Posts

Zaidi ya watu 2,500 wameuwawa au kujeruhiwa Haiti

Image
  Zaidi ya watu 2,500 wameuwawa au kujeruhiwa katika ghasia za magenge nchini Haiti kuanzia Januari hadi Machi, zikiwa zimeongezeka kwa asilimia 53 katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2023, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haiti (BINUH) imeeleza. Takriban 590 waliuwawa wakati wa operesheni za polisi, BINU imesema katika ripoti. Imebainika kuna kadhaa ambao hawakuhusika katika vurugu za magenge, baadhi walikuwa na ulemavu wa viungo vya kuwazuia kutembea, na takriban 141 waliuwawa na makundi ya raia yenye hasira na kujichukulia sheria mkononi. Ghasia nyingi zilifanyika katika mji mkuu wa Port-au-Prince, wakati takriban watu 438 wakitekwa nyara katika maeneo mengine ya nchi. Maeneo ya bandari ya La Saline na Cite Soleil ya mji mkuu yalikuwa na mashambulizi makubwa zaidi ya muda mrefu. Wanachama wa magenge waliendelea na vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana katika vitongoji vya wapinzani, magerezani, na kambi za wakimbizi ripoti hiyo

Aliyejichoma moto New York nje ya mahakama ya kesi ya Trump afariki

Image
  Mwanamme mmoja aliyejichoma moto nje ya mahakama ambako kesi ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, inafanyika amefariki dunia polisi wamesema. Idara ya polisi ya jiji la New York, imeiambia The Associated Press Jumamosi kwamba mtu huyo alitangazwa kuwa amekufa na wataalamu wa hospitali ya eneo hilo. Mwanamme huyo alikuwa katika bustani ya Collect Pond, majira ya saa saba na nusu mchana wa Ijumaa, akitoa na kutupa vipeperushi vinavyounga mkono tetesi za njama kisha akajimwagia mafuta na kujichoma moto maafisa na mashahidi wamesema. Idadi kubwa ya polisi walikuwepo karibu na eneo wakati hayo yanatokea. Baadhi yao na raia walikimbilia kumsaidia mtu huyo. Kutokana na majeraha ya moto alilazwa hospitali akiwa katika hali mahutut. Mtu huyo inaelezwa alitokea Florida na kwenda New York siku chache zilizopita.

Mlipuko wa Iraq umeuwa afisa usalama

Image
  Mlipuko mkubwa katika kambi ya jeshi nchini Iraq mapema Jumamosi umemuua afisa wa kikosi cha usalama cha Iraq, kinachojumuisha makundi yanayoungwa mkono na Iran. Kamanda wa kikosi hicho amesema ni shambulizi huku jeshi likisema kuwa linafanya uchunguzi na kulikuwa hakuna ndege za kivita angani wakati wa tukio. Vyanzo viwili vya usalama vilisema hapo awali kwamba shambulizi la anga lilisababisha mlipuko huo, ambao ulimuua afisa wa kikosi cha uratibu cha PMF na kuwajeruhi wengine wanane huko Kalso, kituo cha kijeshi kilichopo karibu kilomita 50 kusini mwa Baghdad. Katika taarifa, PMF imesema mkuu wa wafanyakazi Abdul Aziz al-Mohammedawi alitembelea eneo hilo na kukagua maelezo ya kamati za uchunguzi zilizopo mahali ambapo shambulizi limetokea. Jeshi la Iraq linasema kamati ya kiufundi inafanya uchunguzi wa mlipuko ambao ulitokea saa saba usiku wa kuamkia Jumamosi.

Shambulizi la Israel lauwa 6 Gaza

Image
  Shambulizi la anga ya Israel, kwenye nyumba moja katika mji wa kusini mwa Gaza limesababisha vifo vya watu tisa, sita kati yao wakiwa watoto, maafisa wa hospitali wamesema Jumamosi, wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake ya takriban miezi saba katika eneo lililozingirwa la Palestina. Vita vya Israel dhidi ya kundi la wanamgambo wa Hamas vimesababisha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika eneo ambalo tayari ni tete la Mashariki ya Kati. Mashambulizi hayo yalikwenda kwenye jengo la makazi katika kitongoji cha Tel Sultan magharibi mwa mji wa Rafah, kwa mujibu wa walinzi wa kiraia wa Gaza. Miili ya watoto hao sita, wanawake wawili na mwanamme mmoja ilipelekwa katika hospitali ya Rafah Abu Yousef al-Najjar, taarifa za hospitali hiyo zilionyesha. Hospitalini, jamaa walilia na kuikumbatia miili ya watoto hao ikiwa imefungwa sanda nyeupe huku wengine wakiwafariji.

Urusi yaendeleza mashambulizi ya makombora

Image
  Vikosi vya Russia, vilifyatua makombora saba kutoka mkoa wa Belgorod na Black Sea katika malengo ya Ukraine, Aprili 20, jeshi la anga la Ukraine limeripoti. Makombora mawili ya angani yaliyokuwa yakiongozwa na Kinzhal yaliharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine, kwa mujibu wa jeshi la anga, na kuongeza kuwa pia lilitungua ndege tatu za upelelezi za Russia. Katika wiki za hivi karibuni, Russia, imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine huku akiba ya mifumo ya ulinzi wa anga na risasi za Ukraine ikipungua, na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya raia na uharibifu mkubwa. Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Russia, imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga ilitungua ndege 50 za Ukraine zisizo na rubani katika mikoa minane ya Russia, Aprili 20.

Kwa nini Israel inafanya mashambulizi ya fosforasi nyeupe huko Gaza na Lebanon?

Image
  Chanzo cha picha, AP Saa 1 iliyopita Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, Israel imeendelea kutumia mabomu ya fosforasi nyeupe kuvuka mpaka wa kusini mwa Lebanon. Ikiwa ni gesi yenye sumu, inadhuru macho na mapafu na inaweza kusababisha hali ya kuchoma, na kwa hivyo matumizi yake yanadhibitiwa chini ya sheria za kimataifa. Jeshi la Israel linasema kuwa matumizi yake ya silaha hii yenye utata dhidi ya wanamgambo wa Gaza na Lebanon ni halali. Hata hivyo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema suala hilo linafaa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita. Wamarekani wanasema watachunguza matumizi ya Israel ya fosforasi nyeupe katika nchi zote mbili. Je, kwa kutumia silaha karibu na raia, majeshi ya Israel yanakiuka sheria? Au hii inazingatiwa kweli wakati wa vita? "Silaha hii inaruka kama ukungu mweupe. Lakini inapofika ardhini, inageuka kuwa unga. Ali Ahmed Abu Samra, mkulima mwenye umri wa miaka 48 kutoka kusini mwa Lebanon, anasema alijikuta akizungukwa na wingu zi

Chad yataka Marekani isitishe shughuli za kijeshi nchini humo

Image
  Chad imeitaka Marekani isitishe mara moja kwa shughuli za kijeshi katika kambi ya nchi hiyo iliyo kati ya kaskazini na kati mwa Afrika. Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga la Chad amesema kuwa hajapokea nyaraka zozote kutoka kwa Wamarekani "zinazoonyesha sababu ya wao kuhatajia kuwepo kwao katika Uwanja wa Ndege za Kijeshi wa Adji Kosseï (BAK)" katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena. Kulingana na Jenerali Idris Amin Ahmed, hakuna mfumo wa kisheria wa kuhalalisha uwepo wa jeshi la Marekani katika uwanja huo wa ndege za kijeshi . Hapo awali vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwa Chad iliitishia Marekani kuwa itavunja makubaliano yao ya ulinzi sambamba na kuwataka wanajeshi wa Marekani kuondoka katika kambi ya Ufaransa katika mji mkuu huo. Uamuzi huo ulikuja baada ya nchi jirani ya Niger kusitisha makubaliano ya kijeshi na Marekani. Kuna vituo vya kijeshi vya Ufaransa na Mar