Nchi zaidi zatangaza maombolezo ya kitaifa kufuatia kufa shahidi Rais Raisi wa Iran

 

May 22, 2024 02:22 UTC
  • Nchi zaidi zatangaza maombolezo ya kitaifa kufuatia kufa shahidi Rais Raisi wa Iran

Kufuatia kufa shahidi Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi, nchi nyingi duniani zimetangaza maombolezo ya kitaifa, huku viongozi wa kimataifa wakiendelea kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na taifa la Iran.

Msitu wa Dizmar katika Mkoa wa Azarbaijan Mashariki ulikuwa eneo la ajali mbaya ya helikopta siku ya Jumapili, na kusababisha vifo vya Rais Raisi na ujumbe alioandamana nao.

Mbali na Rais, ndani ya helikopta hiyo walikuwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tabriz Seyyed Mohammad Ali Al-e Hashem na mwanachama wa timu ya walinzi wa rais Mahdi Mousavi. Rubani wa helikopta, rubani mwenza na wahudumu wa ndege pia walikuwa miongoni mwa wengine waliokuwa kwenye helikopta hiyo.

Huku kukiwa na hali mbaya ya hali ya hewa, timu za watafutaji zilifanikiwa kupata mabaki ya helikopta iliyoteketea baada ya kufanyika upekuzi wa kina. Kwa bahati mbaya, ilithibitishwa kuwa abiria wote waliokuwemo walikufa shahidi.

Baada ya habari hizo kuenea, risala za rambirambi zimekuwa zikimiminika Iran kutoka duniani kote, huku nchi kama Syria, Lebanon, Iraq, India, Pakistan, Tajikistan, Uturuki, Cuba na Sri Lanka zikitangaza maombolezo ya kitaifa.

Serikali za Syria na Lebanon zilitangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 3, wakati India, Iraq na Pakistan zikitangaza maombolezo ya siku moja ya serikali. Serikali ya Tajikistan pia imetangaza siku mbili za maombolezo.

Siku ya Jumanne, Uturuki, Cuba, na Sri Lanka zilitangaza maombolezo ya siku moja ya umma kuonyesha mshikamano na watu na serikali ya Iran.

Rais Raisi na ujumbe alioandamana nao walikuwa wakirudi kutoka kwenye sherehe za ufunguzi wa bwawa kwenye Mto Aras ambayo pia ilihudhuriwa na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo