Mwanaume mmoja aambiwa yeye si Muingereza baada ya miaka 42 kuishi Uingereza

 aZ

Mwanaume mmoja - mfanyakazi mstaafu kutoka Ghana mwenye umri wa miaka 74 ambaye ameishi Uingereza kwa karibu miaka 50 - Nelson Shardey, kutoka Wallasey huko Wirral, kwa miaka mingi alikuwa akidhani amekuwa raia rasmi wa Uingereza.

Aligundua kumbe sivyo mwaka 2019, licha ya kulipa ushuru maisha yake yote ya utu uzima, na sasa anakabiliwa na malipo ya maelfu ya pauni ili kukaa na kutumia huduma za afya za NHS.

Ofisi ya Mambo ya Ndani ilikataa kutoa maoni kuhusu kesi hiyo ya kisheria inayoendelea.

'Sijawahi kuulizwa'

Wakala wa magazeti aliyestaafu Shardey alikwenda Uingereza kwa mara ya kwanza mwaka 1977 kusomea uhasibu, kwa viza ya mwanafunzi ambayo pia ilimruhusu kufanya kazi.

Baada ya mapinduzi katika nchi yake ya asili ya Ghana familia yake haikuweza tena kumtumia pesa za ada. Ndipo akaamua kufanya kazi, na anasema hakuna mtu aliyewahi kuhoji haki yake ya kuishi au kufanya kazi nchini Uingereza.

Alioa mwanamke wa Uingereza na kuhamia Wallasey ili kuendesha biashara yake mwenyewe, akiitwa muuza magazeti ama Nelson's News.

Ndoa hiyo ilipoisha, alioa mwanamke mwingine wa Uingereza na wakapata wana wawili Jacob na Aaron.

"Nilijaribu niwezavyo kuwapa elimu bora," anasema Shardey. Aliwaambia wanawe "wasome kwa bidii ili wapate kazi nzuri."

Wote wawili walisoma hadi chuo kikuu na mmoja akawa mtafiti na mwingine akasomea mahusiano ya umma.

Shardey alisema hajawahi kuondoka Uingereza, kwani hakuona haja na alipaona kama nyumbani kwake.

“Hakuna aliyehoji, nilinunua vitu vyangu vyote hata nyumba. Na hakuna mtu aliyenihoji kuhusu chochote," anasema.

Shardey amefanya kazi katika baraza la wazee wa mahakama, na mwaka 2007 alipewa tuzo ya ushujaa baada ya kukabiliana na jambazi ambaye alikuwa akimshambulia msafirisha bidhaa za watu kwa rungu.

Kumbe hakuwa Mwingereza

xc

Chanzo cha picha, Nelson Shardey

Maelezo ya picha, Nelson Shardey akipokea tuzo yake ya ushujaa 2007

Lakini mwaka 2019, alipoomba pasipoti ili aweze kurejea Ghana kufuatia kifo cha mama yake, aliambiwa hakuwa Muingereza.

Ofisi ya Mambo ya Ndani ilisema hakuwa na haki ya kuwa nchini Uingereza.

Maafisa walimwambia atume ombi la kuomba ukaaazi rasmi wa baada ya miaka 10. Ndani ya kipindi cha miaka 10 itamgharimu takribani pauni 7,000 kuishi, na pauni 10,500 zaidi katika kipindi hicho hicho ili kupata huduma za afya.

"Siwezi kumudu kulipa pesa hizo," alisema Shardey, ambaye anapata nafuu kutokana na matibabu ya saratani ya tezi dume.

"Kuniambia nifanye malipo hayo ni adhabu, na sio haki kwa njia yoyote ile. Sielewi kwa nini kuna hii shida, kwa sababu niliweka maisha yangu yote katika nchi hii."

Alipojaribu kuongeza haki yake ya kukaa Uingereza mtandaoni miaka miwili iliyopita, alijaza fomu isiyo sahihi. Hiyo ilimaanisha mchakato wa kusubiri miaka 10 utaanza tena upya 2023.

Kwa hivyo, Shardey hataruhusiwa kisheria kukaa Uingereza moja kwa moja hadi atakapofikisha umri wa miaka 84.

"Nilidhani ni utani. Ni ujinga," alisema mwanawe Jacob, ambaye anafanya utafiti wa moyo, mishipa na damu.

"Kwa nini asubiri miaka 10 wakati amekuwa hapa tangu 1977? Amekuwa hapa kwa muda mrefu zaidi kuliko watu ambao wanafanya kazi katika Ofisi ya Mambo ya Ndani juu ya kesi yake."

Mambo ya Kisheria

ZX

Chanzo cha picha, Nelson Shardey

Maelezo ya picha, Nelson Shardey na wanawe wawili walipokuwa wadogo

Kwa usaidizi wa Nicola Burgess, wakili katika kitengo cha Msaada kwa Wahamiaji cha Greater Manchester (GMIAU), Shardey sasa anaipeleka Ofisi ya Mambo ya Ndani mahakamani.

Kesi yake - ambayo wanawe wanajaribu kulipia kupitia ufadhili wa watu. Anaamini Ofisi ya Mambo ya Ndani ilipaswa kuliangalia jambo lake kwa namma tofauti kwa sababu ya muda mrefu ambao amekuwa nchini Uingereza, na tuzo yake ya ushujaa na huduma kwa jamii. .

"Tunamjua mfanyakazi mmoja wa kijamii ambaye ameangalia faili lake na kupendekeza apewe ruhusa ya kubaki kwa muda usiojulikana kwa sababu ni kesi ya kipekee," Bi Burgess alisema.

"Na unapoiangalia kesi yake katika ngazi ya binafsi, kama Nelson angekuwa rafiki yako au jirani yako, ungekubali haraka apewe haki ya kukaa."

Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Ndani alisema; "haifai kutoa maoni juu ya kesi zinazoendelea kisheria."

 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo