Majeshi ya Israel yawaua makumi ya Wapalestina katika mashambulizi ya Gaza

 .

Vikosi vya Israel viliwaua Wapalestina 60 katika mashambulizi ya anga na ardhini katika Ukanda wa Gaza siku ya Alhamisi na kupigana kwa karibu na wanamgambo wanaoongozwa na Hamas katika maeneo ya mji wa kusini wa Rafah, maafisa wa afya na vyombo vya habari vya Hamas wamesema.

Vifaru vya Israel vilisonga mbele katika kusini mashariki mwa Rafah, kuelekea wilaya ya magharibi ya mji wa Yibna na kuendeleza operesheni yake katika vitongoji vitatu vya mashariki, wakaazi walisema.

Reuters imezungumza na mkaazi mmoja ambaye alisema, "Majeshi ya Israel yanajaribu kusonga mbele zaidi kuelekea magharibi, yapo kwenye ukingo wa Yibna, ambako kuna watu wengi. Bado hawajaivamia," mkazi mmoja alisema, akiomba jina lake lisitajwe.

"Tunasikia milipuko na tunaona moshi mweusi ukitoka katika maeneo ambayo jeshi limevamia. Ulikuwa usiku mwingine mgumu sana," aliambia Reuters kupitia programu ya mazungumzo.

Israel ilianzisha mashambulizi yake huko Gaza kufuatia shambulio lililoongozwa na Hamas dhidi ya jamii za kusini mwa Israeli mnamo Oktoba 7 na kuua watu 1,200 huku zaidi ya 250 wakichukuliwa kama mateka.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo