Harakati za kumkutanisha rais wa Rwanda na mwenzake wa DRC zinaendelea

 Mchakato wa Nairobi wa kusaka amani mashariki mwa DRC umeendelea kuingia dosari kutokana na matukio kadhaa wakati ule wa Luanda ukifufuliwa kuhakikisha viongozi wa Rwanda na DRC wanakutana. 

Kinshasa inachukulia kuwa mchakato wa Nairobi ulishindwa kufikia ufanisi wake na sasa umesimama ambapo matukio ya hivi karibuni kati ya Kenya mwenyeji wa mazungumzo na DRC ndio imekuwa sababu.

Viongozi wa DRC walilaani hatuwa ya Corneille NangaA kutangaza uasi akiwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, jambo ambalo lilisababisha Kinshasa kumrejesha nyumbani balozi wake jijini Nairobi.

Corneille Nangaa, anatuhumiwa na Kinshasa kwa kutangaza uasi akiwa jijini Nairobi.
Corneille Nangaa, anatuhumiwa na Kinshasa kwa kutangaza uasi akiwa jijini Nairobi. AFP - LUIS TATO

Kuanzia hapo juhudi za kurejesha hali katika usawa ziliendelea kufanyika. Lakini kauli ya hivi karibuni ya rais wa Kenya William Ruto kwenye vyombo vya habari kwamba swala la M23 ni tatizo la wakongomani, kauli ambayo haikupokelewa vizuri na viongozi wa DRC.

Tamko hilo la rais Ruto ambalo halikulaaniwa na jumuiya ya nchi za kikanda inavunja uaminifu kwa taasisi hiyo ya kikanda kulingana na mmoja miongoni mwa washauri wa Felix Thisekedi.

Kauli ya rais William Ruto kuhusu suala la M23 imelaaniwa vikali na Kinshasa.
Kauli ya rais William Ruto kuhusu suala la M23 imelaaniwa vikali na Kinshasa. AFP - ARSENE MPIANA

Hata hivyo, usuluhishi wa Angola unaendelea ambapo hivi karibuni majadiliano yanatarajia kuanza tena.

Waziri wa mambo ya nje wa DRC amekutana na mwenzake wa Angola mwishoni mwa juma lililopita, kulingana na duru mbalimbali DRC na Rwanda wote wamewasilisha mipango yao ambapo Kinshasa imewasilisha mpango wake wa kuwaondoa wapiganaji wa FDLR na kusisitiza kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Congo.

Paul Kagame wa Rwanda , João Lourenço wa Angola na Felix Thisekedi wa DRC katika mkutano wa awali
Paul Kagame wa Rwanda , João Lourenço wa Angola na Felix Thisekedi wa DRC katika mkutano wa awali AFP - JORGE NSIMBA

Mazungumzo yataendelea kwenye ngazi ya wizara kwa dhamira ya kuandaa mkutano baina ya Kagame na Felix Tshisekedi.

 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo