Wizara ya fedha ya Marekani yasema ilidukuliwa na China katika 'tukio kubwa'
Mdukuzi anayefadhiliwa na serikali ya China ameingia katika mifumo ya Wizara ya fedha ya Marekani, na kuweza kuvifikia vituo vya kazi vya wafanyakazi na baadhi ya nyaraka ambazo hazijaainishwa, maafisa wa Marekani walisema Jumatatu.
Udukuzi huo ulifanyika mwanzoni mwa Disemba na uliwekwa wazi katika barua iliyoandikwa na wizara ya fedha kwa wabunge kuwaarifu kuhusu ya tukio hilo.
Wizara hiyo iliutaja udukuzi huo kama "tukio kubwa", na lkuongeza kuwa limekuwa likifanya kazi na FBI na mashirika mengine kuchunguza athari za udukuzi huo.
Msemaji wa ubalozi wa China mjini Washington DC aliiambia BBC News kwamba shutuma hizo ni sehemu ya "mashambulizi yaliyolenga kuharibu sifa" na yalifanywa "bila msingi wowote".
Pamoja na FBI, idara hiyo imekuwa ikifanya kazi na Wakala wa Usalama wa mtandao na miundombinu na wachunguzi wa mahakama wa ili kubaini athari ya jumla ya udukuzi huo.