Wanawake 100 wa BBC 2024: Ni nani yuko kwenye orodha mwaka huu?

 

Wanawake 100 wa BBC 2024: Ni nani yuko kwenye orodha mwaka huu?

Picha ya baadhi ya washiriki wa msimu huu wa BBC World Service 100 Women

BBC imezindua orodha yake ya wanawake 100 mashuhuri duniani mwaka 2024

Miongoni mwao ni Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Nadia Murad, Aliyenusurika ubakaji na mwanaharakati Gisele Pelicot, muigizjai Sharon Stone, Mwanariadha wa Olimpiki Rebeca Andrade na Allyson Felix, muimbaji Raye, msanii Tracet Emin, mwanaharakati wa tabia nchi Adenike Oladosu na mwandishi Rivera Garza.

Kutoka kukabiliana na migogoro hatari na mizozo ya kibinadamu huko Gaza, Lebanon, Ukraine na Sudan, hadi kushuhudia mivutano ya kijamii uliyofuatiwa na chaguzi tofauti duniani, wanawake wamelazimika kufikia viwango vipya vya ujasiri.

Wanawake 100 wa BBC inafahamu fika jinsi mwaka huu ulivyowahangaisha wanawake kwa kuwaenzi wale ambao wanahamasisha mabadiliko kwa ujasiri huku ulimwengu unaowazunguka ukibadilika. Orodha hii pia imejitolea kuchunguza athari za dharura za hali ya hewa, na kuwaangazia wanaharakati waanzilishi wanaosaidia jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuishi nazo.

Majina hayajaorodheshwa kwa mpangilio maalum

Chagua kitengo
Sunita Williams

Sunita Williams, Marekani

Mwanaanga

Wakati mwanaanga wa Nasa Sunita Williams alipoabiri chombo cha Starliner tarehe 5 mwezi Juni, alitarajia kurejea kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga(ISS) baada ya siku nane.

Lakini kufuatia msururu wa hitilafu za kimitambo, Williams na wanaanga wezake Barry Wilmore walifahamishwa kuwa hawataweza kurejea duniani hadi Februari 2025.

Williams, rubani mstaafu wa helikota ya jeshi la wanamaji na mshikiliaji rekodi wanamke aliyetembea zaidi angani,alikuwa mtu wa kwanza kukimbia mbio za marathon angani mwaka 2007.

Licha ya kuwa mbali familia yake na marafiki kwa 400km juu ya ardhi, amepokea kwa ustahamilivu taarifa za kuendelea kusalia katika anga za mbali, akielezea chombo cha angani anachotumia kuwa ''mahali pake pa furaha''

Hamida Aman

Hamida Aman, Afghanistan

Mjasiriamali wa vyombo vya habari na elimu

Wakati wasichana wa Afghanistan walipozuiliwa kupata elimu ya shule ya upili na Taliban, mjasiriamali wa vyombo vya habari Hamida Aman aliamua kuanzisha Begum Academy, chuo kinachotoa elimu mtandaoni bila malipo kwa wanafunzi ambao hawakuweza kuenda shule.

Katika mwaka uliopita, mtandao huo wa elimu umeweza kutoa video zaidi ya 8,500 za elimu kwa lugha za Dari na Pashto, inayojumuisha mtaala wa wanafunzi wa darasa la saba hadi 12.

Mnamo mwezi Machi alizindua Begum TV, chaneli ya kielimu kutangaza kozi za chuo cha Begum kupitia setilaiti.

Huduma hiyo ilifuatiwa na Radio yake ya mradi wa Begum, kitoa kilichoanzishwa na wanawake, kwa ajili ya wanawake, ambacho kilianzishwa baada ya Taliban kuchukua uongozi wa Afghanistan mwaka 2021.

Adenike Titilope Oladosu

Adenike Titilope Oladosu, Nigeria

Mtetezi wa haki ya hali ya hewa

Mnigeria Adenike Titilope Oladosu ni mwanzilishi wa I Lead Climate Action, vuguvugu la wanawake na vijana mashinani linalopigania mabadiliko ya hali ya hewa.

Amefanya kazi kuhamasisha jamii jinsi uchafuzi wa mazingira ulivyoathiri Ziwa Chad- katika makutano ya mataifa ya Nigeria, Niger, Chad na Cameroon- ambapo raslimali za maji zinapungua zinazua vurugu.

Kazi ya Oladosu inaangazia masuala ya kimazingira na kijamii, hasa vileyanavyomuathiri mwanamke wa Kiafrika, ambaye anamhami kwa ujuzi wa kilimo katika maeneo ambayo kuenea kwa jangwa kunaathiri moja kwa moja usalama wa chakula.

Kwa kushiriki katika makongamano kadhaa ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kuanzia mwaka 20219, amewahimiza watunga sera kupatia kipaombele masuala ya kustahamili mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.

Mgogoro wa hali ya hewa ni suala la ustahimilivu ambalo hatuna budi kushinda. Kunusurika mgogoro huu tunahitaji kuwekeza katika teknolojia na uvumbuzi.

Adenike Titilope Oladosu

Plestia Alaqad

Plestia Alaqad, Maeneo ya Palestina

Mwandishi wa habari na mshairi

Plestia Alaqad mwenye umri wa miaka 22 alikuwa ndio mwanzo amehitimu kutoka chuo kikuu wakati vita vya Gaza vilipoanza. Katika siku za mwanzo za vita, alichapisha video yake akiwa ndani ya nyumba yake wakati wa mashambulizi makali ya anga ya Israel.

Ilisambaa kwa kasi, na kujikusanyia wafuasi milioni nne kwenye mtandao wa Instagram kwa maelezo yaliyofuata kuhusu hali ya Gaza, kwa kutumia mashairi na maelezo aliyoweka kwenye shajara. Kumbukumbu yake kulingana na ripoti hizi, "Eyes of Gaza", itachapishwa hivi karibuni.

Alaqad ni Mwanahabari Bora wa tuzo ya One Young World 2024. Pia amewatetea Wapalestina katika vikao vya hadhi ya juu kama vile Mkutano wa Kilele wa World Government

Alaqad aliondoka Gaza mnamo Novemba 2023. Ametunukiwa udhamini wa shahada ya uzamili katika masomo ya vyombo vya habari huko Beirut.

Svetlana Anokhina

Svetlana Anokhina, Urusi

Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu

Svetlana Anokhina ametumia muda mwingi kusaidia waathiriwa wa ukatili wa kijinsia kutoroka kaskazini mwa Urusi ,eneo lililo na idadi kubwa ya waumini wa kiislamu kupitia eneo la mashariki mwa Ulaya na Asia.

Pamoja na waathiriwa ,alianzisha mradi wa Marem mwaka wa 2020. Ni mkakati wa kuwasaidia wanawake walio hatarini katika eneo la Dagestan, Chechnya na kuwapatia hifadhi ya muda na kuwapa usaidizi wa kisaikolojia na kisheria.

Anokhina aliamua kugura Urusi mnamo 2021, baada ya maafisa wa usalama wa Chechen na Dagestani kuvamia hifadhi ya wanawake.

Mwaka jana, Mamlaka ilianza kumchunguza aliposhtakiwa kwa uhalifu kwa kukosoa vikosi vya jeshi la Urusi.

Christina Assi

Christina Assi, Lebanon

Mwanahabri mpiga picha

Mwanahabari mpiga picha Christina Assi alikulia Lebanon katika miaka ya 1990- wakati kulikuwa na misukosuko ya mara kwa mara kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe- na hii ilichochea ari yake ya kuangazia mzozo huo na kusimulia taarifa zisizo na kifani za vita

Maisha yake yalibadilika vibaya Oktoba mwaka 2023, alipojeruhiwa katika shambulio la Israel kusini mwa Lebanon.

Shambulio hilo lilisababisha kifo cha mwanahabari mwenzake Issam Abdallah, wafanyakazi wengine watano kujeruhiwa katika tukio ambalo baadaye lilimfanya Assi kukatwa mguu wake.

Kisa hicho kilimfanya apiganie usalama wa wanahabari na kutoa ushiriki wake katika upokezanaji wa mwenge wa Olimpiki wa 2024 mjini Paris kwa heshima ya wanahabari wote ambao waliofariki wakiwa kazini.

Tracey Emin

Tracey Emin, Uingereza

Msanii

Katika miaka ya 1990, Tracey Emin alipata umaarufu kwa michoro ya kichochezi kama vile Kitanda Changu na Hema, ambayo iliwafanya watu kutafakari kuhusu maisha yao ya kimapenzi.

Tangu wakati huo amakuwa jina tajika katika ulimwengu wa sanaa ya uchoraji duniani, akisifiwa kwa mtindo wake wa kipekee wa uchoraji.

Sasa ni miaka 25 tangu kitanda changu kilipoangaziwa mara ya kwanza kwenye onyesho la London na lililoibua mjadala. Emin ambaye wakati mmoja alikejeliwa kama mchoraji mbaya zaidi wa Uingereza, mwaka huu ametambuliwa na Mfalme Charlse kwa mchango wake katika sanaa.

Msanii huyo amefungua Wakfu wa Tracey Emin jini Margate, Uingereza, kuwakuza vipaji vinavyoibuka.

Kuwa mwanamke sasa hivi, nafikiri tunahitaji kuwa na ukakamavu kadiri ya uwezo wetu...Nadhani huu ni wakati ambao tunahitaji zaidi kuwa na umoja na harakati zaidi za kuwapigania wanawake.

Tracey Emin

Shin Daewe

Shin Daewe, Myanmar

Muandaaji Filamu

Mtengezaji filamu aliyeshinda tuzo Shin Daewe alikamatwa alipopatikana na ndege isyo na rubani ndani ya mizigo yake.

Alifunguliwa mashitaka mwaka huu katika taifa lala Myanmar inayoongozwa na jeshi, kutuhumiwa kwa kukiuka sheria za kukabiliana na ugaidi. Katika mahakama iliyoendesha kesi yake faraghani alizuiwa kifungo cha maisha. kuwa na mwakilishi wa kisheria na kuhukumiwa

Muandaji filamu huyo amepinga utawala wa kijeshi tangu mwaka 1988 sio mgeni katika visa vya kuzuilwa.

Ameongoza makumi ya filamu fupi, baadhi ya hizo zikivutia kimataifa ikiwa ni pamoja na filamu yake yamwaka 2007 inayoangazia maandamano ya kupigania democrasia, ambapo maelfu ya watawa wa Kibudha walijiungana maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi.

Nadia Murad

Nadia Murad, Iraq

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel

Nadia Murad, mshini wa tuzo ya Amani ya Nobel. sasa ni mwanaharakati anayepigania haki ya wahanga wa unyanyasaji wa kingono na ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyofanywa na kundi linalojiita Islamic State( IS) mwaka 2014

Alitekwa na wanamgambo wa IS, kugeuzwa kuwa mtumwa na kufanyiwa uovu wa kila aina ikiwa ni pamoja na ubakaji. Murad alifanikiwa kutoroka baada ya miezi mitatu. Tangu wakati huo amekuwa akifahamisha ulimwengu madhila aliyopitia ili kuhamasisha jamii kuhusu unyanyasaji wa kingono unaotokana na mizozo.

Alishirikiana na wakili wa kutetea haki za binadamu Amal Clooney kuiwajibisha IS na kuzindua mkakatiti wa Nadia kusaidia jamii kuanza umya maisha na kuwaombea fidia wale walionusurika.

Miaka 10 baada ya mauaji ya Yazidi, Murad anaendelea kuwa inaendelea ishara ya ustahimilivu

Lazima tutumie kile ninachokiita 'silaha ya roho' kupigania usawa na haki: ukweli, matumaini na huruma.

Nadia Murad

Cristina Rivera Garza

Cristina Rivera Garza, Mexico/Marekani

Mwandishi

Mwandishi mahiri Cristina Rivera Garza amejishindia tuzo tofauti kwa miaka kadhaa ikiwemo ile ya Pulitzer 2024 katika kitengo cha kumbukumbu kupitia kitabu chake Liliana's Invincible Summer kilichoangazia masuala ya mauaji dhidi ya wanawake.

Kupitia kisa cha dada yake- aliyeuawa nchini Mexico na mpenzi wake wa zamani katika miaka ya 1990 - mwandishi anaangazia jinsi ya kukabiliana na majonzi ya kumpoteza mtu wa karibu na safari ya kutafuta haki katika nchi ambayo ina viwango vya juu vya mauaji ya wanawake duniani.

Rivera Garza pia ni mwanzilishi na mwenyekiti wa Mpango wa PhD katika uandishi wa ubunifu nchini Uhispania katika Chuo Kikuu cha Houston.

Kuvuruga na lugha kila mara ili hatimaye lugha iweze kuwasilisha upande wa wanawake katika hadithi inaweza kuweka msingi wa ustahimilivu wa aina yoyote.

Cristina Rivera Garza

Fauzia al- Otaibi

Fauzia al- Otaibi, Saudi Arabia/Uingereza

Mpigania haki za wanawake

Akitumia mitandao ya kijamii kupaza sauti yake isikike, Fawzia al-Otaibi kwa muda mrefu amekuwa akifanya kampeni ya kukomesha mfumo wa malezi ya wanaume nchini Saudi Arabia.

Lakini baada ya mamlaka kuhoji hatua yake, aliamua kukimbia nchi.

Dadake Manahel al-Otaibi - pia mwanaharakati wa haki za wanawake - alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 11 gerezani mapema mwaka huu, baada ya kukutwa na hatia ya mashtaka yanayohusiana na mtindo wake wa mavazi na maoni aliyokuwa ametoa mtandaoni, kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Al-Otaibi amefanya kampeni bila kuchoka kushinikiza kuachiwa kwa dadake. Ukandamizaji wa hivi majuzi dhidi ya wapinzani umesababisha watu wengi kufungwa nchini Saudi Arabia kwa kuchapisha matukio katika mitandao ya kijamii.

Annie Sananduku Mwange

Annie Sananduku Mwange, Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo

Mchimbaji madini

Annie Sananduku Mwange, kama mwanamke wa Congo anayejishughulisha na biashara ya madini, anaongoza vuguvugu la mashinani la kutetea usawa na kukabiliana na unyanyasaji wa kingono katika sekta ya madini, ambayo nusu ya wanaofanya kazi katika migodi ni wanawake.

Kama kiongozi wa kitaifa wa Mtandao wa Wanawake Wachimbaji madini Renafem, anajiita 'mere boss', au mama boss, akiwaweka wanawake kuongoza maeneo ya migodi kama njia ya kuzuia unyanyasaji wa kingongo kutoka kwa wenzao wanaume.

Kwa kuwekeza kwa wanawake anatumia kupunguza ajira ya watoto migodini huku uhitaji wa madini ya cobalt ukiongezeka duniani kutokana na haja ya kukuza kawi safi kupitia bidhaa kama magari ya umeme.

Linda Drofn Gunnrsdottir

Linda Drofn Gunnrsdottir, Iceland

Msimamizi wa makazi ya wanawake

Linda Drofn Gunnrsdottir, anaendesha Makazi ya Wanawake waliolazimishwa kutoroka makwao kutokana na unyanyasaji wa kinyumbani nchini Iceland.

Iceland ni nchi ambayo inaongoza kwa kuwa ''mahali salama kwa wanawake'', lakini ghasia zinazohusiana na unyanyasaji wa kinyumbani zimeendelea kuwa juu.

Kama msimamizi mkuu wa kituo hicho, anaongoza mradi ambao utachangia kufungua nafasi mpya kwa Iceland kujenga makazi maalum kwa wanawake

Drofn Gunnarsdottir anasema miaka 20 iliyopita, 64% ya wanawake waliyoishi katika makazi hayo hatimaye walirejea kwa wanyanyasaji wao, lakini idadi hiyo ilishuka kwa 11% baada ya huduma kuboreshwa.

Anat Hoffman

Anat Hoffman, Israel

Mwanaharakati wa kidini

Anat Hoffman amepigania usawa wa kijisia na ujumuishwaji wa kidini ndani ya dhebebu la Kiyahudi kwa miongo kadhaa.

Ni mwanachama mwanzilishi wa kundi la Women of the Wall, ambalo linatetea usawa wa kuabudu kwa wanawake wa Kiyahudu katika Ukuta wa Magharibi katika mji wa kale wa Jerusalem. Kwa miaka kadhaa amepinga sheria zinazowazuia wanawake kujifunika nguo za sala na kusoma pamoja katika Torah.

Hoffman pia amehudumu kwa miaka 20 kamaMkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kituo cha Israel Religious Action, kitengo cha sheria kinapigania mageuzi na kuimarisha haki ya kijamii.

Kabla ya hapo, alikuwa mwakilishi katika Baraza la Mji wa Jerusalem ambapo alipinga sera zinazokandamiza haki.

Silvan Santos

Silvan Santos, Brazil

Mwanabiolojia

Mwanabiolojia Silvana Santos anahusisha ugunduzi wake mahiri katika fani ya jeni na bahati- alikutana na familia ambayo inakabiliwa na ugonjwa usojulikana katika kila mtaa aliyoishi.

Alifanikiwa kugundua ugonjwa wa SPOAN( soastic paraplegia, optic atrophy, and neuropathy), aina isiyo ya kawaida ya ugonjwa unaoathiri jeni na kuwafanya watu kupooza katika eneo la kaskazini- mashariki mwa Brazil.

Ndani ya miaka 20 tangu alipoanza kufanya utafiti katika mji wa Serrinha dos Pintos, Santos amewasaidia wakazi walioathirika na hali hiyo kupata utambuzi muhimu.

Anachunguza kutokea kwa magonjwa adimu ya kijeni na usiano wa magonjwa hayo na ndoa kati ya watu ambao wana uhusiano wa karibu katika maeneo masikini ya vijijini huko Brazil.

Je, tunaonyeshaje nguvu ya ustahimilivu? Kutambua kuwa maisha ni mzunguko. Tunaieshi hata katika mazingira makali ya ukame. Katika msimu wa mvua tunastawi na kupanda miti ya matunda,

Silvan Santos

Gisele Pelicot

Gisele Pelicot, Ufaransa

Manusura wa ubakaji na mteteaji

Kwa kuondoa haki yake ya kutokujulikana na kuruhusu hadithi yake kufikia ulimwengu, Gisèle Pelicot amekuwa ishara ya ujasiri na uthabiti.

Mumewe wa zamani amekiri kumtumia dawa za kulevya na kumbaka walipokuwa kwenye ndoa, na kuwaajiri wanaume wengine kadhaa pia kumbaka. Mengi ya madai ya ubakaji yalirekodiwa.

Kwa mujibu wa sheria, Pelicot alikuwa na haki ya kutotajwa jina, lakini badala yake aliomba kesi ifanyike hadharani na video zionyeshwe, kwa nia ya kurelekeza "aibu" kwa mshtakiwa. Baadhi ya wanaume wengine 50 waliohusika katika kesi hiyo wamekiri kumbaka, lakini wengi wanasema walishiriki tu katika vitendo vya ngono.

Wakati kesi inafikia hatua yake ya mwisho, wanawake kote ulimwenguni wametiwa moyo na bibi huyu Mfaransa, ambaye anatumai kesi yake itabadilisha sheria na mitazamo ya Ufaransa kuhusu ubakaji na ridhaa.

Kasha Jacqueline Nabagesera

Kasha Jacqueline Nabagesera, Uganda

Mwanaharakati wa Utofauti na ushirikishwaji

Uhusiano wa jinsia moja umeharamishwa nchini Uganda na adhabu yake ni kifungo gerezani- Mwanaharakati wa kutetea haki za LGBTQ+ Kasha Nabagesera anapigania kubadilisha sherea hizo kandamizi.

Kama mwanamke anayejitambulisha wazi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja, amepambana vilivyo kufanya kampeni ya kukomesha unyanyapaa dhiddi ya kumuia ya LGBTQ+ kote Afrika.

Nabagesera amefanikiwa kushitaki magazeti na serikali ya Uganda kwa kuendekeza ubaguzi dhidi ya LGBTQ+: amepinga mara mbili sheria zinazopinga mapenzi ya jinsia moja katika mahakama za Ugand na kwa sasa anapinga sheria ya 2023.

Safari yake ya elimu inajumuisha shahada ya masuala ya biashara kutoka Chuo Kikuu cha Nkumba nchini Uganda, ushirika wa kimasomo kutoka Chuo Kikuu cha Stanford na kuchangia mipango mbali mbali katika majukwa ya ngazi ya juu katika Umoja wa Mataifa, Bunge la Ulaya na Tume ya Afrika.

Maheder Haileselassie

Maheder Haileselassie, Ethiopia

Mpiga picha

Kufanya kazi katika maeneo ambayo mito imekauka na mimea kupungua, mpiga picha Maheder Haileselassie anaangazia jinsi ukame mbaya ulivyozilazimu familia katika nchi yake kuwaoza binti zao wadogo, hatua ambayo imemuwezesha kushinda tuzo ya mwaka 2023 ya Contemporary African Photography Prize.

Mashiriki ya kutetea haki za binadamu yanatarajia idadi ya wasichana wanaokabiliwa na hatari ya kuozwa wakiwa wadogo kutokana na mgogoro wa hali ya hewa itaongezeka kwa thauluthi moja kufikia mwaka 2050.

Upigaji picha wa Haileselassie umechochewa na historia na hali wanazopitia watu anaotangamana nao kila siku na pia maisha yake mwenyewe.

Kazi yake imeonyeshwa katika maeneo mengi ya kifahari ikiwa ni pamoja na katika onyesho la mwaka huu la African Biennale of Photography.

Angela Rayner

Angela Rayner, Uingereza

Naibu Waziri Mkuu

Angela Rayner aliteuliwa naibu waziri mkuu kufuatia uchaguzi mkuu wa mwezi Julai na hatimaye kushikilia wadhifa wa ngazi ya juu katika siasa za Uingereza,

Alizaliwa na kulelewa mjini Stockport.Ryner amekuwa akimtunza mama yake tangu akiwa mdogo alipoacha shule kutokana na ujauzito akiwa na umri wa mika 16. Alifanya kazi kama mhudumu wa kijamii katika baraza la mitaa na kupanda ngazi hadi kuwa mwakilishi wa chama cha wafanyakazi

Rayner alichaguliwa mara ya kwanza kama Mbunge wa chama cha Labour wa eneo bunge la Ashton-under-Lyne mwaka 2015- mwanamke wa kwanza kuwakilisha eneo bunge- na baadaye kuhudumu kama waziri kivuli wanawake na usawa miongoni mwa nyadhifa zingine.

Kwa sasa anahudumu kama waziri wa ndani wa masuala ya makazi,jamii na serikali za mitaa

Harbia Al Himiary

Harbia Al Himiary, Yemen

Mhandisi wa uhifadhi wa urithi

Huku majengo mengi yenye umuhimu wa kihistoria yakiharibiwa baada ya miaka mingi ya vita nchini Yemen, mhandisi Harbia Al Himiary alianza kazi ya kuyakarabati upya.

Akishirikiana na mashirika mengine kama vile Unesco, amekarabati makumi ya majengo ya makazi na urithi huko Old Sana’a na kote nchini. Unesco imechunguza uharibifu katika maeneo zaidi ya 16,000.

Kazi yake katika uwanja wa uhifadhi wa urithi haijaangazia maeneo ya kihistoria pekee bali pia imeimarisha ubora wa maisha ya watu wengi.

Al Himiary pia imetoa mafunzo kwa wakazi wa eneo hilo katika ufundi wa jadi wa ujenzi na kuwahimiza wasichana wachanga kuingia katika tasnia hiyo.

Maria Teresa Horta

Maria Teresa Horta, Ureno

Mshairi

Mwandishi na mwanahabari Maria Tesa Horta ni mmoja wa wanawake mashuhuri nchini Ureno na mwandishi aliyeandika vitabu vilivyoshinda matuzo kadhaa, lakini anajulikana zaidi kimataifa kama mwandishi mwenza wa tamthilia ya Novas Cartas Portuguesas( New PortugueseLetters).

Mkusanyiko wa vitabu vya tamthilia, ushairi na vitabu vinavyoangazia hisia za kimapenzi ulipigwa marufuku mwaka 1972 na utawala wa kimabavu. Horta na mwandishi mwenzake walishtakiwa kwa kuandika uchafu na ''kutumia vibaya uhuru wa vyombo vya habari''.

Kesi ya Maria watatu, kama ilivyojulikana, iligonga vichwa vya habari na kuhamasisha maandamano kote duniani.

Kesi hiyo ilimalizika baada ya mapinduzi ya Carnation ya mwaka 1974 kuondoa utawala huo- mwaka huu ni maadhimisho ya mwaka wa 50 wa tukio hilo la kihistoria.

Lesley Lokko

Lesley Lokko, Ghana/ Uingereza

Msanifu mijengo

Juhudi zake za ''kuleta demokrasia katika fani ya usanifu mijengo'' imemuwezesha Lesley Lokkonkupata medali ya dhahabu kutoka Taasisi ya Royal British Architects 2024- moja ya tuzo ya juu zaidi katika fani yake na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kupokea tuzo hiyo kutoka taasisi hiyo ilipoanzishwa mwaka 1848.

Amepigania kuwaleta watu kutoka maeneo ambayo hayajawakilishwa vyema katika fani yake kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Msomi huyo wa Ghana- Uskochi pia alikuwa mwanamke wa kwanza menye kizazi cha Afrika kuanzisha usanifu mjengo wa Venice Biennale, ambapo anaangazia mada za decarbonisation(kuhama kutoka kwa utumizi wa mafuta ya kisikukuu hadi mkaaw a mawe) na dicolonisation (mchakato wa kupatia uhuru mataifa yaliyoongozi wa na wakoloni)

Ni muanzilishi wa Taasisi ya African Futures mjini Accra ambayo inaangazia uhusiano kati ya usanifu mijengo, utambulisho na rangi.

Ustahamilivu ni uwezo wa kuendelea kupambana hata ukikabiliwa na changamoto, ambayo mara nyingi huwa vigumu kuvumilia.

Lesley Lokko

Aruna Roy

Aruna Roy, India

Mwanaharakati wa kijamii

Aruna Roy, mpiganiaji haki za watu maskini nchini India akiachakazi yake katika utumishi wa umma ili kujishughulisha moja kwa moja na jamii katika maeneo ya mashambani.

Alianzisha shirika la mashinani Mazdoor Kisan Shakti Sangathan(MKSS), ambayo inaangazia uwazi na mishahara ya haki. Imekuwa kiungo muhimu katika kutunga sheria ya kihistoria ya mwaka 2005 inayowawezesha wananchi kudai uwajibikaji wa serikali.

Kwa zaidi ya miongo minne, Roy amekuwa mstari wa mbele wa mikakati inayoongozwa wa wananchi, hatua ambayo ilimfanya kupata matuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya Ramon Magsaysay ambayo inajulikana kama 'Tuzo ya Nobel ya Asia'.

Ni rais wa Shirikisho la Kitaifa la Wanawake wa Kihindi na mwaka huu alitoa kitabu cha kwa jina, The Personal is Political ambacho kinaangazia maisha yake.

kwa kuzingatia muundo mzuri, mara nyingi tunashindwa kutambua ndoto ya karibu

Aruna Roy

Yumi Suzuki

Yumi Suzuki, Japan

Mlalamishi katika kesi ya kulazimishwa kufunga uzazi

Yumi Suzuki aliezaliwa na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo, alikabiliwa na unyanyapaa tangu akiwa na umri mdogo. Akiwa na umri wa miaka 12 alifanyiwa hysterectomy, utaratibu wa upasuaji wa wa kufunga kizazi.

Kuanzia miaka ya1950 hadi 1990, baadhi ya watu waliokuwa na ulemavu kama Suzukiwalifungwa kizazi kwa nguvu nchini Japan ktutokana na sheria ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1996.

Suzuki na walalamishi wengine 38 waliishitaki serikali, na baada ya mchakato mrefu wa sheria mahakamani hatimaye alishinda kesi yake. Mnamo mwezi Julai Mahakama ya Juu Zaid ya Japan iliamua kwamba utaratibu huo ulienda kinyume na katiba na kuiamuru serikali kuwalipa fidia wathiriwa.

Mamlaka imekiri kuwa wa16,50 walifungwa kizazi bila ridhaa yao.

Einav Zangauker

Einav Zangauker, Israel

Mwanaharakati wa kutetea kuachiwa kwa mateka

Mwanaharakati na mama yake Matan mwenye umri wa miaka 24,Einav Zangauker alitekwa nyara katika mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas tarehe 7 Oktoba. Mwenza wa mwanawe wa kiumbe Ilana walitekwa katika tukio lingine na kurejeshwa nyumbani katika mpango wa kubadilishana wafungwa.

Tangu wakati huo ameendelea kuangazia mzozo wa mateka, akiwataka viongozi kuchukua hatua na kuhamasisha maandamano ya kila wiki.

Zangauker amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Israel kwa kushindwa kutafuta njia ya kuwarejesha mateka nyumbani, ingawa alikipigia kurachama tawala cha Waziri Mkuu Benjamin.

Anataka makubaliano ya kusitisha mapigano yafikiwe ili mateka waliosalia waachiwe huru.

Feng Yuan

Feng Yuan, China

Mtetezi wa haki za wanawake

Mtetezi wa muda mrefu wa haki za wanawake nchini China, Feng Yuan ni mkurugenzi mwanzilishi wa Equality Beijing. Shirika hilo lililoanzishwa mwaka 2014 linajishughulisha zaidi na masuala ya mageuzi ya sheria, kujenga uwezo na kukabiliana na ukatili wa kijinsia kupitia simu ya msaada.

Katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa akiwasaidia wahanga wa MeToo wa China na kutoa mafunzo kwa waajiri kuzuia unyanyasaji wa kingono katika mazingira ya kazi.

Feng alifanya kazi kama mwanahabari akijikita zaidi katika masuala ya wanawake kuanzi mwaka 1986 - 2006

Tangu katikati ya miaka ya 1999, alisaidia kuanzisha mikakati kadhaa isiyokuwa ya kiserikali kuhusu wanawake na vyombo vya habari, HIV/Ukimwi, uongozi, na kuwawezesha vijana. Ameandika na kuhariri machapisho ndani na nje ya China.

Amanda Zurauwski

Amanda Zurawski, Marekani

Mtetezi wa Haki za afya ya uzazi

Mwezi Agosti 2022, Amanda Zurawski aligundua maji yake ya uzazi yametoka kabla ya muda wake wa kijfungua. Madaktari walimwambia mtoto wake hataponea.

Zurawski anaishi Texas, na alinyimwa haki ya kutoa mimba. Baada ya Mahakama ya Juu zaidi kubatilisha uamuzi wa kesi ya iliyowasilishwa na Roe v Wade miezi miwili kabla ya jimbo hilo kupiga marufuku utoaji mimba hadi pale maisha ya mama yako hatarini. Siku tatu baadaye alipatwa na mshtuko na kwa kuwa maisha yake yalikuwa hatarini hatimaye alipewa idhini ya kutoa mimba.

Machi 2023, Zurauski na wanawake 19 waliojipata katika hali kama hiyo waliwasilisha kesi mahakama dhidi ya jimbo hilo- kesi ya kwanza ya wanawake walionyimwa haki ya kuavya mimba tangu kubatilishwa kwa uamuzi wa kesi ya Roe v Wade. Mahakama ya Juu zaidi ya Texas ilitupilia mbali kesi ya kupinga marufuku ya uaviaji mimba.

Sasa anaapa kuendelea kupigania ''kurejesha na kulinda haki za uzazi nchini''.

Jahana Bahamon

Jahana Bahamon, Colombia

Mwanaharakati wa kijamii

Ziara ya gereza ya Colombia ilibadilisha maisha ya muigizaji Johana Bahamon, ilimchochea kuwafanyia kazi wale wanaohitaji ''fursa ya pili'.

Mwaka 2012 aliachana na taaluma yake ya uigizaji na kugeukia mageuzi ya gereza na kuanzisha Wakfu wa Accion Interna, shirika lisilo la kiserikali linalosaidia wafungwa wa Colombia walioachiwa huru.

Wakfu huo unaripotiwa kufikia zaidi ya watu 150,000 na vituo 132 vya kuwashikilia watu kote nchini.

Mwanaharakati huyo wa kijamii pia alikuwa mhamasishaji wa sheria ya kutoa nafasi ya mwaka 2022,inayofahamika kama muswada wa Johanna Bahamon, ambao ulianzisha mpango wa kutoa takrima ya kuimarisha ufikiaji wa ajira na masomo kwa watu waliachiwa kutoka gerezani.

Kuwa mstahamilivu ni zaidi ya kuendelea mbele na maisha baada ya kupitia kipindi kigumu: ni kufanya uamuzi wa kubadilisha changangamoto kuwa fursa ya kujiendelea kimaisha.

Jahana Bahamon

Rosemarie Wydler- Walti

Rosemarie Wydler- Walti, Uswizi

Mwalimu na mwanaharakati wa hali y ahewa

Kama rais mwenza wa KlimaSeniorinnen- au Wanawake wakuu wanaolinda hali ya hewa- Rosmarie Wydler- Walti aliongoza mapambano ya kisheria ya miaka tisa dhidi ya serikali ya Uswizi kati Mahakama ya Ulaya ya Kutetea Haki za Binadamu

Huku kukiwa na wanawake wengine 2,000, walimu wa chekechea wa kuwakilishwa wakili Wydler Walti alihoji jinsi serikali ya Uswizi ilivyoshughulikia hali ya joto kali iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi akiongeza kuwa ilihujumu haki ya kuwa na afya, na kwamba umri na jinsia yao hasa inawaweka katika hali hatarishi.

Mnamo mwezi Aprili mahakama iliamua kuwa juhudi za nchi za kupunguza uzalishaji wa hewa chafu haija

Ingawa bunge la Uswizi baadaye lilipinga uamuzi huo, kesi hiyo iliweka mfano wa jinsi ya kushughulikia kesi za masuala ya hali ya hewa.

Sharon Kleinbaum

Sharon Kleinbaum, Marekani

Rabbi

Mwanzilishi wa jumuiya LGBTQ+ miongoni mwa Wayahudi huko New York, rabi Sharon Kleinbaum ametumia miongo mitatu kuleta mabadiliko katika makutano ya haki na dini.

Aliteuliwa mwaka wa 1992 kama rabi wa kwanza wa kike wa Usharika wa Beit Simchat Torah, ameongoza jamii kupitia heka heka - ikiwa ni pamoja na janga la Ukimwi katika miaka ya 1990.

Alisimamia upanuzi wa washiriki wa kutaniko hilo ili kujumuisha watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, na sasa inaaminika kuwa sinagogi kubwa zaidi la LGBTQ+ nchini Marekani.

Kleinbaum, ambaye alistaafu mwaka huu, amekuwa akiongoza miradi ya haki za kijamii na aliteuliwa kujiunga na Tume ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini ya Marekani na Rais Joe Biden.

Furaha ni kitendo cha upinzani wa kiroho na kisiasa.

Sharon Kleinbaum

Shilshila Acharya

Shilshila Acharya, Nepal

Mjasiriamali wa Uendelevu

Shilshila Acharya anaendesha mojawapo wa mtandao mkubwa wa kuchakata plastiki nchini Nepal. Biashara yake ya usimamizi wa taka Avni Ventures inaajiri wafanyakazi kutoka jamii zilizotengwa na inalenga kuwajumuisha wanawake zaidi katika sekta ya kijani.

Acharya alikuwa kiungo muhimu katika kampeni ya mwaka 2014 ya 'No Thanks, I Carry My Own Bag, ambayo ilichangia kupigwa marufuku kwa utumiaji wa mifuko ya plastiki.

Mwalimu huyo anayehamasisha masuala ya hali ya hewa na jinsi ya kushughulikia taka pia anajihusisha mpango wa usafi wa kila mwaka katika eneo la Himalayas kuondoa taka zilizoachwa na wakweaji milima, kuokota jumla ya tani 119 za taka tangu 2019.

Kupitia juhudi zake baadhi ya taka hizi hutumiwa tena wanawake mafundi wa kiasili kutengeneza vikapu, mikeka na vito ili kujikimu kimaisha.

Shireen Abed

Shireen Abed, Maeneo ya Palestina

Daktari wa watoto

Mashambulio ya mabomu na kukosa raslimali hakukumzuia Shireen Abed kuwatunza watoto wachanga mjini Gaza.

Alitoroka nyumbani kwake mwanzoni mwa vita Israel na Gaza mwaka 2023 baada ya jengo la ghorofa alilokuwa akiishi ndani kuharibiwa. Lakini mtaalamu huyo wa watoto aliendeleakuwatunza watoto wachanga katika kambi ya wakimbizi.

Akitumia tajriba yake ya miaka kadhaa katika uangalizi wa watoto wachanga katika hospitali kuu ya watoto huko Gaza- hivi karibuni zaidi kama mkurugenzi wa kitua cha wanawake kujifungua cha Al Shifaa- alianzisha sehemu ya dharura ili kuwawezesha wahudumu wa afya kutoa tiba hali ya dharura kwa kutumia raslimali kidogo, na kuwafunza madaktari wengine.

Hali ngumu ilimlazimu kuondoka Gaza pamoja na binti zake wawili mapema mwaka huu, lakini Abed anaendelea kuwasaidia madaktari walio nyanjani kutoka mahali alipo.

Olivia McVeigh

Olivia McVeigh, Uingereza

Mrembuaji

Baada ya kupatikana na ugonjwa wa alopecia, Olivia Mc Veigh alianza kuvalia wigi. Katika harakati za kijaribu mitindo tofauti na kutumia nywele mbadala, alianzisha jukwaa la kuwatia moyo na kuwahamasisha wanawake wanaokabiliwa na tatizo la kupoteza nywele.

Akiwa na wafuatiliaji nusu milioni, amefanya uvaliaji wigi kuwa jambo la kawida huku akiendelea kuhamasisha jamii kuhusu alopecia na afya ya wanawake.

McVeigh, mrebuaji na mshawishi kutoka Ireland Kaskazini, alianza kupoteza nywele zake katika miaka yake ya ujanani.

Sasa anaandaa warsha ya wigi na kusimulia safari yake ya maisha kwa ujasiri, na kutoa jukwaa salama kwa wanawake walio na alopecia kuja pamoja na kujadiliana kuhusu hali inayowakabili.

Ustahamilivu ni taji ambalo sisi wanawake tunavalia. Tunaweza kupokea, kubadilisha na kujifunza kustawi katika mazingira , bilatuliyo nayo bila kujali hali inayotukabili.

Olivia McVeigh

Safa Ali

Safa Ali, Sudan

Mkunga

Wakati mapigano makali yalipozuka katibu na hospitali ya Sudan mwaka jana, Dkt Saafa Ali alikataa kuondoka na kuwaacha wafanyakazi wenzake licha ya mashambulio ya mara kwa mara.

Kwa sasa anahudumu katika Hosipitali ya AI Saudi ya wanawake ya kujifungua na anafanya upasuaji na kutibu magonjwa wanawake yanayohusiana na masuala ya kizazi katika mazingira ya mzozo unaoendelea.

Pia anaendelea kuwafunza karibu madaktari 20 waliohitimu katika masuala ya uzazi ili kukabiliana na suala la upungufu wa wahudumu wa kimatibabu.

Naamini kuwa kupitia upinzani wa wanawake kuna matumaini ya uponyaji,haki na siku zijazo ambapo hatutahitaji tena kuishi kwa hofu. Ni ustahamilivu wao ndio unanikumbusha bado matumaini bado yapo hata katika mazingira magumu zaidi.

Safa Ali

Roxy Murray

Roxy Murray, Uingereza

Mwanaharakati wa kutetea haki za ulemavu

Kuzungumzia wazi kuhusu muelekea wake wa kijinsia kama mtu anayeishi na hali ya Sclerosis, Roxy Murray anatumia jukwa lake kuwahamasisha watu wanaougua magonjwa hatari na changamoto wanazopitia linapokuja suala la ujumushwaji katika sekta ya tiba, misaada na ushirika.

Uanaharakati wa Murray hutumia historia yake katika mtindo, kuwasaidia watu wenye ulemavu kufanya shughuli zao za kila siku kwa mtindo na kukuza mwonekano wa watu wenye ulemavu kutoka kwa makundi ya wachache na makabila tofauti.

Ni mwanzilishi wa podcast ywa The Sick and Sickening, ambayo inashiriki hadithi zisizochujwa kuhusu kuishi na ulemavu na ugonjwa kuanzia udhibiti wa maumivu hadi afya ya uzazi.

Kama mwanamke mwenye ulemavu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja, ustahamilivu ni suala la kibinafsi sana kwake. Inahusu uwezo wa kuhoji mifumo ambayo imewatenga watu kama mimi.

Roxy Murray

Rikta Akter Banu

Rikta Akter Banu, Bangladesh

Muuguzi na muanzilishi wa shule

Katika kijiji cha mashambani kaskazini mwa Bangladesh ambako muuguzi Rikta Akter Banu anaishi, kuwa na mtoto mwenye ugonjwa ua mlemavu ni laana.

Wakati binti yake, ambaye alikuwa anaugua ugonjwa wa celebral palsy, alipozuiliwa kujiunga na shule ya msingi , aliamua kuuza kipande chake cha ardhi kujenga shule yake mwenyewe.

Shule ya walemavu ya Akhter Banu sasa ina wanafunzi 300 na imebadili mtazamo wa jamii kuhusiana na ulemavu.

Ingawa shule hiyo awali ilijengewa watoto walio na ulemavu wa kusoma, sasa inawahudumia vijana wadogo walio na ulemavu wa aina tofauti.

Sara Berkai

Sara Berkai, Uingereza/ Eritrea

Mbunifu wa vifaa vya sayansi vya DIY kwa watoto

Sara Berkai, raia wa Eritrea aliyezaliwa Sudan na kulelewa mjini London alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kusoma hadi chuo kikuu ambako alisomea masuala ya watoto.

Ni mwanzilishi wa Ambessa Lay, kampuni ya mtandaoni ambayo hutengeneza vifaa vya elimu vya DIY za watoto, na kuwahimiza kushiriki katika utengenezaji wa vifaa vya kuchezea.

Berkai hutoa fursa kwa watoto ambao hawako shuleni kufikia elimu kupitia michezo. Alikuja na wazo hilo wakati alipokuwa akifunza katika warsha ya STEM kwa watoto waliofurushwa makwao katika mataifa ya Ethiopia na Eritrea mwaka 2019.

Wazo lake la ubunifu limetambuliwa kwa jina lake kujumuishwa kwenye orodha ya Jarida la Forbes ya 30 Under 30 kwa mchango wake katika jamii miongoni mwa sifa zingine.

Usthamilivu ni kufikia malengo kwa vitendo- kujitolea kufikia malengo mema maishani kwa kuzingatia upendo.

Sara Berkai

Brigitte Baptiste

Brigitte Baptiste, Colombia

Mwanaecolojia

Kama mtu aliyebadili jinsia, mwanabiolojia Brigitte anachunguza muundo wa kawaida kati ya bayoanuwai na utambulisho wa kijinsia.

Anatumia lenzi ya ajabu kuchanganua mandhari na viungo katika jitihada ya kupanua dhana ya 'asili' kuhusu mfumo bora wa ikolojia. Katika mazungumzo yake katika kipindi cha TEDx 2028 alitumia Quindio wax palm, mti wa kitaifa wa Colombia, kama mfano wa viumbe vinavyojulikana kubadili jinsia kutoka ile ya kiumme hadi ya kike katika maisha yake yote.

Kama msomi tajika, Babtiste alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya Alexander von Humboldt kwa miaka 10 na sasa anahudumu ka rais wa Chuo Kikuu cha EAN mjini Bogota, taasisi ya elimu ya juu inayojikita katika masuala ya ujasiriamali endelevu.

Pia ametetea watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTQ+ kupata ufadhili zaidi katika elimu ya juu.

Naomi Chanda

Naomi Chanda, Zambia

Mkulima na mkufunzi

Kama mwelekezaji wa kilimo na katika shamba la kufundishia Naomi Chanda ana dhamira ya kuifanya jamii yake kufanya kazi kwa kutumia mbinu za kuheshimu na kuhifadhi ardhi.

Anaangazia mbinu za kisasa za kilimo cha unyunyuziaji ambao unatumia maji kidogo kukuza mimia ambayo inakuwa kwa haraka- akiwatumia wanawake kupata suluhisho la changamoto inayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kupitia shirika la wasichana lisilo la kiserikali linalofahamika kama Camfed, Chanda anasaidia kuwafunza wanawake vijana 159 kukumbatia mbinu za kilimo ambazo zitawawezesha kukabiliana na migogoro ya hali ya hewa katika maeneo ya kaskazini magharibi ya Zambia, ambako kiangazi cha muda mrefu na kubadilika kwa ghafla kwa misimu ya kilimo kumewaathiri wakulima wadogo.

Rosa Vasquez Espinoza

Rosa Vasquez Espinoza, Peru

Biolojia ya kemikali

Kutokana na hekima ya bibi yake ambaye ni tabibu,mwanasayansi Rosa Vasquez Espinoza amejiunga na kazi yake ya kuchanganya maarifa ya sayansi na ya asilia ili kuhifadhi mabadiliko ya viumbe hai katika msitu wa Peru.

Kama mwanzilishi wa utafiti wa kimataifa wa Amazon,anafanya kazi kwa ushirikiano na jamii za kiasili ili kutambua masuala ambayo hayajaguswa katika msitu.

Akizuru katika mfumo wa ikolojia wa mashinani katika sayari,kazi ya Espinoza inajumuisha kutambua bakteria mpya katika mto ulio na joto wa zamani amazoni,na kuongoza uchambuzi wa kemikali ya kwanza ya nyuki wasio na sumu na asali ya dawa Peru.

Vile vile ni balozi wa kimataifa wa jamii ya Ashaninka ,kundi la asilia kubwa zaidi kusini Marekani.

Xuan Phuong

Xuan Phuong, Vietnam

Muelekezaji filamu, mwandishi na miliki wa nyumba ya sanaa

Xuan Phuong ambaye anakaribia kuadhimisha mwaka wake wa kuzaliwa wa 95 ana kila la kujivunia maishani mwake kama mwandishi na mwelekezi.

Ameshuhudia mara mbili vita vya Vetnam, na kupigania uhuru wa nchi yake kutoka kwa Ufaransa akiwa na umri wa miaka 16.

Baada ya kuhitimu kuwa daktari amekuwa mkuu wa kliniki, mwandishi wa vita na mwelekezaji filamu katika runinga ya Vietnam, na kushuhudia matukio ya kihistoria kama kuanguka kwa Saigon.

Akiwa na umri wa miaka 62, badala ya kustaafu, alianzisha nyumba ya sanaa ya Lotus- moja ya nyumba ya sanaa ya kibinafsi katika mji wa Chi Minh katika juhudi za kufahamisha ulimwengu kuhusu sanaa ya Wavietnam. Pia amewakuza wasanii wanaoibuka hatua ambayo imempatia umaarufu mkubwa.

Zhanylsynzat Turganbaeva

Zhanylsynzat Turganbaeva, Kyrgyzstan

Msimamizi wa Makavazi

kuhifadhi na kuhuisha urithi wa kitamaduni wa Krygstan ni kipaumbele cha Zhanylsynzat Turganbaeva.

Anaendesha makavazi mjini Bishkek, ambayo inaangazia vitu vya kisanaa vya kitaifa ambavyo vinavutia idadi kubwa ya wageni.

Sehemu ya kazi yake ya ufadhili inahusisha kuhifadhi fasihi ya Kyrgystan, ikiwa ni pamoja Epic of Manas ambaye inasimulia hadithi ya shujaa ambaye anasemekana aliunganisha makabila 40 katika eneo la Kyrgystan.

Toleo moja la shairi kuu lililoorodheshwa na Unesco lina takriban mishororo 5,000 ambayo bila shaka ni shairi refu zaidi duniani (mara 20 zaidi ya ile ya The Odyssey). Kazi ya Turganbaeva ni kutoa fursa na rasilimali kwa ajili ya 'Manschis', watumbuizaji mashairi haya ya Wakrygystan.

Gabriela Salsa Cabrera

Gabriela Salsa Cabrera, Mexico

Mtayarishi Progamu na mwanayayasi wa data

Lugha yake ya mama, Nahuati haikuwa kwenye jukwaa la Google la kufasiri lugha ambayo hutumiwa sana, hadi Gabriela Salas Cabrera alipoingilia kati.

Mhandisi huyu ameshirikiana na kampuni hiyo kubwa ya teknolojia katika miradi wa lugha kujumuisha hii na lugha zingine asilia za Mexico kwenye fasiri ya Google. Tafsiri ya Nahuati tayari imetolewa kwa umma mwaka huu.

Kazi ya Salasa hutumia uwezo wa Akili Mnemba (AI) ili kukuza lugha ambazo haziwakilishwi vilivyo, na pia kuimarisha uwepo wa wanawake wa kiasili katika tasnia ya teknolojia.

ni mtaalamu wa utayarishaji wa AI unaolenga kitu maalum, na anasomea sayansi ya data katika Chuo Kikuu cha Poitecnica, mjini Madrid, Uhispania.

Ustahamilivu kwa wanawake ni moto ambao hauzimiki, kugeuza maumivu kuwa motisha na kutoa mwangaza kwa wale wanaofuta.

Gabriela Salsa Cabrera

Dilorom Yudosheva

Dilorom Yudosheva, Uzbekistan

Mshonaji na mfanyabiashara

Miaka miwili iliyopita, Dilorom Yuldo alipoteza miguu yote miwili katika ajali ya kuvuna. Lakini hili halikumzua kuwa na ndoto kubwa.

Alitaka kujifunza ujuzi mpya huku akiwasaidia wanawake vijana wa Uzbekistan kujipatia kipato, kwa hivyo aliamua kuanzisha biashara yake ya ushonaji.

Alijifunza misingi ya ujasiriamali na usimamizi wa rasilimali na akaendelea kutoa mafunzo kwa zaidi ya wanafunzi 40. Ndani ya miezi kadhaa, kampuni yake ilikuwa kwa kasi ya haja kiasi cha kuweza kuandaa warsha za bila malipo na kupata kandarasi ya kushona sare za wafanyakazi na watoto wa shule.

Biashara yake sasa imekuwa chanzo cha mapato kwake na kwa makumi ya wanawake wengine.

Raye

Raye , Uingereza

Mwimbaji

Mwimbaji-mtunzi wa nyimbo Raye aliweka historia katika Tuzo za Brit za mwaka huu, na kushinda tuzo sita kati ya saba alizoteuliwa na kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushinda mtunzi bora wa mwaka.

Mnamo 2021, Raye aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba alikuwa kwenye vita vya miaka saba na lebo yake ya rekodi ya Polydor kutoa albamu yake mwenyewe.

Aliwasilisha albamu yake ya kwanza ya studio My 21st Century Blues kama msanii huru mnamo 2023, kwa mafanikio muhimu na ya kibiashara.

Amezungumza kwa uwazi kuhusu matatizo ambayo amekumbana nayo katika tasnia ya muziki na nje, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, matatizo ya afya ya akili, na amewahi kushinikiza malipo ya haki kwa watunzi wa nyimbo.

Nour Emam

Nour Emam, Misri

Mjasiriamali Fem-tech

Mwalimu wa afya ya ngono, Nour Emam anaangazia mada kama usafi wa hedhi, aafya ya uzazi na ufahamu wa ngono, masuala ambayo yanadaiwa kuwa mwiko kujadiliwa na wanawake katika maeneo ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Emam ni mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mtendaji wa Motherbeing, kampuni ya kiteknolojia (ya wanawake) ambayo hutoa huduma kupitia kliniki ya Cairo na jukwaa la kijiditali, kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya kupitia teknolojia.

Ana azi,ia kuwawezesha wanawake kupata uelewa kuhusu miili yao, huku akitoa maelezo ya kweli mbinu za uzazi wa mpango na kuwasaidia kujadili masuala hayo muhimu bila uoga au kuona haya.

Rebeca Andrade

Rebeca Andrade, Brazil

Mchezaji wa mazoezi ya viungo

Rebeca Andrade ameshinda jumla ya medali sita ambazo zimemfanya kuwa mwanaolimpiki wa Brazil aliyepata medali nyingi zaidi (pia ana medali tisa za mashindano ya dunia)

Alishinda mazoezi ya sakafuni katika michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, na kumpiku mchezaji Simone Biles ambaye ameshinda medali nyingi zaidi duniani. Wakati wa sherehe ya kuvishwa medali, Biles na mchezaji mwenzake wa Marekani Jordan Chiles walitoa heshima zao kwa Mbrazili huyo, ishara ambayo ilipata umaarufu mitandaoni na kuwa nembo ya Olimpiki ya mwaka huu.

Ni mmoja kati ya ndugu zake wanane, na mpaka alipotimiza umri wa miaka 10 alikuwa akitembea kuenda mazoezini kutoka nyumbani kwao viungani mwa mji wa Sau Paulo, huku mama yake akifanya kazi za ndani kulipia mazoezi yake.

Juhudi zake zimemuwezesha kuhimili majeraha mengi aliyopata na amekuwa akizungumzia wazi wazi kuhusu umuhimu wa kupatia kipaumbele suala la afya ya akili.

Kuwa mstahimilivu kunahusiana na jinsi tunavyoshughulikia mambo yanayotupata na kuwasaidia wenzetu kuona mazuri hata wakati mambo ni mabaya sana.

Rebeca Andrade

GeorginaLong

GeorginaLong, Australia

Ekolojia ya matibabu

Kupitia matibabu maalum, ekolojia ya kinga Georgina Long anataka kufikia ulimwengu usio na vifo vya saratani.

Kama Mkurugenzi mwenza katika Taasisi ya Melanoma nchini Australia, Long alipata umaarufu mnamo 2024 baada ya kutengeza tiba ya kwanza duniani ambayo ilimsaidia daktari mwenzake na rafiki yake, Richard Scolyer kuishi bila ugonjwa baada ya kupata aina fulani ya saratani ya ubongo.

Long na kundi lake, ikiwa ni pamoja na mgonjwa mwenyewe- waligundua kuwa tiba ya kinga ilifanya kazi vyema wakati mchanganyiko wa dawa inapotumiwa kabla ya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo.

Tiba yao ya hali ya juu ilitokana na utafiti wa miaka kadhaa ya melanoma, ikisifiwa kwa kuokoa maisha ya maelfu ya wagonjwa waliopatikana na saratani ya ngozi.

Viongozi wa siku zijazo wanapaswa kutetea uelewa wa ubinadamu, kuwawezesha watu kupinga mfumo uliopitwa na wakati na kutafuta suluhu za kiubunifu kwa matatizo yanayowakabili.

GeorginaLong

Allyson Felix

Allyson Felix, Marekani

Mwanariadha

Akiwa na rekodi ya kushinda medali 20 za mashindano ya kimataifa na medali za olimpiki 11 anazojivunia ,Allyson Felix ni mwanariadha mahiri katika mashindano ya kukimbia katika historia.

Baada ya kupata matatizo ya uzazi na kujifungua binti yake kabla ya muda wake wa kuzaliwa, aligeuka kuwa mwanaharakati mahiri wa kutetea haki ya afya ya uzazi. Sasa amepokea ruzuku ya dola milioni 20 za Kimarekani kutoka kwa wakfu wa Melinda Gates kuendeleza masuala ya afya ya uzazi kwa wanawake weusi nchini Marekani.

Mwanariadha aliyestaafu alikuwa kiungo muhimu katika ufunguzi wa kambi ya kwanza ya olimpiki ,katika mashindano ya mwaka huu mjini Paris

Pia mwaka huu,alichaguliwa kujiunga na kamati ya kimataifa ya wanariadha Olimpiki,na kuanzisha kampuni binafsi ya spoti inayozingatia michezo ya wanawake.

Ukakamavu ni kutafuta nguvu na ari ya kukabiliana na changamoto zinazokupata,na kutumia vikwazo kama kichocheo cha kukufanya uendelee unachofanya bila kusita.

Allyson Felix

Enas Al- Ghoul

Enas Al- Ghoul, Maeneo ya Palestina

Mhandisi wa kilimo

Wakati maji ilipokuwa haba mjini Gaza kutokana na vita, Enas Al- Ghoul alihisi kuwa amepata suluhisho.

Mhandisi huyu wa kilimo alitumia vifaa vya kuchakata kama mbao, glasi na vitiu vingine kutengeza kifaa ambacho kinatumia nguvu ya jua kutoa chumvi kwa maji ya bahari.

Kifaa hicho sasa kimekuwa kitu cha kuokoa maisha kwa watu wengi wanaoishi katika vyandarua katika maeneo ya Khan Younis kusini kwa Ukanda wa Gaza, baada ya miundombinu ya maji kuharibiwa tangu Oktoba 2023.

Al-Ghoul ambae amejitolea kutumia ujuzi wake kuwasaida Wapalestina waliofurushwa makwa pia ametengeneza jiko linalotumia nguvu ya jua na kujifunza kuchakata nyenzo kutengeneza vitu kama magodoro ya kulalia na mabegi.

Katalin Kariko

Katalin Kariko, Hungary

Mwankemia na Mshidi wa Tuzo ya Nobel

Utafiti uliosifiwa wa mwanakemia wa Hungary Katalin Kariko kuhusu Asidi ya Ribonucleic (kwa kifupi RNA) iliyobadilishwa (mRN) ulitumiwa na kampuni za BioNTech/ Pfizer and Moderna kutengeza chanjo ya Covid- 19.

Ilimwezesha kushinda tuzo ya Nobel (pamoja na mwenzake Drew Weissman) kwa mchango wake wa ''kuunda chanjo kwa kaso ambayo hakijawahi kushuhudiwa wakati wa tishio kubwa zaidi la afya ya binadamu katika ulimwengu wa kisasa''.

mRNA, nyenzo inayohusika na kubadilisha DNA yetu kuwa protini, ni dhaifu sana na ni vigumu kufanya kazi nayo, lakini Kariko aliamini inaweza kuwa na jukumu katika utengenezaji wa dawa.

Teknolojia hiyo ilikuwa ikifanyiwa majaribio kabla ya janga la corona, lakini sasa imetolewa kwa mamilioni ya watu kote duniani ili kuwalinda dhidi ya ugonjw ahatari wa Covid-19.

Fanya kazi kuelekea malengo yako kwa kuzingatia kile unachoweza kufanya na wala sio kile ambacho wengine wanapaswa kufanya. Ukishindwa jifunze kutoka na kosa lako. Simama endelea kupambana shauku iile ile uliyokuwa nayo.

Katalin Kariko

Su Min

Su Min, China

Msafiri na mshawishi

Akiwa na miaka 50 baada ya kunusurika unyanyasaji wa ndoa, Su Min alianza safari ya kibinafsi kuzuru maeneo tofauti nchini China, kwa kutumia gari lake, chandarua na malipo yake ya uzeeni.

Safari yake imemfikisha zaidi ya miji 100 katika zaidi ya mikoa 20 tangu alipoanza kuendesha gari mwaka 2020.

Ameangazia safari yake yote na hadithi yake imezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii, huku akiwatia moyo wanawake wengine wa umri wa makamo, ambao mara nyingi hujulikana kama 'shangazi' katika jamii, kwa kuthubutu kwenda kinyume na hali ilivyo.

Sasa anawafuasi milioni sita katika mitandoa kadhaa ya kijamii na maisha yake yamegeuka kuwa filamu- kama Rolling Stone- iliyotolewa mwaka huu.

Sasha Luccioni

Sasha Luccioni, Canada

Mwanasayansi wa kompyuta

Katika ulimwengu ambao unaendeana na ukuaji wa haraka wa teknolojia ya Akili Mnemba (AI), kufuatilia jinsi viwanda vinavyochangia uchafuzi wa hewa kunaweza kusahalika.

Mwanasayansi ttajika wa AI Sasha Luccioni amesaidia kubuni kifaa ambacho kinawasaidia wenye viwanda kubaini kiwango cha kaboni wanachozalisha wanapofuatilia kupitia code fulani ambayo imepakuliwa zaidi ya mara 1.3m.

Luccioni ni kiongozi wa masuala ya hali ya hewa wa Hugging Face, kapuni changa ya kimataifa ambayo inafanya kazi na mifano ya AI ya chazo wazi na anataka ''kuleta uhuru katika ufunzaji mzuri wa kutumia mashine''.

Lengo lake ni kuboresha uendelevu wa teknolojia ya AI, na analenga kukuza mfumo wa ukadiriaji wa nishati ambao kambuni zainazoibuka za AI zinaweza kutumia kulinganisha athari ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Zakia Khudadadi

Zakia Khudadadi, Afghanistan

Mwanaparalimpiki wa Taekwondo

Kama mshiriki wa kwanza wa Timu ya Olimpiki ya Walemavu kuwahi kushinda medali, Zakia Khudadadi aliandikisha historia katika mchezo ya Paris.

Mwanariadha huyo aliyezaliwa bila mkono mmoja, alianza kufanya mazoezi ya Taekwondo kisiri akiwa na umri wa miaka 11 katikaukumbi wa mazoezi katika mji wake wa Herat, magharibi mwa Afghanistan.

Mwanzoni alikataa nafasi ya kushiriki michezo ya Olimpiki ya Walemavu mjini Tokyo baada ya Taliban kurejea madarakani mwaka 2021.

Lakini baada ya Kamati ya Kimataifa ya Paralimpiki kuingilia kati kwa usaidizi wa Ufaransa, aliondolewa sala Afghanistan na hatimaye kuwa mwanamichezo wa kwanza wa Afghanistan kushiriki katika mashindano ya michezo baada ya Taliban kuchukua uongozi.

Safari yangu kuelekea kupata medali ya Olimpiki inashiria nguvu ya ustahamilivu wa mwanamke wa Afghanistan, ya mwanamke mkimbizi, na ya kila mwanamke. Kwa ktokata tamaa tunaendelea kuonyesha hakuna kitu ambacho mwanamke hawezi kukifanya.

Zakia Khudadadi

Olga Olefirenko

Olga Olefirenko, Ukraine

Mkulima

Baba yake alipofariki mwaka wa 2015, Olga Olefirenko alitaka kutimiza ndoto yake ya kujiingiza kwenye kilimo cha ufugaji. Baada ya kununua mifugo, alianza kufanya kazi lakini punde si punde alitatizika kifedha na ikamlazimu kuuza mifugo yote.

Lakini hakutaka kuachana na ndoto ya baba yake - ambaye aliuawa vitani huko Donbass akiwa kazini kama kamanda wa kikosi maalum cha wanamaji.

Mwaka jana aliweka pamoja mpango wa biashara kuomba zabuni ya ufadhili kutoka kwa Mfuko wa Veterani wa Ukraine na alifanikiwa.

Olefirenko alianza kuendesha shamba lake tena, kwa kuzingatia kilimo cha kisasa, matumizi ya teknolojia mpya za kilimo, na kutengeza nafasi ya ajira kwa jamii ya eneo hilo, ambapo anaonekana kama msukumo kwa juhudi na uongozi wake.

Margarita Barrientos

Margarita Barrientos, Argentina

Mwanzilishi wa Soup kitchen

Kuanza kuwapikia supu watu 15, kupitia mradi wa Soup kitchen hadi kuwalisha watu 5,000 kwa siku, Margarita Barrientos anafahamika kwa kujitolea kwake kukabiliana na njaa nchini Argentina, ambako 53% ya watu milioni 46 wanakabiliwa na umasikini.

Barrientos, kama mzaliwa wa eneo la nchi linalokadiriwa kuwa masikini zaidi, alikabiliwa na majanga kuanzia utotoni. Alianzisha mradi wa soup kitchen Los Piletones mwaka 1996, na kuukuza hadi kuwa wakfu ambao unaendesha kituo cha ulezi wa siku, kituo cha afya na karakana y akushona nguo na maktaba.

Huduma yake kwa jamii imepokea usaidizi kutoka kwa biashara nyingi na watu maarufu- mwanasoka Lionel Messi hivi karibuni alimpatia fulana iliyotiwa saini kuuza kupitia mnada.

Kauna Malgwi

Kauna Malgwi, Nigeria

Kiongozi wa Muungano wa wasimamizi wa maudhui

Kauna Malgwi ni mwanaharakati anayetetea haki za wafanyikazi katika tasnia ya teknolojia na akili Mnemba (AI). Mwanasaikolojia huyo wa kimatibabu anaongoza Muungano wa Wasimamizi wa Maudhui nchini Nigeria na kuongeza ufahamu kuhusu kazi inayofanyika nyuma ya pazia katika mafunzo ya mifumo ya AI.

Katika jukumu lake la awali kama msimamizi wa maudhui wa Facebook, Malgwi anasema alionyeshwa video za ubakaji, watu kujitoa uhai na unyanyasaji wa watoto, ambayo ilimfanya akosa usingizi kutokana na wasiwasi.

Yeye ni mmoja wa wasimamizi wa zamani 184 ambao wameishtaki kampuni mama ya Facebook ya Meta, pamoja na wakandarasi wadogo wa kampuni hiyo nchini Kenya, kwa kusimamishwa kazi kinyume cha sheria, baada ya mtoa taarifa kutaja mazingira duni ya kazi.

Ametoa ushahidi katika Bunge la Ulaya ili kutetea haki za wasimamizi wa maudhui.

Wanawake wanaweza kupinga na kubadilisha hali halisi ya ulimwengu wetu ulioparaganyika kwa kuleta mtazamo kamili unaothamini maendeleo ya kiteknolojia na ustawi wa kiakili.

Kauna Malgwi

Idania del Rio

Idania del Rio, Cuba

Mjasiriamali wa mitindo

Clandestina ni duka la kwanza la mitindo lililofanikiwa kujisimamia kutoka Cuba kuuza ngua mitandaoni kote duniani. Ilianzishwa kupitia ushirikiano na mbunifu mitindo Idania Del Rio.

Kampuni hiyo ilianzishwa wakati Rais Raul Castroalipolegeza vikwazo dhidi ya biashara huru.

Kampuni hiyo ambayo waendeshaji wake wengi ni wanawake iko Havana, na bidhaa zake zinajivunia utamaduni wa Wacuba. Lengo lake ni kuhimiza watu kufurahia ubunifu wa kisiwa hicho. Del Rio inajumuisha vitu kama upcycling katika uzalishaji wa bidhaa zake na kujikita zaidi katika maendeleo endelevu.

Mhitimu huyo wa Taasisi ya Ubunifu ya Havana (ISDI) alitengeneza mabango yanayotumiwa na nyumba za sanaa, kumbi za sinema na matamasha kabla ya kuanzisha biashara yake ya mitindo.

Olga Rudnieva

Olga Rudnieva, Ukraine

Mwanzilishi wa kituo cha Superhumans

Kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Olga Rudnieva alihisi anahitaji kufanya kitu kuwasaidia wale waliojeruhiwa katika mzozo huo.

Watu waliopoteza viungo vyao vya mwili vitani walionekana na wengi kama waathirika, lakini kwa Rudnieva walikuwa watu wasio wa kawaida 'Superhumans' ambao walihitaji kupata msaada wote ambao angeweza kuwapatia.

Alifungu kituo cha kukabiliana na kiwewe cha Superhumas mjini Lviv, ambacho anaendesha kama Afisa Mkuu Mtendaji kwa usirikiano na kundi la wataalamu. Kituo hicho kinatoa viungo bandia kwa wagonjwa na hivi karibuni kimezidua kitengo cha ushauri nasaha.

Zaidi ya watu 1,000 wamenufaika kutokana na huduma zake miaka miwili ya kwanza tangu kilipoanza kuendesha shughuli zake.

Ustahamilivu ni kuamshwa kila asubuhi ni milio ya king'ora za tahadhari na kuendelea kupigania nchi yako. Ni kutambua upya 'wajibu wako', badala ya kujiuliza 'mbona mimi?' Ni kutafuta njia ya kufanya mambo zaidi hata ukiwa na siku chache kila siku.

Olga Rudnieva

Shahrnush Parsipur

Shahrnush Parsipur, Iran/Marekani

Mwandishi na mfasiri

Shahrnush Parsipur ni mmoja wa waandishi mashuhuri wa riwaya wa Iran, ameshughulikia masuala ya mwiko katika kazi yake, kama vile ukandamizaji wa kijinsia wa wanawake na uasi katika jamii.

Alianza kazi yake kama mwandishi wa hadithi na mtayarishaji wa vipindi ya Televisheni na Redio ya Kitaifa ya Iran, lakini alijiuzulu kwa kupinga kunyongwa kwa wanaharakati wawili wa mashairi kabla ya mapinduzi ya 1979. Hii ilisababisha kufungwa kwake kwa mara ya kwanza.

Tangu mapinduzi, kazi yake imepigwa marufuku sana nchini Iran na Parsipur alifungwa tena kwa kurejelea wazi masuala yanayohusu ubikira katika riwaya yake ya Women Without Men. Baadaye filamu hii ilifasiriwa na kuonyeshwa nje ya Iran.

Parsipur amesimulia kwenye uandishi wake akile alichopitia alipokuwa kizuizini, na ameishi uhamishoni nchini Marekani tangu 1994.

Sneha Revanur

Sneha Revanur, Marekani

Mtaalamu wa Akili Mnemba

Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Sneha Revanur tayari yuko kifua mbele kwenye fani yake ta teknolojia. Ni muanzilishi wa Encode Justice, vuguvugu la kimataifa la vijana linalohamasisha usalama, usawa katika matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba(AI), ikiwa na zaidi ya wanachama 1300 katika mataifa 30.

Kazi ya Revanur inalenga kupunguza vitisho vinavyotokana na teknolojia inayoibuka na kujumuisha vijana katika mazungumzo muhimu.

Ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Stanford na wakati wa likizo anatoa huduma za usaidizi kuhusiana na masuala ya AI na Sera za Kidijitali.

Hivi majuzi alitajwa kuwa kijana mdogo zaidi kujumuishwa kwenye orodha ya uzinduzi ya Jarida la Time la watu watu walio na ushawishi mkubwa katika masuala ya AI.

Tuna nafasi ya kukabiliana na vitisho vya AI kabla hatujanufaika na na uwezo wake. Kwangu mimi huu ni ustahamilivu: kuruka vizingiti vilivyoibuka ili kufikia malengo ya siku zijazo.

Sneha Revanur

Subin Park

Subin Park, Afrika Kusini

Mwanzilishi wa Klabu ya Stair Crusher

Wakati Subin Park ambaye anatumia kiti cha magurudumu alipogundua hawezi kufika sehemu nyingi alizotaka kufika, aliamua kutumia ujuzi wake kama mkuu wa zamani wa teknolojia ya mawasiliano kuangazia suala hilo.

Park ni mwanzilishi mweza wa klabu ya Stair Crusher, mradi ambao unakusanya maelezo kuhusu njia na maeneo yasio rafiki kwa walemavu nchini Korea Kusini.

Mradi huo unaazimia kutengeza ramani ya kuwaelekeza watumiaji.

Kufikia sasa zaidi ya wananchi 2,000 wamechangia hifadhidata kupitia Klabu ya Stair Crusher na maeneo 14,000 kote nchini yamekaguliwa na kuhakikiwa kwa ufikiaji.

Pooja Sharma

Pooja Sharma, India

Mtendaji wa ibada ya mazishi

Kwa miaka mitatu iliyopita, Pooja Sharma amekuwa akifanya ibada ya mwisho ya wafu ya maiti ambazo hazijadaiwa mjini Delhi

Kinachompatia msukumo wa kufanya hivyo ni kitu alichokipitia yeye mwenyewe, baada ya kumfanyia ibada ya mwisho ndugu yake aliuawa na hakuna mtu aliyemsaidia kuandaa mazishi yake.

Sharma alikabiliwa na upinzani kutoka kwa makuhani na jamii kwa ujumla, kwani wajibu huo kitamaduni hufanywa na na wanaume katika dini ya Kihindu.

Licha ya ukosoaji huo, amefanya ibada ya wafu kwa maiti zaidi ya 4000 kutoka dini tofauti, akiweka kazi yake katika mitandao ya kijamii na kutetea haja ya kumpatia kila mtu heshima ya mwisho anapofariki.

Helen Molyneux

Helen Molyneux, Uingereza

Mwanzilishi mwenza, Monumenta Welsh Women

Kabla ya mwaka 2021 hapakuwa na sanamu zilizowekwa kuwatambua wanawake wa Wales.

Kushughulikia hilo, wakili Helen Molyneux alishirikiana na wenzake kuanzisha Monumental Wels Women, shirika lisilo la kiserikali linalolenga kuimarisha uwakilishi wa wanawake wa Vwales na kutambua michango na mafanikio yao.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya umma, Molyneux na timu yake walipanga kuweka sanamu tano za wanawake, kuhakikisha michango yao haisahauliki.

Kundi hilo limeweka sanamu nne - ya kwanza ilikuwa ya mwalimu mkuu wa kwanza mweusi wa Wales Betty Campbell mjini Cardiff, ikifuatiwa na ya Elaine Morgan huko Maountain Asha, Cranogwen mjini Llangrannog na Lady Rhonddn huko Newport.

Yasmeen Mjalli

Yasmeen Mjalli, Maeneo ya Palestina

Mbunifu

Ubunifu wa mitindo wa Yasmeen Majalli umechochewa na maisha ya Wapalestina na utamaduni wao.

Baada ya kukulia kusini mwa Marekani, alihamia Ramallah katika eneo la Ukingo wa Magharibi, ambako alizindua chapa yake ya Nol collctiion mwaka 2020.

Lebo yake ya mitindo inafanya kazi na duka la kushona nguo linaloendeshwa familia moja ambayo hutoa rangi ya asili kupitia vyama vya ushirika vya wanawake ambayo vinatengeza nguo pamoja. Washonaji na mafundi wengine wote wanatumia mbinu ya kiasili ya ufundi wa Palestina wa kuunda kitambaa.

Mjalli ametumia vitambaa vyake kusimulia hadithi ya Wapalestina. Pia anaangazia unyanyasaji wa mitaani unaowakabili wanawake kote duniani, kwa kuchora maneno 'not yours habibti' (sio yako habibi) kwenye jaketi na fulana za denim.

Hinda Abdi Mohamoud

Hinda Abdi Mohamoud, Somalia

Mwanahabari

Hinda Abdi Mohamoud amekuwa mwandishi makini tangu akiwa mdogo. Ameandika hadithi kuhusu watu wakitoroka ghasia katika mji wake wa Hargeisa nchini Somalia.

Sasa ni mhariri mkuu wa Bilan, chombo cha habari cha kwanza kinachoendeshwa na wanawake nchini humo.

Kituo hicho kilibuniwa kukabiliana na unyanyasaji unaowakabili wanawake wa Kisomali katika maeneo ya kazi-changamoto ambazo zimeangaziwa na ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa.

Bilan inalenga kuangazia masuala ya kijamii katika mojawapo wa mataifahatari zaidi duniani kwa wanahabari, kwa kujikita zaidi kwenye taarifa kama vile Wasomali wanaoishi na HIV, yatima wanaonyanyaswa, na zeruzer wanaotengwa na jamii zao.

Samia

Samia, Syria

Mtaalamu wa saikolojia Samia - ambaye BBC imeamua kuficha utambulisho wake ili kulinda usalama wake binafsi - amekuwa akiwaunga mkono Wasyria wanaokabiliwa na kiwewe kilichosababishwa na migogoro ya miaka mingi.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, na wengi wa wale walionusurika mara nyingi wameachwa wakiishi katika hali mbaya na kukabiliwa na matatizo ya afya ya akili kama vile unyogovu na wasiwasi.

Akifanya kazi katika kliniki ya afya ya akili inayosimamiwa na Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji, Samia anaendesha vikao vya ushauri kwa watu waliohamishwa na familia zao katika kambi ya wakimbizi kaskazini-mashariki mwa Syria.

Licha ya rasilimali haba, anaendelea kujitolea kuboresha afya ya akili ya wagonjwa wake na amejitolea kukuza uhamasishaji katika mazingira ya shida.

Tracy Otto

Tracy Otto, Marekani

Mfuma mishale

Alishambuliwa akiwa nyumbani na mpenzi wake wa zamani mwaka 2019, Tracy Otto na kuachwa akiwa amepooza kutoka kifuani hadi sehemu ya chini ya mwili wake na kupoteza jicho lake la kushoto. Kwa kuwa alikuwa na azma ya kuwa mwanamitindo wa mazoezi hakuwa na budi kurejelea maisha ya kawaida.

Mwezi Machi 2021, aliamua kujiunga na mchezo amabao hakuwahi kujaribu- kufuma mishale. Alilenga shabaha kwa mshale wa kwanza na moja kwa moja akavutiwa na mchezo huo.

Mwaka huu, Otto alishiriki kwa mara ya kwanza michezo ta Olimpiki ya Walemavu. Kutokana na ulemavuwake anatumia mdomo wake kufuma mshale.

Karibu miaka mitano baadaye, Otto pia anatumia tajiriba yake kutetea walionusurika ukatili wa nyumbani.

Noella Wiyaala Nwadei

Noella Wiyaala Nwadei, Ghana

Msanii wa muziki wa Afro -pop

Muimbaji na mtunzi wa muziki Noella Wiyaala Nwadei anajulikana kwa jina la kisanii kama Wiyaala, ambalo linamaanisha 'mtendaji' katika lugha yake ya Sissala.

Anatambuliwa kwa mtindo wake wa kipee wa mavazi, kwasababu anajishonea mwenyewe nguo zake na vifaa vingine anavyomia jukwaani ili kuonyesha utamaduni wa eneo analotoka kaskazini mwa Ghana.

Baadhi ya nyimbo zake zinaangazia unyanyasaji unaowakabili wanawake wa Kiafrika. Wiyaala amefanya kazi kwa karibu na mashirika ya Umoja wa Mataifa na kwa ushirikiano na mamlaka nchini Ghana kukabiliana na ndoa za utotoni.

Pia amejenga kituo cha sanaa,kufungua kituo cha redio ya kijamii na mgahawa kutoa nafasi ya ajira na ubunifu wa nyumbani kwao Funsi.

Nejla Isik

Nejla Isik, Uturuki

Kiongozi wa kijiji na mhifadhi misitu

Mkulima Nejla ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa kiongozi wa eneo la Ikizkoy magharibi mwa Uturuki ameongoza mapambano dhidi ya ukataji miti katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Wakati msitu wa Akbelen ulipokumbwa na tishio la kuharibiwa kutokana na pendekezo la uchimbaji makaa wamawe, Isik na wanawake wengine walikabiliana na hatua hiyo kisheria kukomehsa ukataji miti ambao ungetoa nafasi kwa miradi ya uchimbaji madini.

Wakati huo kampeni yao ya kuhifadhi mazingira ilisababisha makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji waliokua wameamua kutoa ulizi wa misitu, lakini Isik na wanavijiji wenzake waliapa kusimama kidete licha ya changamoto na tishio la kupigwa faini iliyowakabili kwa kuingia katika msitu huo bili idhini (faini hiyo baadaye ilifutiliwa mbali).

Wanawake walio majumbani, mashambani na mitaani ndio waliofanikisha mapambano hayo...ni wao ndio wanaopamba ulimwengu, na bila shaka watauokoa.

Nejla Isik

Susan Collins

Susan Collins, Marekani

Seneta

Susan Collins ambaye sasa hivi anahudumia muhula wake wa tano anaiwakilisha jimbo la Maine, ndiye mwanamke wa Republican aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika Seneti ya Marekani.

Amefanya kazi mara kwa mara na vyama ili kutoa sheria muhimu. Yeye ni mmoja wa maseneta sita walio na jukumu la kuanzisha Sheria ya Kuendeleza masuala ya Ukoma Hedhi na Afya ya Wanawake, ambayo itawekeza $275m katika utafiti wa kukoma hedhi, matibabu, na uhamasishaji wa umma katika miaka mitano ijayo.

Collins pia aliandika Sheria ya Mradi wa Kitaifa wa Alzeima, ambayo inaratibu mpango wa kitaifa wa kuzuia na kutibu ugonjwa wa Alzeima. Amefanya kazi ili kuhakikisha ufadhili wa mradi hadi 2035, na kwamba inazingatia idadi kubwa ya watu ambao hawajahudumiwa pamoja na watu walio na ugonjwa wa kupooza ubongo.

Huang Jie

Huang Jie, Taiwan

Mwanasiasa

Huang Jie anajulikana kwa kutetea usawa wa kijinsia. Mnamo mwezi Januari mwaka huu alishinda kiti cha ubunge na kuwa mwanamke wa kwanza wa Taiwan ambaye anashiriki mapenzi ya jinsi moja LGBTQ+

Ameanzisha mageuzi makubwa wakati wa kazi yake ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kupata haki za wanawake wasio na waume na wanawake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupata tiba ya uzazi na kuishinikiza serikali kutoa ruzuku ya bidhaa za hedhi kwa wanawake waliona mapato ya chini na walemavu.

Baada ya kuweka hadharani muelekeo wake wa kijinsia mwaka 2023, amezungumzia wazi waziunyanyasaji aliyokumbana nao.Kama muathiriwa na filamu ghusi za kingono, anateta kuimarishwa kwa sheria zilizopo ilikukabiliana na unyanyasaji wa kingono mitandaoni.

Ustahalivu wa kweli ni kukumbatia tofauti zetu. Kadiri sauti nyingi zitakavyoshirikishwa ndivyo nguvu yetu inaimarika - hasa wale wanaochukuliwa kuwa wanyonge, wanawake na jamii ya LGBTQ+.

Huang Jie

Hadiqa Kiani

Hadiqa Kiani, Pakistan

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo

Kama mmoja wa nyota wa muziki wa Pakistan, Hadiqa Kiani anajulikana kwa sauti yake ya kuvutia na mchango wake katika jamii.

Tangu alipopata umaarufu miaka ya 1990, msanii huyo wa muziki wa pop amekuwa mwanamke mashuhuri Asia ya Kati, na pia balozi wa heri njema wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa.

Ili kukabiliana na mafuriko mabaya yaliyokumba Pakistan mwaka 2022 , Kiani alizindua mradi wa Vaseela-e- Raah kuwasaidia walioathirika na mafuriko hayo katika maeneo ya Balochistan na Punjab Kusini.

Alitoa wito kwa umma kusaida familia zilizosambaratishwa na mafuriko. Mwaka jana mradi wake ulitangaza kuwa umewajengai waathiriwa nyumba 370 na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa katika maeneo hayo.

Zhina Modares Gorji

Zhina Modares Gorji, Iran

Mpigania haki za Wanawake

Mwanahabari wa Kikurdi na mwanaharakati Zhina Modares Gorji alianzisha chama cha wanawake cha Zhivano mwaka 2019, ambacho kinatumia elimu, maandamano na kusaidia juhudi za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake.

Modares Gorji amekamatwa mara mbili kuanzishwa kwa vuguvugu la Iran's Woman. Life, Freedom. Mwanzoni alihukumiwa kifungo cha miaka 21 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ''kueneza propaganda dhidi ya utawala'', Lakini sasa anahudumia kifungo cha miaka miwili baada ya hukumu dhdi ya ke kubadilishwa.

Alikuwa mwanachama wa kampeni ya One Million Signatures ambayo ilipania kutafuta uungwaji mkono wa umma kushinikiza marekebisho ya katiba ya Iran, hasa sheria inayowabagua wanawake.

Ni mmoja wa kundi la wapiga picha wanawake wa Kikurdi, muongozaji wa podcast ya wanawake na kitabu cha watoto ambayo inaangazia kuwatia moyo wanawake wa Kikurdi.

Guerline M. Jozef

Guerline M. Jozef, Haiti

Mpiganiaji wa haki za Uhamiaji

Kufanya kazi katikika makutano ya siasa na rangi nchini Marekani, Guerline M. Jozef anapigania haki za uhamiaji.

Ni mwanzilishi wa Bridge Alliance, shirika la Haiti linaloongozwa na wanawake ambalo linaangazia watu wenye asili ya Kiafrika.

Chini ya uelekezi wake, Muungano huo uliwasilisha kesi dhidi ya Donald Trump mwaka huu kuhusiana madai yasio na msingi aliyotoa akisema kwamba wahamiaji kutoka Haiti wanakula ''wanyama wa kufuga nyumbani'' katika hotuba yake mjini Springfield, Ohio wakati wa kampeni ya urais.

Jozef kwa muda mrefu amekuwa mkosoaji mkubwa wa kufukuzwa kwa raia wa Haiti. Shirika lake hivi karibuni lilitoa wito kwa utawala wa Biden kuacha kuwarudisha nyumbani waomba hifadhi waliokimbilia Marekani ili kuepuka ghasia za magenge nchini mwao.

Ruth Lopez

Ruth Lopez, El Salvador

Wakili

Ruth Lopez mwenye shauku ya sheria na haki ni afisa mkuu wa masuala ya sheria wa Cristosal, shirika ambalo linafanya kazi kuendelezademokrasia kote Amerika ya Kati.

Amekuwa akijikita katika kupambana na rushwa, sheria ya uchaguzi na ulinzi wa haki za binadamu nchi El Salvador.

Kama mkosoaji wa utawala wa nchi na taasisi zake, amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kupigania ukuzaji wa uwazi wa kisiasa na uwajibikaji wa umma unaosimamiwa na wananchi wenyewe.

Kazi yake ilipata umaarufu mapema mwaka huu wakati Eli Salvador ilipomchagua tena rais Nayib Bukeli kwa muhula wa pili madarakani. Bukele ambaye umaarufu wake uliongezeka kufuatia msako mkali dhidi ya wahalifu, amejiita ''dikteta mzuri zaidi duniani''.

Ann Chumaporn (Waaddao)

Ann Chumaporn (Waaddao), Thailand

Mtetezi wa haki ya LGBTQ+

Wakati Thailand ilipotia saini muswada wa usawa wa ndoa kuwa sheria na kuwa nchi ya kwanza Asia Mashariki kutambua ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, Ann 'Waaddao' Chumaporn alikuwa na sababu ya kusherehekea,

Alikuwa ameongoza juhudi za kupitisha muswada huo bungeni, akihudumu kama kamishena wa kushughulikia babadikio ya kisheria katika mabunge yote ya wawakilishi na Seneti.

Kama mwanzilishi mwenza wa Bankok Pride na mwanaharakati kutoka maeneo ya vijijini kusini mwa Thailand, Chumaporn amekuwa akitetea haki ya wapenzi wa jinsia moja kwa zidi ya muongo mmoja.

Wakati wa maandamano ya vijana ya mwaka 2020 nchini Thailand, aliibuka kama kiongozi wa chama cha Feinist Libertaion Front kinachounga mkono demokrasia; alikabiliwa na mashataka manane kutokana na uwanaharakati wake wa kisiasa.

Katherinre Martinez

Katherinre Martinez, Venezuela

Wakili wa kutetea haki za binadamu

Baadhi ya wagonjwa wadogo katika hospitali ya watoto ya Jose Manuel de Los Rios mjini Caracas, Venezuela wanatoka katika familia masikini inayotunzwa na mzazi mmoja.

Prepara Familia, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na Katherine Martinez, inatoa vitu muhimu kama vile nguo, vifaa vya kimatibabu na chakula- na usaidizi wa kisaikolojia.

Kama wakili anayetetea haki za binadamu, Martinez anaweka orodha ya kile ambacho yeye na timu yake wanakiona kama unyanyasaji wa haki dhidi ya watoto na walezi wa kike katika mazingira ya hospitali, ili kuwawezesha waathirika kutafuta fidia.

Baada ya kushuhudia viwango vya juu vya utapiamlo nchini Venezuela, Prepara Familia pia ilifungua kituo cha kuwapatia watoto na wanawake wajawazito vidonge vya nyongeza ya lishe na vitamini bila malipo.

Firda Marsya Kurnia

Firda Marsya Kurnia, Indonesia

Mwanamusiki wa bendi ya Heavy metal

Kuvunja miiko ya kijinsia na kanuni za kitamaduni ni vitu ambavyo amezoea kufanya Firda Marsya Kurnia kama muimbaji mkuu na mpigaji gita katika bendi ya wanawake, wanaovalia hijab.

Kuimba kwa Kiingereza na Kisudan, moja ya lugha inayozungumzwa sana nchini Indonesia ni jambo ambalo watatu hao wanaangazia katika muziki wao kuelezea mahangaiko ya wanawake katika jamii ya mfumo dume

Kumekuwa na malalamiko dhidi yao kutoka kwa Waislamu wahafidhina ambao hawakupokea hatua yao ya kujiingiza katika muziki wa bendi.

Lakini bendi hiyo imepiga hatua kubwa tangu walipoianzisha miaka 10 iliyopita katika shule yao ya vijijini huko Garut,West Java. Mwaka huu walitumbuiza katika tamasha la Glastonbury, na kuwa bendi ya kwanza ya Indonesia kutumbuiza katika historia ya miaka 54 ya tamasha hilo la muziki .

Latisha McCrudden

Latisha McCrudden, Ireland

Mwanaharakati wa jumuiya ya wasafiri wa Ireland

Ana miaka 20 tu, lakini Latisha McCrudden tayari amejitambulisha kama mtetezi mahiri wa jumuiya ya Wasafiri wa Ireland.

Kama mwanachama, anataka kupambana na miiko inayozunguka jamii ndogo za Ireland ana kutumia sauti yake kama manusura wa unyanyasaji wa nyumbani kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

McCrudden ambaye pia ni mwanafunzi wa somo la sheria katika Chuo Kikuu cha Galway, anahudumukama mwanachama katika Jukwaa la Kitaifa la Wasafiri Vijana na Baraza la Kitaifa la Wanawake wa Ireland, na Kikundi cha kutoa msaada kwa Wasafiri, Minceirs Whiden.

Anatarajia kugombea katika uchaguzi ujao wa ndani mwaka wa 2029 na kuleta mabadiliko kwa mustakabali wa Ireland

Gabby Moreno

Gabby Moreno, Guatemala

mwanamuziki

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo anayesifika katika ulingo wa muziki wa Kilatini, Guatemala Gaby Morono alipata umaarufu baada ya kushinda Grammy ya Albamu Bora ya Kilatini ya muziki wa Pop mnamo 2024.

Muziki wake unatokana na mchanganyiko wa lugha mbili zilizoshawishiwa na mitito ya Americana ay Soul na wa watu wa Kilatini. Muziki wake unaashiria urithi mkubwa wa kitamaduni.

Moreno pia ni raia wa kwanza wa Guatemala kuwa balozi wa heri njema wa Unicef, kutetea haki za watoto.

Hivi karibuni alizindua kampeni ya kushinikiza upatikanaji wa vifaa bora vya elimu, katika nchi ambayo inakadiriwa wasichana na wavulana 2.7m wako nje ya mfumo wa shule.

Hala Alkarib

Hala Alkarib, Sudan

Mwanaharakati wa kupambana na ukatili wa kingono vitani

Kama mkurugenzi wa kikanda wa shirika la mipango ya wanawake katika Upembe wa Afrika(SIHA), Mwanaharakati mashuhuri na mwandishi Hala Alkarib anaongoza mikakati inayoangazia masuala ya ukatili wa kijinsia kikanda.

Tangu vita vilipozuka nchini Sudan mnamo Aprili 2023, SIHA imekuwa ikifuatilia mizozo inayohusiana na ukatili wa kingono, na kutoa msaada kwa wanawake na wasichana

Ripoti ya Octonar 2024 ya Umoja wa Mataifa ilionya kuwa kuhusu ''viwango vya juu'' vya visa hivyo, ikiwanyoshea kidole cha lawama wanamgambo wa RSF kwa kutekeleza ''uhalifu wa kikatili'', madai ambayo RSF ilikanusha.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa takriban manusura 400 wa ukatili wa kingono unaohusishwa na migogoro ya kivita wamepewa usaidizi tangu mwezi Julai 2024, ikielezea hili hiyo kama ''kionjo tu'' cha madhila yanayowakabili waathiriwa.

Kemi Badenoch

Kemi Badenoch, Uingereza

Kiongozi wa chama cha Conservative

Kemi Badenoch ambaye alichaguliwa kiongozi wa chama cha Conservative mwezi Novemba ni mwanamke wa kwanza mweusi kuongoza chama kikuu cha kisiasa nchini Uingereza.

Kwa sasa ni Mbunge wa eneo la Essex Kaskazini Mashariki lakini pia aliwahi kuwa waziri wa biashara na masuala ya wanawake na usawa.

Badenoch alizaliwa mjini London kutokana na wazazi wa Kinigeria lakini alilelewa Lagos Nigeria na Marekani. Alirejea Uingereza akiwa na umri wa miaka16 kutokana na kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Nigeria na kusomea shahada ya uhandisi wa komyuta na sheria.

Kabla ya kijiunga na siasa, alikuwa mkurugenzi msaidizi wa benki binafsi ya Coutts na mkurugenzi wa kidijitali wa gazeti la The Spectator,

Lourdes Barreto

Lourdes Barreto, Brazil

Mtetezi wa haki za wafanyakazi wa ngono

Lourdes Barreto ametumia muda wake mwingi maishani kupigania haki ya wafanyabiashara wa ngono. Amekuwa ngozo muhimu katika kampeni nyingi.

Alianza uanaharakati huko Bele do Para katika eneo la Amazon, baadaye kwa ushirikiano wenzake akaazisha Mtandao wa Makahaba wa Brazil katika miaka ya 1980- mojawapo ya vuguvugu rasmi la wafanyakazi wa ngono Amerika Kusini.

Barreto ambaye sasa yukukweye miaka yake ya 80, amekuwa akipinga ubaguzi dhidi ya watu hao.

Alichangia kubuniwa kwa sera za kuzuia HIV nchini na kupigania kuenea kwa maambukizi ya HIV miongoni mwa jamii ya wachimbaji madini. Mwaka 2023, alichapisha wasifu wake.

Naomba hadithi zetu zithaminiwe. Wanawake duniani wana uwezo mkubwa kuwa na ndoto ambazo zitabadilisha jamii.

Lourdes Barreto

Vinesh Phagat

Vinesh Phagat, India

Mwanamieleka

Mshiriki wa Olimpiki mara tatu,Vinesh Phogat ambaye ni mcheza miereka na mkosoaji mkuu wa mtazamo wa kijinsia dhidi ya wanawake katika michezo.Ameshinda medali katika mashindano ya dunia,Michezo ya Jumuiya ya Madola,na Michezo ya Asia.

Mwaka ambao Phogat alitunukiwa kuwa mwanamke wa kwanza katika mchezo wa miereka kufika fainali yamashindano ya Olimpiki,lakini aliondolewa kwa kinyang'anyiro baada ya kushindwa katika awamu ya kuinua uzani .Baadaye alistaafu kutika kwa michezo na kujiunga na siasa.

Akipaza sauti kuhusu mitazamo ya kijinsia,Phogat alikuwa sura ya maandamano ya wacheza miereka nchini India dhidi ya mkuu wa shirikisho lao,Brij Bhushan Singh.,ambaye alituhumiwa kwa shtaka la unyanyasaji wa kingono dhidi ya wachezaji wa jinsia ya kike -shtaka ambalo alilikanusha.

Maandamano yaligonga vichwa vya habari kufuatia maafisa wa polisi kumzuilia Phogat na wengine wakati wa maandamo

Uwezo wa kuinuka baada ya kuwa siku isiyokuridhisha kazini na kujipa moyo ni njia moja ya kuwa mkakamavu.

Vinesh Phagat

Joan Chelimo Melly

Joan Chelimo Melly, Kenya/Romania

Mkimbiaji wa masafa marefu

Akisherehekewa kwa mafanikio yake katika mbio za masafa marefu, mwanaolimpiki raia wa Romania mzaliwa wa Kenya Joan Chelimo alishinda medali ya fedha katika Mashindano ya Uropa mwaka huu.

Mbali na michezo, ni mwathirika wa ukatili wa kijinsia anatumia hadithi yake mwenyewe kuangazia tishio linalowakabili wanariadha wa kike.

Alishirikiana kuanzisha Tirop's Angels, shirika la wanariadha wa Kenya lililobuniwa baada ya mauaji ya mwanariadha mwenzake na mshikilizi wa rekodi ya dunia Agnes Tirop mwaka 2021, ambalo linapinga ukatili wa kijinsia kupitia shughuli mbalimbali.

Mwaka huu mauaji ya mwanariadha wa Olimpiki Rebecca Cheptegei yaliyotekelezwa na mpenzi wake wa zamani yaliibua tena wito wa kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya mauaji ya wanawake.

Ninaamini kwamba mabadiliko ya kweli huanza pale tunapoamua kuwa mateso yetu sio mwisho wa maisha, bali ni mwanzo wa mambo makubwa zaidi.

Joan Chelimo Melly

Mahrang Baloch

Mahrang Baloch, Pakistan

Daktari na mwanaharakati wa kisiasa

Mahrang Baloch amekuwa miongoni mwa mamia ya wanawake ambao wamekuwa wakishiriki maandamano nchini Pakistan, kulalamikia visa vya watu kutoweka katika mazingira ya kutatanisha mkoani Balochistan.

Mwito wake wa kutetea haki ulikuja baada ya baba yake mzazi kuchukuliwa na maafisa wa usalama mwaka 2008 na kupatikana akiwa amefariki miaka miwili baadaye akiwa na dalili za kuteswa.

Mwishoni mwa mwaka 2023, Baloch aliongoza mamia ya wanawake kushiriki matembezi ya maili 1,000 (1,600km) hadi mji mkuu wa Islamabad kushinikiza kupata taarifa kuhusu jamaa zao waliotoweka. Alikamatwa mara mbili wakati safari hiyo.

Waandamanaji kutoka mkoa wa Balochistan, kitovu cha uasi wa kitaifa, wanasema wapendwa wao walichukuliwa na kuuawa na vikosi vya usalama vya Pakistan wakati wa operesheni ya kukabiliana na uasi. Mamlaka mjini Islamabad inapinga madai hayo.

Daktari huyo amekuwa mwanaharakati maarufu chini ya mwavuli wa Kamati ya BYC Baloch Yakjeht i(Umoja) -shirika lake binafsi la kutetea haki za binadamu. Juhudi zake katika masuala ya kutetea haki za binadamu zilijumuishwa katika orodha ya TIME100 NEXT 2024 ya viongozi wanaoibuka.

Inna Modja

Inna Modja, Mali

Msanii na mtetezi wa hali ya hewa

Mpiganiaji haki ya masuala ya hali ya hewa, mwanamuziki na mtayarishaji filamu Inna Modja ni mwanamke ambaye amejuhusisha na mambo mengi - kuanzia kupinga ukeketaji wa wanawake hadi kuetea uendelevu.

Alitayarisha na kuigiza filamu ya The Great Wall, ambayo inaangazia Juhudi kabambe za Afrika kudhibiti upanuzi wa jangwa na na kuhuisha ardhi iliyoharibiwa katika eneo la Sahel kusini mwa jangwa la Sahara- kuanzia mashariki hadi magharibi kupitia mataifa 12.

Ni balozi wa nia njema wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na uharibifu wa misitu, na amekuwa akipaza sauti ya jamii zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Modja pia ni mwanzilishi mwenza wa shirika lisilo la kiserikali ambalo linajumuisha uvumbuzi ,teknolojia na michezo ya kuhamasisha matokeao chanya.

Hana- Rawhiti Maipi- Clarke

Hana- Rawhiti Maipi- Clarke, New Zealan

Mwanasiasa

Hana- Rawhiti Maipi- Clarke, mwenye umri wa miaka 22, alikuwa manamke mdogo sana wa Mari kuchaguliwa katika bunge la New Zealand

Wakati wa hotuba yake ya kwanza, alicheza Haka, densi ya kusherehekea ya jamii ya Maori, na kutoa wito wa kuongezwa kwa uwakilishi wa jamii za ki. Hivi karibuni aliongoza Haka nyingine ambayo ilisitisha shughuli bungeni kupinga muswada wenye utata.

Maipi- Clarke anatetea kwa moyo wote haki ya jamii ya Maori, kuhifadhi utamaduni na masuala ya mazingira. Akiwa na umri wa miaka 17 alichapisha kitabu chak echa kwanza kuhusu kalenda ya mwezi wa Maori

Mwaka huu alipokea tuzo ya kifahari ya One Young Wourld kwa kuwa mwanasiasa wa mwaka kutokana na juhudi zake za kupaza sautu ya wanasiasa vijana wa jamii ya kiasili.

Wanawake hawana budi kubisha milango hasa katika maeneo ambayo hawajakaribishwa, iwe ni katika siasa za ngazi ya kijamii, kitaifa au kimataifa

Hana- Rawhiti Maipi- Clarke

Hend Sabry

Hend Sabry, Tunisia

Muigizaji

Muigizaji Hend Sabry ni mmoja wa wanawake mashuhuri katika filamu za Kiarabu. Jukumu lake katika filamu ya The Silences of the Palace(1994) iliangazia unyanyasaji wa kingono na kijamii unaowakabili wanawake wa Tunisia.

Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kiarabu kuwa mwamuzi katika Tamasha la Filamu la Venice mwaka 2019.

Hivi karibuni alishiriki katika filamu ya Olfa's Daughters ambayo iliteuliwa kama filamu ya Tunisia kuwania tuzo ya Oscars 2024 katika kitengo cha Best Documentary Feature.

Mwezi Novemba, alijiuzulu kama balozi wa heri nhea wa Umoja wa Mataifa, kulalamikia kile alichokiita utumizi wa njaa kama silaha katika vita vya Gaza.

Sio tu kuishi; bali ni kujijenga upya na kuendelea namaisha licha ya changamoto unazopitia...kubadilisha hali ngumu unayopitia kwa utahamilivu.

Hend Sabry

Elaha Soroor

Elaha Soroor, Afghanistan

Muimbaji na mtunzi

Wakati ambao sauti ya wanawake nchini Afghanistan inazimwa katika maeneo ya umma, muimbaji Elaha Soroor aliandika wimbo wa Anna, Kar, Azadi! (Mkate, Kazi, Uhuru!) kukabiliana na ukandamizaji na kutoa ujumbe wa kutia moyo.

Wimbo huo uliangaziwa mara ya kwanza mwezi Oktoba katika kongamano la wanawake wa Afghanistan huko Albania.

Katika filamu inayoangazia kazi yake, sanaa na muziki, msanii huyo aliyeshinda tuzo mara nyingi anatumia jukwaa lake kutetea haki za wanawake.

Saroor, ambaye anatokea jamii ndogo ya Hazara alipatikana kupitia kipindi maarufu cha kusaka talanta cha Afghan Star mwaka 2009. Lakini alikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kujiingiza katika fani ya muziki na kuondoka nchini mwaka 2010.

Lilia Chanysheva

Lilia Chanysheva, Urusi

Mwanaharakati wa kisiasa na mfungwa wa zamani

Kama mmoja wa wafungwa 26 walioachiwa mwezi Agosti mwaka huu kama sehemu ya mpango wa kubadilishana wafungwa, mwanaharakati Lilia Chanysheva aliondoka Urusi alipopata uhuru wake.

Chanycheva alikuwa akiongoza ofisi ya mwanasiasa wa upinzani marehemu Alexei Navalny katika eneo la Urusi la Nahkortostan. Kazi yake ilijumuisha kuchunguza visa vya ufisadi, kupigania uchaguzi wa haki na uhuru wa kujieleza.

Kabla ya kumfanyia kazi Navalny alikuwa mwanauchumi na mshauri wa masuala ya kodi wa mashirika ya kimataifa mjini Moscow.

Mwaka 2021, alikamatwa na kushtakiwa kwa kuwa na misimamo mikali na kuhumiwa kifungo cha miaka tisa na nusu gerezani. Alihudumia kifungo hicho kwa miaka miwili na miezi tisa kabla ya kuachiwa huru.

Danielle Cantor

Danielle Cantor, Maeneo ya Israel/Palestina

Mwanaharakati wa kitamaduni

Kama mwanzilishi mwenza wa Culture of Solidarity, mradi wa mashinani ulioanzishwa wakati wa janga, Danielle Cantor ametoa msaada wa chakula kwa familia za Tel Aviv.

Kwa ushirikiano na mwanzilishi mwenza wake Alma Beck, anaendesha House of Solidarity, jukwaa ambalo limetoa njia mbadala kwa watu kukutana, kujadili na kuhudhuria matamasha ya kitamaduni na warsha.

Hivi karibuni aliandika na kupiga picha Spreads,kitabu cha usanii ambacho kinatumia utamaduni wa chakula kuchunganua siasa za utambulisho wa kijamii kattika maeneo ya Waisraeli na Wapalestina.

Kwa ushirikiano na wanawake wengine, Cantar amekuwa akijiunga na maandamano ya kushinikiza usitishaji wa mapigano ya mara kwa mara Mashariki ya Kati na kufikia makubaliano ya amani.

Wanawake wanapotumia huruma yao wanaweza kubaini mfumo wa wa ukosefu wa haki na kutathmini upya njia ya kusonga mbele.

Danielle Cantor

Sharon Stone

Sharon Stone, Marekani

Muigizaji

Nyota wa filamu za Marekani maarufu Hollywood Sharon Ston ameweka alama katika fani yake ya uigizaji mbele na nyume ya skrini kwa miongo mitatu.

Muigizaji huyo alipata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kupitia filamu ya Basic Instinct, nakuigiza katika filamu zingine maarufu kama vile Total Recal na Casino ambazo zilimfanya kushinda tuzo ya Golden Glibe na kuteuliwa kuwania tuzo ya Oscar.

Pamoja na kazi yake kubwa ya uigizaji, Stone amefanya kazi ya uhisan kuunga mkono mikakati mingi, na kutambuliwa kwa kupewa tuzo ya Amani na washindi wa Nobel kutokana na juhudi zake za kuwasaidia wati wanaoishi na HIV.

Mapema mwaka huu, ufanisi wake ulisherehekewa zaidi baada ya tuzo mpya ya nyota wa kitaifa wa Golden Globe.

Ustahamilivu ni chaguo. Huna budi kuchagua unachotaka. Unaweza kuamua kuendelea kulia kwa maumivu au kulia kwa furaha kutokana na kilie ulichofikia.

Sharon Stone

Madison Tevlin

Madison Tevlin, Canada

Mtangazaji na mwanamitindo

Baada ya kushiriki katika kampeni ya Assume That I can, video ya Madison Tevlin ilipata umaarufu mkubwa mwaka huu na kuzima dhana kuhusu watu walio na ugonjwa Down Syndrome.

Kampeni ya kuhamasisha watu kuhusu hali hiyo ilitazamwa na na zaidi ya watu milioni 150 na kushinda tuzo kutokana namatokeo ykae chanya, ikiwa ni pamoja na simba wa dhahabu wa kifahari katika tamasha la Cannes Lions.

Tevin ambaye ni muigizaji na mwanamitindo aliangaziwa katika Wiki ya mitindo ya New York, akazungumzia ujumuishwaji wa mkakati wa Clinton Global na kupokea tuzo ya uhamasishaji ya Quincy Jones.

Ameandaa kipindi cha mazungumzo kilichopendekezwa kuwania tuzo cha Why Do You Think iAm? na podcast ya the 21 Questions.

Ustahamilivu ni kutokata tamaa kabisa hata wakati ambapo ninahukumiwa au kupuuzwa...Ni kusimamia kile unachoamini na kutokata tamaa iwe ni kwangu binafsi au kwa jamii yangu.

Madison Tevlin

Naomi Watanabe

Naomi Watanabe, Japan

Mchekeshaji

Kama mmoja wa washawishi maarufu zaidi wa Japan, Naomi Watanabe amefungua njia kwa kizazi kipya cha wanawake wachekeshaji nchini mwake.

Amevunja vizuizi katika sanaa ya vichekesho vinavyotawaliwa na wanaume, kujipambanua kama mhusika mkuu wa kike na kuandaa maonyesho maarufu.

Watanabe pia anasaidia kubadili mitazamo kuhusu miili nchini Japani,kwa kuanzisha na kuongoza harakati ya kuwa na mtazamo chanya kuhusu miili inayojulikana kama pochakawaii,ikiwa na maana "tipwatipwa na uzuri".Alizindua mojawapo ya chapa ya kwanza Japani inayotengeza nguo za watu walio na unene kupita kiasi.

Baada ya kupata ufanisi mkubwa katika filamu na televisheni ya kijapani,kwa sasa amehamia Marekani kujitosa katika jukwaa la kimataifa la uchekeshaji.

Je unawezaje kuthubutu kuwa Imara?huwa najiuliza,Kama hunipendi,ni sawa.Naomba unipe muda wa mwaka mmoja huenda nikabadilisha mtazamo wako'.Huu ndio mtazamo huwa nimeushikilia.

Naomi Watanabe

Zhiying(Tania) Zeng

Zhiying(Tania) Zeng, Chile

Mchezaji wa Tenisi ya mezani

Mchina - Mchile na mchezaji tenisi ya mezani Zhiying Zeng- au Tania- alishiriki michezo ya Olompiki kwa mara ya kwanza mwaka 2024 mjini Paris akiwa na umri wa miaka 58.

Ilikuwa suala la muda tu:chini ya ukufunzi wa mama yake aligeukia taaluma ya michezo akiwa na umri wa miaka 12. Alifuzu kujiunga na timu ya taifa ya China lakini baadaye akahamia Chile,ambako aliachana na mchezo huo kwa miaka 30 kuangazia biashara zake.

Janga la Covid-19 ilimfanya Tania kurejelea tenisi ya mezani.

Kufikia mwaka 2023 aliorodheshwa kuwa mchezaji wa ngazi ya juu wa kike nchini Chile, akiiwakilisha taifa lake katika mashindano ya Amerika Kusini na michezo ya Pan American kabla ya kufikia ''ndoto yake ya maisha'' ya kufuzu kwa Olimpiki

Kim Yeji

Kim Yeji, Korea Kusini

Mlenga shabaha wa Olimpiki

Haiba na mafanikio ya michezo ilimafanya Kim Yeji kupata umaarufu kimataifa mwaka huu.

Mlenga shabaha huyo alijishindia medali ya fedha katika ulengaji shabaha wa 10m kwa wanawake katika mashindano yake ya kwanza ya olimpiki mwezi Julai, baada ya kuweka rekodi ya dunia ya ulengaji shabaa wa 25m kwa wanawake miezi kadhaa kabla.

Video zake zilisambaa katika mitandao ya kijamii, sio tu kusifia ujuzi wake bali pia haiba na umakini wake uliwavutia watu sana.

Kim Yeji amezungumza kwa uwazi kuhusu majukumu yanayoambatana na uzazi. Anachukua mapumziko kutoka mchezoni ili kupata muda na binti yake wa miaka sita.

Kupitia michezo tunaonyesha ustahamilivu, kufanya kazi pamoja kwa kujitolea- maadili ambayo kwa mtazamo wangu ni zaidi ya kucheza uwanjani kwasababu inachangia mageuzi ya kijamii

Kim Yeji

Chloe Zhao

Chloe Zhao, Uingereza

Muelekezaji Filamu

Mshindi wa tuzo ya Oscar kwa uelekezaji filamu na mwandishi Chloe Zhao ni mwanamke wa kwanza asiyekuwa mzungu(of colour)- na mmoja kati ya wanawake watatu katika historia - kushinda tuzo ya Academy ya muelekezaji bora

Zhao mzaliwa wa Beijing alihamia Uingereza na Marekani. Anajielezea kama mtu wa kuhamahama- mada inayoenzi filamu yake ya Nomadland(2020)

Kutoka kuangazia jamii yake ya jadi katika filamu zake hadi kuelekeza filamu tofauti za kuvutia kama vile Marvrl Universe, Zhao anahisi kwa shauku kile kinachotuunganisha kama wanadamu.

Mwaka huu amekuwa akielekeza utunzi wa Maggie O'Farrell uliyotokana na riwaya ya Hamnet ya enzi ya Shakespeare ambayo itatolewa mwaka 2025.

Ikiwa hatutabadilisha muundo wa tasnia tunayofanyia kazi, tutakuwa tukimaanisha kwamba tunahitaji kuwa kama wanaume ili kuwa na thamani. Sidhani hapo ndipo nguvu zetu zilipo.

Chloe Zhao

Picha ya baadhi ya washiriki wa msimu huu wa BBC World Service 100 Women

100 Women ni nini?

Wanawake 100 wa BBC huwatambua wanawake 100 mashuhuri kotoka kote duniani kila mwaka. Tunatayarisha makala, taarifa na mahojiano - ambayo yanawapa wanawake kipaumbele na kuzichapisha au kuzitangaza katika majukwaa yote ya BBC

Fuatilia Wanawake 100 wa BBC kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook kwa kutumia #BBC100Women

Wanawake hawa walichaguliwa vipi?

Timu ya BBC 100 Women iliandaa orodha ya majina kwa kuzingatia utafiti uliofanywa na kupendekezwa na mtandao wa Idhaa 41 za BBC na BBC Media Action.

Tulikuwa tunawatafuta wanawake ambao waligonga vichwa vya habari au juhudi zao zilichangia taarifa muhimu katika kipindi cha miezi 12 zilizopita, ikiwa ni pamoja na wale ambao wamefanya vitu vya kutia moyo na kuimarisha jamii zao kwa njia muhimu inga hazikuangaziwa katika vyombo vya habari.

Majina hayo pia yalikaguliwa kulingana na maudhui ya mwaka huu ya ustahamilivu. Tulitaka kutambua changamoto ambazo wanawake walikumbana nazo mwaka huu kote duniani kwa kuwateua wale- ambao kupitia ustahamilivu - wanajitahidi kuimarisha maisha katika ngazi ya kijamii au kimataifa. Pia tulitathmini majina ya wanawake wanaofanya kazi katika nyanja ya mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo kundi la waanzilishi wa miradi inayoangazia hali ya hewa na viongozi wa mazingira waliteuliwa.

Tumejumuisha sauti katika nyanja zote za kisiasa na katika maeneo yote ya kijamii na kuambatanisha majina hayo na mada husika.

Orodha hiyo pia iliandaliwa kwa kuzingatia uwakilishi wa kikanda, na hatua zote za kuhakikisha hakuna upendeleo zilitumiwa kabla orodha ya mwisho ya majina yaliyochaguliwa kutolewa. Wanawake wote wametoa idhini ya kujumuishwa kwenye ordha hii.

Popular posts from this blog

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni