Matokeo ya uchaguzi Afrika kusini: Hatma ya ANC

 .

Chama tawala Afrika kusini kimefanikiwa kujikusanyia 40% ya kura katika uchaguzi mkuu nchini wakati zoezi la kuhesabu kura likielekea kukamilika.

Matokeo hayo ni pigo kubwa kwa chama ambacho Nelson Mandela alikiongoza kupata ushindi wa kishindo baada ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo 1994.

Kimepoteza uwingi bungeni kwa mara ya kwanza, lakini matokeo haya yanakuja kwa mshtuko kwa rais Cyril Ramaphosa na chama chake.

Wachambuzi wengi walitabiri kuwa chama hicho kitafikia 50% na katika hali mbaya sanakitakaribiakujizolea 45% ya kura.

Kwa sasa ANC kimefanikiwa kujizolea 40% baada ya97% ya matokeo kutoka maeneo ya kupiga kura kutangazwa na tume ya uchaguzi.

Chama hicho sasa kitalazimika kuingia katika muungano, hatua inaidhinisha mwanzo mpya katika siasa za Afrika kusini.

Uchaguzi ulifanyika Mei 29.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo