Mbu waliobadilishwa vinasaba waachiliwa nchini Djibouti kupambana na malaria

 .

Makumi ya maelfu ya mbu waliobadilishwa vinasaba (GMO) wameachiliwa nchini Djibouti katika juhudi za kukomesha kuenea kwa spishi vamizi wanaosambaza malaria.

Mbu dume wasiouma aina ya Anopheles stephensi mbu waliotengenezwa na Oxitec, kampuni ya teknolojia ya kibayoteknolojia yenye makao yake makuu nchini Uingereza, hubeba jeni inayoua watoto wa kike kabla ya kukomaa.

Mbu jike pekee ndio wanaouma na kusambaza malaria na magonjwa mengine ya virusi.

Ni mara ya kwanza kwa mbu wa aina hiyo kutolewa Afrika Mashariki na mara ya pili barani humo.

Teknolojia kama hiyo imetumika kwa mafanikio nchini Brazil, Visiwa vya Cayman, Panama, na India, kulingana na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Zaidi ya mbu kama hao bilioni moja wameachiliwa kote ulimwenguni tangu 2019, CDC inasema.

Kundi la kwanza la mbu hao waliachiliwa hewani siku ya Alhamisi huko Ambouli, kitongoji cha jiji la Djibouti.

Ni hatua ya majaribio katika ushirikiano kati ya Oxitec Ltd, serikali ya Djibouti na shirika lisilo la kiserikali la Mutualis.

“Tumetengeneza mbu wazuri wasiouma, wasioambukiza magonjwa. Na tunapowaachilia mbu hawa rafiki, wao hutafuta na kujamiiana na mbu wa kike mbaya,” mkuu wa Oxitec Gray Frandsen aliambia BBC.

Mbu hao wanaozalishwa katika maabara hubeba jeni ya "kujizuia" ambayo huzuia watoto wa mbu wa kike kuishi hadi utu uzima wanapooana.

Ni watoto wao wa kiume pekee wanaosalia lakini hatimaye wangekufa, kulingana na wanasayansi wa mradi huo.

Tofauti na mbu dume aina ya Anopheles colluzzi waliotolewa nchini Burkina Faso mwaka wa 2018, mbu hao rafiki wa stephensi bado wanaweza kupata watoto.

Kuachiliwa kwa mbu hao ni sehemu ya Mpango Rafiki wa Mbu wa Djibouti ambao ulianzishwa miaka miwili iliyopita ili kukomesha kuenea kwa Anopheles stephensi, aina vamizi ya mbu waliogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 2012.

Wakati huo nchi ilikuwa kwenye hatihati ya kutokomeza malaria, wakati ilirekodi karibu visa 30 vya malaria. Tangu wakati huo, kesi za malaria zimeongezeka kwa kasi nchini hadi 73,000 kufikia 2020.

Spishi hiyo sasa ipo katika nchi nyingine sita za Afrika - Ethiopia, Somalia, Kenya, Sudan, Nigeria na Ghana.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo