Msitari wa mbele wa Ukraine kuanguka muda wowote majira ya joto-gazeti

 


Kulingana na tathmini za gazeti hilo, Urusi "haijawahi kuwa karibu na malengo yake" katika eneo maalum la operesheni ya kijeshi kama ilivyo sasa hivi

Msimamo ambao Ukraine imekuwa ikishikilia kwa miezi kadhaa iliyopita katika eneo maalum la operesheni ya kijeshi huenda ukaporomoka msimu huu wa joto, Politico iliripoti, ikitoa mfano wa maafisa kadhaa wa ngazi za juu.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mstari wa mbele wa Ukraine huenda ukaporomoka msimu huu wa joto kutokana na mashambulizi ya Urusi yanayodhaniwa kuwa makubwa na makali sana, kwani majeshi ya Urusi ni mengi zaidi ya yale ya Ukraine. Duru za gazeti hilo zilisema hali ni ngumu kutokana na ukosefu wa silaha za Magharibi, jambo ambalo linadhoofisha ari ya wanajeshi wa Ukraine. Politico ilisema kuwa maofisa wa Ukraini "wanakubali kwa faragha kwamba hasara zaidi [za eneo] haziepukiki msimu huu wa joto," swali ni jinsi watakavyoweza kupambana na kulinda maeneo muhimu. Kulingana na tathmini ya gazeti hilo, Urusi "haijawahi kuwa karibu na malengo yake" katika maeneo maalum ya operesheni za kijeshi kama ilivyo wakati huu, wakati ambapo Ukraine inaonesha wazi wazi kulemewa katika nyanja zote

Hapo awali, Kamanda Mkuu wa Ukraine Alexander Syrsky aliandika kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba hali yamsitari wa  mbele imeongezeka kuwa  hatari. Mnamo Aprili 16, Rais wa Ukrain Vladimir Zelensky alitia saini mswada wa kuimarisha uhamasishaji, ambao ungeruhusu kuandikishwa kwa mamia ya maelfu zaidi ya Waukreni.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo