Mawaziri 13 wa Mambo ya Nje wakiwemo 6 wa G7 waitaka Israel isitishe uvamizi wa ardhini wa Rafah


  • Mawaziri 13 wa Mambo ya Nje wakiwemo 6 wa G7 waitaka Israel isitishe uvamizi wa ardhini wa Rafah

Shirika la habari la DPA la Ujerumani limeripoti kuwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 13 wametia saini barua ya kuuonya na kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe uvamizi wake wa ardhini katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada zaidi kuwafikia Wapalestina.

Ikinukuu ripoti katika gazeti la Suddeutsche Zeitung la Ujerumani, DPA imeripoti kuwa, ukiondoa Marekani, wanachama wengine wote wa Kundi la Mataifa Saba yaliyoendelea kiviwanda (G7) wametia saini barua hiyo ya kurasa nne ambayo iliandikwa siku ya Jumatano.

Katika barua iliyotumwa kwa waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel Israel Katz, mawaziri hao wameitaka serikali ya Benjamin Netanyahu ipunguze hali ya uharibifu na inayozidi kuwa mbaya ya kibinaadamu huko Ghaza kwa kufungua vivuko vyote vya mpakani kwa ajili ya kuingizwa misaada, ikiwa ni pamoja na kivuko cha Rafah na Misri, ambacho hivi sasa kiko chini ya udhibiti wa kijeshi wa utawala huo wa Kizayuni.

Barua hiyo ilitiwa saini na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi sita wanachama wa G7 ambazo ni Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Japan na Canada, pamoja na wenzao kutoka Australia, Denmark, Finland, Uholanzi, New Zealand, Korea Kusini na Sweden…/

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo