Mwanaume apigwa risasi hadi kufa baada ya sinagogi la Ufaransa kuchomwa moto

 k

Polisi wa Ufaransa wamemuua mwanamume mmoja baada ya sunagogi kuchomwa moto katika mji wa kaskazini-magharibi wa Rouen.

Mwanamume huyo ambaye alikuwa amejihami kwa kisu na kifaa cha chuma alipigwa risasi baada ya kuwatishia maafisa, mwendesha mashtaka wa Rouen amesema.

Meya wa Rouen, Nicolas Mayer-Rossignol amesema shambulio dhidi ya sinagogi halikuathiri tu jamii ya Wayahudi, bali jiji zima "limepigwa na mshtuko".

Ripoti za Ufaransa zinasema mshukiwa huyo alikuwa raia wa Algeria na alikuwa akikata rufaa dhidi ya amri ya kuondoka Ufaransa.

Polisi waliitwa mwendo wa saa moja kasoro robo (04:45 GMT) baada ya moshi kuonekana ukitoka katika sinagogi.

Mshambuliaji huyo alipanda juu ya pipa kubwa la taka na kurusha bomu la petroli kupitia dirisha dogo, na kulichomo moto sinagogi.

Maafisa wawili wa polisi walifika eneo la tukio kwa kasi, baada ya mtu huyo kuonekana kwenye kamera za ulinzi.

Mshukiwa alikuwa juu ya paa la sinagogi walipofika, kulingana na waendesha mashtaka.

"Afisa alifyatua risasi mara tano, na kumpiga mtu huyo mara nne," mwendesha mashtaka wa umma wa Rouen Frédéric Teillet, alieleza kwamba alikuwa ameona picha kwenye kamera za usalama.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo