Uhispania, Norway na Ireland kuitambua rasmi taifa huru la Palestina

 Nchi tatau za Ulaya Uhispania, Norway na Ireland zitalitambua Taifa la Palestina leo Jumanne katika mkutano na waandishi wa habari mjini Brussels, tangazo lililotolewa wiki iliyopita na ambalo liliamsha hasira kwa Israel.

Dakika 1

Maandamano ya kuunga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York, Aprili 22, 2024.
Maandamano ya kuunga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York, Aprili 22, 2024. REUTERS - Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez alitangaza hivi karibuni kwamba nchi yake italitambua Taifa la Palestina tarehe 28 Mei.

Takriban nchi 140 zimelitambua taifa la Palestina, kulingana na barua ya hivi majuzi kwa Umoja wa Mataifa.

nchi hizo zinajumuisha wanachama wa Kundi la nchi 22 za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi 57 za Ushirikiano wa Kiislamu na Harakati Zisizofungamana na Siasa zenye wanachama 120.

Uingereza na Marekani ni miongoni mwa mataifa ambayo hayaitambui rasmi taifa la Palestina.

Mapema mwezi huu waziri wa mambo ya nje Bwana Cameron alipendekeza kuwa serikali, pamoja na washirika wake, inaweza "kuangalia suala la kulitambua taifa la Palestina, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa".

Israel haitambui utaifa wa Palestina na serikali ya sasa ya Israel inapinga kuundwa kwa taifa la Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Gaza. Inasema kuwa hali kama hiyo itakuwa tishio kwa uwepo wa Israeli.

 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo