Shambulio Rafah: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura

 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana kwa dharura leo Jumanne mchana kujadili hali ya Rafah. Mkutano huo, ambao haujafungwa, uliombwa na Algeria, mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza, vyanzo kadhaa vya kidiplomasia vimeliambia shirika la habari la AFP. 

Dakika 2

Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York.
Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York. ©REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) litakutana kwa dharura Jumanne alasiri kujadili hali ya Rafah baada ya shambulio baya ambao lilichoma mahema yaliyokuwa yakikaliwa na Wapalestina katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao, ilitangazwa Jumatatu kutoka kwa vyanzo vya kidiplomasia.

Israel inaongeza mashambulizi mjini Rafah siku ya Jumanne licha ya nchi kadhaa na viongozi kadhaa duniani kulani mashambulizi yake mabaya ya anga dhidi ya kambi ya watu waliokimbia makazi yao ambayo ilisukuma Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano wa dharura kuhusu hali katika eneo hili la Gaza.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa uchunguzi "kamili na wa uwazi" kuhusu shambulio la bomu la Rafah.

Jeshi la Ulinzi la Raia la Palestina liliripoti miili mingi "iliyoteketea" katika moto huo ambao uliteketeza kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya Barkasat, inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), kaskazini magharibi mwa Rafah.

"Tuliona miili iliyochomwa, iliyokatwa vipande vipande... kesi za kukatwa viungo, watoto waliojeruhiwa, wanawake na wazee," ameshuhudia Mohammed al-Mughayyir, afisa wa Ulinzi wa Raia katika Ukanda wa Gaza.

Picha kutoka shirika la Hilali Nyekundu la Palestina, kulingana na eneo lililolengwa na shambulio hilo liliteuliwa na Israeli "kama eneo la kibinadamu", zinaonyesha matukio ya machafuko, ambulensi zenye ving'ora na waokoaji katikati ya usiku kwenye eneo linalowaka moto , kuwahamisha majeruhi wakiwemo watoto.

Baada ya ICJ

Shambulio hilo la mauaji dhidi ya Rafah lilikuja saa chache baada ya mashambulizi ya roketi, yaliyodaiwa na Hamas, kwenye mji mkuu wa Israel Tel-Aviv kutoka Rafah, lakini pia siku mbili baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa, ambayo iliamuru Israel siku ya Ijumaa kusitisha mashambulizi yake mjini Rafah.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, operesheni hii tayari zimesababisha, katika karibu wiki tatu, Wapalestina wapatao 800,000 kukimbia, na hivyo kuwalazimu watu ambao walijaribu kupata hifadhi huko Rafah mapema katika vita kuhama tena.

Vita hivyo vilichochewa na shambulio lililotekelezwa Oktoba 7 katika ardhi ya Israel na makomando wa Hamas waliojipenyeza kutoka Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,170, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya AFP iliyofanywa kulingana na data rasmi ya Israeli.

 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo