Miili mingine mitatu ya mateka wa Israel yapatikana Gaza

 xx

Miili ya mateka wengine watatu wa Israel imeopolewa kutoka Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema.

Ni wale wa Hanan Yablonka, Michel Nisenbaum na Orion Hernandez, ilisema katika taarifa yake.

IDF ilisema miili hiyo ilipatikana katika mji wa kaskazini wa Jabalia katika operesheni ya pamoja na shirika la kijasusi la Israel iliyofanyika usiku kucha.

Hii inakuja wiki moja baada ya miili mingine mitatu ya mateka kupatikana huko Gaza.

Mateka waliouawa walikuwa miongoni mwa watu 252 waliotekwa nyara wakati wapiganaji wenye silaha wa Hamas waliposhambulia Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua takriban watu 1,200.

Kuna takriban mateka 130 ambao bado wanashikiliwa huko Gaza, Israel inasema.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo