Watu 1,300 wa Myanmar wamekimbilia Thailand

 



Takriban watu 1,300 wamekimbia kutoka mashariki mwa Myanmar kuelekea Thailand, maafisa wamesema Jumamosi, wakati mapigano mapya yakizuka katika mji wa mpakani ambao hivi karibuni ulitekwa na wapiganaji wa msituni wa kikabila.

Wapiganaji kutoka kabila la walio wachache la Karen wiki iliyopita waliiteka ngome ya mwisho ya jeshi la Myanmar ndani na kuzunguka Myawaddy, ambayo imeungana na Thailand kwa madaraja mawili katika Mto Moei.

Mapigano ya karibuni kabisa yalizuka asubuhi wakati wapiganaji wa msituni wa Karen walipoanzisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Myanmar waliokuwa wamejificha karibu na daraja la pili la urafiki la Thailand na Myanmar, kivuko kikuu cha biashara na Thailand, alisema mkuu wa polisi Pittayakorn Phetcharat katika wilaya ya Mae Sot nchini Thailand.

Alikadiria kuwa akriban watu 1,300 walikimbilia Thailand.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo