Yote unayopaswa kujua kuhusu uchaguzi wa Afrika Kusini 2024

 


Rais Cyril Ramaphosa anasema mafanikio ya ANC hayapaswi kusahaulika

Chanzo cha picha, AFP

Raia wa Afrika Kusini wanashiriki uchaguzi mkuu leo Mei 29, huku baadhi ya kura zikipendekeza chama tawala cha African National Congress (ANC) kinaweza kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30.

Ukosoaji unaoongezeka dhidi ya chama kilichoongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi chini ya hayati Nelson Mandela umepunguza uungwaji mkono wake, na kuongeza uwezekano wa serikali ya mseto.

Uchaguzi wa Afrika Kusini utafanyika lini?

Tarehe 29 Mei, karibu wapiga kura milioni 28 wa Afrika Kusini waliojiandikisha wana nafasi ya kuchagua wawakilishi katika mabunge ya kitaifa na majimbo.

Utakuwa uchaguzi mkuu wa saba wa kidemokrasia nchini humo.

Umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano tangu 1994, wakati utawala wa weupe wachache ulipoisha na ANC kuingia madarakani.

Ni nini kiko hatarini kwa ANC na sera zake ni zipi?

Chama cha ANC ambacho sasa kinaongozwa na Rais Cyril Ramaphosa kinakabiliwa na shinikizo kubwa.

Ukosefu wa ajira uliokithiri, ambao ulifikia 32% mwaka jana, kukosekana kwa usawa wa kiuchumi, tuhuma za ufisadi na kukatwa kwa umeme mara kwa mara kumepunguza umaarufu wake.

Viwango vya juu vya uhalifu wa kikatili, wastani wa ubakaji 130 na mauaji 80 kwa siku katika miezi mitatu iliyopita ya mwaka 2023 pia yamepunguza imani kwa mamlaka.

Lakini ANC inasema inajitahidi kutatua matatizo haya.

Na inawasihi watu wasifumbe macho kuona faida waliyopata tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi.

Chama hicho kinasema viwango vya umaskini vimepungua, idadi kubwa ya Waafrika Kusini wanaishi katika nyumba nzuri na upatikanaji wa huduma za afya umeboreka.

xx

Chama cha ANC kimeahidi kutengeneza fursa mamilioni za kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ili kuimarisha uwekezaji, kusaidia sekta binafsi na kumaliza ufisadi.

Vyama vya upinzani vya DA na EFF vinaahidi nini?

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kinasema "nchi iko kwenye mgogoro".

Inataka kufanya uchumi huria, ikiwa ni pamoja na kuelekea kwenye ubinafsishaji mkubwa zaidi.

Imeahidi kuunda nafasi mpya za kazi milioni mbili, kumaliza kero ya kukatwa kwa umeme na "kupunguza kwa nusu kiwango cha uhalifu".

DA inasema inaweza kuiokoa Afrika Kusini

Chanzo cha picha, EPA

Ili kukabiliana na ukosefu wa ajira na usawa, chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) , chama cha tatu kwa ukubwa bungeni kina masuluhisho makubwa ya kiuchumi.

Chama kinahoji kuwa ANC haijarekebisha usawa wa kiuchumi wa ubaguzi wa rangi. Inapanga kugawa tena ardhi kwa watu walio na uwezo mdogo.

EFF pia inataka kutaifisha migodi, mabenki na sehemu nyingine muhimu za uchumi, ikisema kwamba utajiri wa nchi hiyo utatumika kuwanufaisha watu wengi.

Je, Jacob Zuma na chama cha MK?

Rais wa zamani Jacob Zuma, ambaye aliondolewa madarakani na Bw Ramaphosa kutokana na madai ya ufisadi ambayo anayakanusha na baadaye kufungwa jela kwa kukaidi amri ya mahakama, ameweka uzito wake wa kisiasa nyuma ya mpinzani mpya wa ANC.

Rais wa zamani Jacob Zuma amekuwa akifanyia kampeni chama cha MK

Chanzo cha picha, Reuters

Chama cha uMkhonto we Sizwe (MK), ambacho kimechukua jina lake kutoka kwa tawi la zamani la ANC, kinaongeza kutotabirika zaidi kwa kinyang'anyiro hicho.

Kinaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika jimbo analotoka Bw Zuma la KwaZulu-Natal.

Katika ilani fupi inaahidi kubadilisha Afrika Kusini, ikiwa ni pamoja na lengo la kuunda nafasi za kazi milioni tano.

Nani anaweza kuwa rais ajaye wa Afrika Kusini?

Waafrika Kusini hawampigii kura rais.

Badala yake wanachagua wajumbe 400 wa Bunge la Kitaifa, ambao wanakwenda kumpigia kura kiongozi mpya wa nchi ndani ya siku 30 za uchaguzi mkuu.

EFF inasema kuwa udhibiti mkubwa wa hali ya uchumi utaunda jamii yenye haki

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa hivyo, hakuna wagombeaji urais kama hao, lakini kila kiongozi wa chama anaongoza kampeni zao za kitaifa na picha yao itaonekana kwenye karatasi ya kura.

Rais wa ANC Ramaphosa, John Steenhuisen wa DA na Julius Malema wa EFF wote watashiriki.

Kiongozi wa chama chochote anaweza kupata kura nyingi katika Bunge la Kitaifa baada ya uchaguzi atatarajiwa kuwa rais ajaye.

Je, uchaguzi unafanyikaje?

Sehemu ya viti ambavyo vyama vimetengwa katika Bunge la Kitaifa lenye wajumbe 400 inahusiana moja kwa moja na sehemu ya kura watakazopata kila chama.

Mnamo 2024, wagombea wa kujitegemea watajumuishwa kwa mara ya kwanza.

Hii ina maana kwamba Waafrika Kusini watapiga kura tatu:

  • Bunge la Kitaifa: Moja kwa viti 200 na vyama vya kisiasa vilivyotajwa kwenye kura
  • Bunge la Taifa: Moja kwa viti 200 vilivyobaki na karatasi tofauti ya kupigia kura kwa kila jimbo kati ya majimbo tisa, ikiorodhesha vyama katika mkoa huo na wagombea binafsi.
  • Bunge la Mkoa: Moja kwa ajili ya wagombea binafsi au vyama katika bunge la mkoa.
xx

Serikali ya umoja itaundwa vipi nchini Afrika Kusini?

Katiba haielezi jinsi muungano unaweza kuundwa.

Lakini kwa kuchukulia kuwa ANC inasalia kuwa chama kikubwa zaidi, makundi madogo madogo yanaweza kukubaliana kwa njia isiyo rasmi kuunga mkono serikali ya ANC kwa misingi ya kura baada ya kura ili kuingia katika makubaliano.

Au, kwa upande mwingine, ANC inaweza kuingia katika muungano rasmi na baadhi ya vyama, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya maandishi yanayoelezea mipango ya kisheria na usambazaji wa nyadhifa za baraza la mawaziri.

Chama kingine chochote kitakabiliwa na chaguo sawa.

Lakini pia kuna uwezekano wa muungano wa upinzani.

Katika mpango wa kabla ya uchaguzi, kundi la vyama, linaloongozwa na DA, limetia saini kile kinachojulikana kama Mkataba wa Vyama vingi vya Afrika Kusini.

Ikiwa kwa pamoja watapata zaidi ya 50% ya viti, tayari wamekubali kuunda serikali ya umoja. Mkataba huo haujumuishi EFF.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo