwa ni kweli, linaweza kuwa onyesho la nguvu: katika simulizi hii, Iran ilirusha karibu makombora 300 na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israeli na kushindwa kusababisha uharibifu mkubwa, wakati kombora moja lilipopiga shabaha muhimu.

Kiwango cha uharibifu unaosababishwa na shambulio hili pia huathiri ujumbe ambao Israeli inakusudia kutuma kwa Iran.

Iwapo Israel imeweza kuleta madhara makubwa kwa jeshi la Iran au uwezo wa kiulinzi kwa shambulio moja lililolengwa na sahihi, kwa kawaida itakuwa na athari kubwa zaidi za kuzuia.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ikiwa hakuna mashambulizi zaidi yatakayotokea, hakutakuwa na kuongezeka kwa migogoro ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili , angalau kwa muda mfupi.

Je, mvutano umekwisha?

Kwa kuwa hata shambulio dogo la kombora linaweza kufikia malengo muhimu ya kimkakati kwa Israeli, mashambulizi zaidi yanaweza yasitokee.

Ikiwa hakutatokea mashambulizi ya ziada, uwezekano wa kuongezeka kwa harakati za kijeshi kati ya nchi hizo mbili utasitishwa, angalau katika muda mfupi.

Ukweli ni kwamba Israel ina vichocheo vingi vya kuepusha kuongezeka kwa mivutano , na kuwafanya washirika wake wa Magharibi kuridhika na kujiweka katika mstari wa mbele.

Msimamo wa kimataifa wa Israel ulikuwa umedhoofika sana katika wiki za hivi karibuni kimataifa, hadi kufikia hatua ambapo miezi sita ya mzozo wa Gaza, Marekani haikuipiga tena kura ya turufu dhidi ya Israel katika Baraza la Usalama.

Azimio hili liliitaka Israel kukubaliana mara moja kusitisha mapigano, hali isiyokubalika kwa Israel kwani bado ina idadi kubwa ya raia wake wanaoshikiliwa na makundi ya Kiislamu ya Palestina, ikiwemo Hamas.

Muda mfupi baada ya azimio hilo kupitishwa, Israel ilishambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kuanzia hapo, habari kuhusu vita vya Gaza ziliathiriwa pakubwa na mvutano wa kijeshi kati ya nchi hii na Iran.

Iran ilipojibu shambulio hili kwa kuishambulia Israel kwa makombora mnamo Aprili 13, msimamo wa kimataifa wa Israel ulibadilika haraka machoni pa washirika wake wa Magharibi .

Baada ya shambulio la Iran, serikali za Ulaya kama Uingereza na Ufaransa, wala maafisa wa Marekani, hawakuzingatia zaidi mgogoro wa kibinadamu wa raia huko Gaza au haja ya kubadilishwa mkakati wa kijeshi ya Israel, badala yake walisisitiza haki halali ya Israel ya kujihami. yenyewe dhidi ya nchi ya kigeni.

Israel iliondoka haraka kutoka kushutumiwa kwa kukiuka haki za binadamu na sheria za kimataifa katika simulizi kubwa la vita vya Gaza hadi kuonyeshwa kama mwathirika wa shambulio la kombora lililoenea na Iran, mwanachama asiyeridhika wa jumuiya ya kimataifa na serikali ya kidini yenye itikadi kali na isiyo ya kawaida. rekodi nzuri sana.

Miitikio ya serikali za Ulaya na Marekani kuhusu mashambulizi ya Iran yalionyesha kuwa kukabiliana na nguvu na ushawishi wa Iran ni kipaumbele cha juu sana kwa nchi za Magharibi.

Hata hivyo, msaada huu ulioenea wa Magharibi kwa Israeli unakuja na masharti. Kuongezeka kwa vita na kuongezeka ukosefu wa usalama katika Mashariki ya Kati changamoto kwa kiasi kikubwa maslahi ya Magharibi katika eneo.

Kwa sababu hii, mara tu mashambulizi ya Iran yalipoisha, walianza kampeni mpya ya kisiasa yenye lengo la kuzuia mashambulizi makubwa ya Israel dhidi ya Iran.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran siku ya Ijumaa huenda yakawafurahisha washirika wake wa Magharibi, ambao wamekuwa wakiitaka kutojibu mashambulizi ya Tehran ya Aprili 13.

Iwapo jibu la Israel kwa Iran ni dogo katika mashambulizi ya Ijumaa asubuhi, hakika haitawaridhisha wafuasi wa Benjamin Netanyahu ambao wana misimamo mikali ya sera za kigeni.

Hata hivyo, upeo na vipimo vya shambulio hilo huenda vitawafurahisha washirika wa Magharibi wa Israel na wale wote wanaotetea kujizuia kwa pande zote mbili ili kuepusha maangamizi ya vita kamili.

Kinyume chake, iwapo Israel itapuuza maonyo na nasaha za mara kwa mara za wanadiplomasia wake wa Magharibi na kutengeneza mazingira ambayo yanaifanya Iran itangaze kuwa itajibu tena, na kwa upana zaidi kuliko hapo awali, Israel inaweza kupoteza tena huruma ya washirika wake kwa urahisi.

Mbali na washirika wa nchi za Magharibi wa Israel, ambao wamelishinikiza baraza la mawaziri la vita la Netanyahu liepuke kuichokoza zaidi Iran, ndani ya Israel baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanaamini kuwa nchi hiyo kwa wakati huu haipaswi kupoteza rasilimali zake za kijeshi katika vita hatari na Iran.

Israel imekuwa ikikabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa kwa miaka mingi na nafasi ya Netanyahu katika kilele cha muundo wa mamlaka ya nchi yake ni tete.

Juu ya hayo, mashambulizi ya Oktoba 7 ya Hamas, jibu la Israel na kushindwa kuwaachilia mateka na kuwaangamiza Hamas tayari yamemgharimu Netanyahu na kuzidi kudhoofisha msimamo wake.

Kwa hivyo, kwa Israeli, shambulio lililoenea ambalo husababisha uharibifu mkubwa kwa Irani sio kazi rahisi.

Shambulio kama hilo, pamoja na kuathiri nafasi mpya ambayo Israel imeipata kimataifa, linaweza kuwa na matokeo yasiyoweza kudhibitiwa ambayo hayatakiwi kwa jeshi na jumuiya ya usalama ya Israel wala yanaendana na maslahi ya kisiasa ya vyama kama vile Likud, ambao kwa sasa wanashikilia madaraka. katika Israeli, na wanapingwa na wapinzani wao.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China