Papa aashiria uwezekano wa 'mshawishi wa Mungu' kuwa mtakatifu

 .

Kijana mzaliwa wa London - ambaye ustadi wake wa kueneza mafundisho ya kanisa katoliki mtandaoni ulimfanya aitwe "mshawishi wa Mungu" - anatarajiwa kuwa mtakatifu.

Carlo Acutis alifariki dunia mwaka wa 2006, akiwa na umri wa miaka 15, ikimaanisha kuwa angekuwa milenia wa kwanza - mtu aliyezaliwa mapema miaka ya 1980 hadi mwishoni mwa miaka ya 1990 - kutangazwa kuwa mtakatifu.

Inafuatia Papa Francis kuhusisha muujiza wa pili kwake.

Ilihusisha uponyaji wa mwanafunzi wa chuo kikuu huko Florence ambaye alikuwa na damu kwenye ubongo baada ya kuumia kichwa.

Carlo Acutis alikuwa ametangazwa mwenye heri - hatua ya kwanza kuelekea utakatifu - mnamo 2020, baada ya kuhusishwa na muujiza wake wa kwanza - kumponya mtoto wa Brazil kutokana na ugonjwa wa kuzaliwa ulioathiri kongosho yake.

Muujiza wa pili uliidhinishwa na Papa kufuatia mkutano na idara ya watakatifu ya Vatican.

Bado haijajulikana ni lini atatangazwa kuwa mtakatifu.

Carlo Acutis alifariki dunia huko Monza, nchini Italia, baada ya kugundulika kuwa na saratani ya damu, akiwa ametumia muda mwingi wa utoto wake nchini humo.

Mwili wake ulihamishwa hadi Assisi mwaka mmoja baada ya kifo chake, na kwa sasa unaonyeshwa wanaotembelea eneo hilo.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo