Afrika ni eneo la pili kwa ustawi wa kasi kiuchumi duniani, Afrika Mashariki yaongoza
![Afrika ni eneo la pili kwa ustawi wa kasi kiuchumi duniani, Afrika Mashariki yaongoza](https://media.parstoday.ir/image/4c3sb945d6f08d2eynm_800C450.jpg)
Jumla ya nchi 41 za Afrika (yaani, 72% ya bara zima) zinatarajiwa kuonyesha viwango vya juu vya ukuaji wa kiuchumi mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana. Hayo ni kulingana na Mtazamo wa Kiuchumi wa Afrika wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Zaidi ya hayo, mwaka wa 2024 na 2025, bara Afrika litadumisha
nafasi yake kama eneo la pili linalokua kwa kasi, baada ya Asia inayokua
kila wakati.
Ukuaji wa wastani wa Afrika uliongezeka hadi 3.7% mwaka 2024 na 4.3% mwaka 2025, juu ya wastani wa dunia uliotabiriwa wa 3.2%.
Mnamo 2024, uchumi nchi 17 Afrika unatarajiwa kukua kwa zaidi ya 5%.
Idadi hiyo inaweza kufikia 24 mwaka wa 2025 kadiri ukuaji
unavyoongezeka.
Afrika Mashariki inatabiriwa kuongoza mkondo huu wa ukuaji na kupita
viwango vya kabla ya 2023. Ukuaji wa wastani hadi wenye nguvu
unatarajiwa katika maeneo mengine.
Licha ya ukuaji, bara bado linakabiliwa na changamoto. Afrika inaweza
isifikie Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030, kulingana na
utafiti. Mtazamo wa Kiuchumi wa Afrika wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
unadai kuwa wengi wa watu maskini zaidi duniani watakuwa wanaishi barani
Afrika ifikapo mwaka 2030 kama hatua hazitachukuliwa kukomesha mkondo
wa umaskini unaozidi kuongezeka.