Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani 2024

 

.

Cristiano Ronaldo ameongoza orodha ya Forbes ya wanariadha wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mara ya nne katika maisha yake ya soka, huku Jon Rahm mcheza gofu akipanda hadi nafasi ya pili.

Ronaldo pia aliongoza orodha hiyo mwaka jana baada ya kuhamia klabu ya soka ya Saudi Arabia ya Al Nassr.

Jarida la biashara la Forbes linasema, mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 39 alipata kiasi cha $260m (£205m) - kutoka $136m (£108.7m) - katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Mpinzani mkubwa wa Ronaldo Lionel Messi ameporomoka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Rahm.

Mchezaji gofu wa Uhispania amepanda hadi nafasi pili nyuma kabla ya kufanyika kwa safari yake ya kwenda kucheza Gofu ya LIV inayofadhiliwa na Saudia na anaripotiwa kupata $218m (£172m).

Mcheza gofu huyo wa Uhispania ni mmoja wa wanariadha 22 walio na umri wa chini ya miaka 30 kwenye orodha hiyo, jambo ambalo linaweza kuashiria mabadiliko.

Wachezaji waliodumu katika hiyo orodha kama vile Serena Williams, Roger Federer na Tom Brady tayari wamestaafu , wakati Ronaldo, LeBron James, Tiger Woods na wanariadha wengine watatu wenye umri wa miaka 39 au zaidi, pia nao wakitarajiwa kuchukua hatua hiyo hivi karibuni.

Wanasoka Neymar na Karim Benzema pia wameingia kwenye 10 bora baada ya kuhamia katika ligi ya soka ya Saudi Pro League.

Giannis Antetokounmpo (katika nafasi ya tano) anaungana na nyota wenzake wa mpira wa vikapu LeBron James (wa nne) na Stephen Curry (wa tisa) kwenye orodha hiyo , huku beki wa pembeni wa kandanda wa Marekani Lamar Jackson akiwa katika nafasi ya 10.

Kulingana na Forbes, wanariadha 10 wanaolipwa zaidi duniani kwa pamoja walipata kiasi cha $1.38 bn (£1.06bn) kabla ya ushuru na ada za mawakala katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, ambayo ni jumla ya juu zaidi kuwahi kutokea.

Katika nafasi ya 14 bora , Canelo Alvarez bondia ambaye alikulia katika maisha ya umaskini wa mashambani na alianza kupigana akilipwa dola 40, anakadiriwa na Jarida la Forbes kuna na thamani ya angalau $275 milioni.

Katika nafasi ya 16 ni bondia wa uzani mzito duniani Anthony Joshua kutoka Uingereza anayedaiwa kuwa na thamani ya $83m.

Joshua alishinda mapambano yake ya kwanza 22 ya kulipwa na alikuwa bingwa wa dunia kutoka 2016 hadi 2019, hadi alipopoteza kwa Andy Ruiz Jr.

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Halaand ambaye ameorodheshwa katika nafasi ya 27 ana thamani ya $61m.

Akiwa miongoni mwa nyota wanaochipuka kwa kasi katika soka, Haaland aliamuru ada ya uhamisho ya dola milioni 63 katika uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester City mnamo 2022.

Mchezaji soka kutoka Afrika anayelipwa fedha nyingi zaidi ni Mohammed Salah kutoka Misri mwenye thamani ya $53m. Salah anashikilia nafasi ya 38.

Nyuma yake ni Sadio Mane mshambuliaji wa Senegal mwenye thamani ya $52m katika nafasi ya 40.

Mané ndiye nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya soka ya Senegal. Alimfuata Cristiano Ronaldo hadi klabu ya Saudi Pro League ya Al Nassr baada ya kukaa msimu wa 2022-23 na klabu ya Ujerumani Bayern Munich.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 10 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani

1. Cristiano Ronaldo, football: $260m (£205m)

2. Jon Rahm, Gofu: $218m (£172m)

3. Lionel Messi, Soka: $135m (£107m)

4. LeBron James, Mpira wa vikapu: $128.2m (£101m)

5. Giannis Antetokounmpo, Mpira wa vikapu: $111m (£88m)

6. Kylian Mbappe, Soka $110m (£87m)

7. Neymar, Soka: $108m (£85m)

8. Karim Benzema, Soka: $106m (£84m)

9. Stephen Curry, Mpira wa vikapu $102m (£80m)

10. Lamar Jackson, Soka ya Marekani: $100.5m (£79m)

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo