Mwanasoka aliyekataa kuufanyia kampeni 'ushoga' afungiwa kucheza mechi nne Ufaransa

 

  • Mwanasoka aliyekataa kuufanyia kampeni 'ushoga' afungiwa kucheza mechi nne Ufaransa

Kiungo wa kati wa klabu ya soka ya Monaco ya Ufaransa Mohamed Camara amefungiwa kucheza mechi nne za ligi ya nchi hiyo baada ya kuficha kwenye jezi yake ujumbe wa kutetea vitendo vichafu vya maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja wakati wa mechi ya mwisho ya ligi ya klabu hiyo msimu huu.

Kamati ya nidhamu ya ligi ya Ufaransa ilisema katika taarifa yake iliyotoa siku ya Alkhamisi kwamba imempiga marufuku mchezaji huyo wa kimataifa wa Mali kwa kukataa "kuchukua hatua moja au zaidi ili kuongeza ufahamu wa vita vya kupambana na wanaochukia ushoga."
 
Michuano ya ubingwa wa soka wa Ufaransa iliandaa kampeni yake ya kila mwaka dhidi ya ubaguzi wakati wa mechi za mwisho za ligi ambapo wachezaji wa kila timu walitakiwa kuvalia beji inayoonyesha neno "homophobia" lenye maana ya uenezaji chuki dhidi ya ushoga likiwa limepigwa mchoro.
 
Hata hivyo katika mechi ya mwisho ya Monaco, Camara aliamua kufunika beji hiyo na akagomea pia kupiga picha ya pamoja ya kabla ya mechi ambapo wachezaji wote walisimama mbele ya beramu lililokuwa na ujumbe huohuo.
Idrissa Gueye

Kufuatia msimamo uliochukuliwa na mwanasoka huyo Muislamu kwa sababu ya imani yake, Waziri wa Michezo wa Ufaransa Amélie Oudéa-Castéra alidai kuwa hatua alizochukua Camara "hazikubaliki" na kutaka "adhabu kali" itolewe dhidi ya mchezaji huyo na klabu yake ya Monaco.

 
Huu ni msimu wa nne mfululizo ambapo vilabu vya soka vya Ufaransa vimetakiwa kutumia nambari za rangi ya upinde wa mvua, beji za mkononi au kwenye jezi zao kupigia upatu vitendo vichafu vya LGBTQ. Migogoro kama hiyo hutokea kila mwaka wakati wa ligi ya soka ya nchi hiyo.
 
Mnamo mwaka 2022, kiungo wa Everton mzaliwa wa Senegal, Idrissa Gueye, ambaye wakati huo alikuwa akiichezea PSG, alikataa kushiriki katika mechi ambayo wachezaji walitakiwa kuvaa jezi za rangi ya upinde wa mvua. Rais wa Senegal wakati huo Macky Sall alimuunga mkono Gueye, na kutangaza kwamba "imani yake ya kidini lazima iheshimiwe".
 
Mwaka jana pia, Nantes ilimpiga faini mshambuliaji wa Misri Mostafa Mohamed kwa sababu sawa na hizo.../

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo