'Kusitisha vita dhidi ya Hamas ni kujiua hadharani' - msemaji wa Israel aiambia BBC


 

Msemaji wa serikali ya Israel David Mencer amekuwa akizungumza na BBC: "Hakuna mamlaka duniani ambayo itatusukuma kujitoa uhai hadharani, ili kusitisha vita vyetu dhidi ya Hamas."

Mawaziri wa baraza la mawaziri la Israel wanakutana baadaye kujadili uamuzi wa mahakama ya ICJ lakini maafisa wa serikali wamesema hapo awali kwamba hakuna mamlaka yoyote duniani ambayo inaweza kuizuia Israel kuwalinda raia wake na kkukabiliana na kundi la Hamas huko Gaza.

Mamlaka ya Palestina (PA) - ambayo inaendesha sehemu za Ukingo wa Magharibi unaokaliwa - na Hamas - ambayo inaendesha Gaza na kushambulia jamii za karibu za Israeli tarehe 7 Oktoba, na kusababisha vita vya sasa - wamekaribisha uamuzi huo.

Hata hivyo Hamas inasema wito wa kusitisha mashambulizi unapaswa kuhusisha Gaza yote na sio Rafah pekee.

Uamuzi huo "unawakilisha makubaliano ya kimataifa kumaliza vita kwenye Ukanda wa Gaza," msemaji wa rais wa PA Nabil Abu Rudeina ameliambia shirika la habari la Reuters.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo