Korea Kaskazini yaangusha maputo ya taka taka Korea Kusini
Korea Kaskazini imeangusha takriban maputo 260 yaliyokuwa yamebeba taka Kusini, na kusababisha mamlaka kuwaonya wakazi wake kusalia majumbani. Jeshi la Korea Kusini pia lilionya umma dhidi ya kugusa puto nyeupe na mifuko ya plastiki iliyowekwa ndani yake kwa sababu ina "takataka na takataka". Puto hizo zimepatikana katika majimbo manane kati ya tisa nchini Korea Kusini na sasa yanachambuliwa. Korea Kaskazini na Kusini zimetumia puto katika kampeni zao za propaganda tangu Vita vya Korea katika miaka ya 1950. Awali jeshi la Korea Kusini lilikuwa limesema linachunguza iwapo kulikuwa na vipeperushi vyovyote vya propaganda za Korea Kaskazini kwenye puto hizo. Tukio la hivi majuzi linakuja siku chache baada ya Korea Kaskazini kusema italipiza kisasi dhidi ya "kutawanywa mara kwa mara kwa vipeperushi na takataka nyingine" katika maeneo ya mpaka na wanaharakati Kusini. "Marundi ya karatasi taka na uchafu hivi karibuni vitatawanywa kwenye maeneo ya mpaka na ndani ya ROK