Mwanaume, 91, mgonjwa wa kwanza kupandikizwa konea ya bandia Uingereza

 .

Mzee mwenye umri wa miaka 91 ambaye alikua mgonjwa wa kwanza nchini Uingereza kupokea konea ya bandia anasema kuwa hiyo imefanya maisha yake kuwa ya "furaha".

Cecil Farley, kutoka Chobham, Surrey, alilazimika kusubiri kwa mwaka mzima kufanyiwa upasuaji wa macho baada ya upandikizaji wa konea ya binadamu kushindwa.

Lakini alipewa fursa ya kuwekewa konea bandia.

Madaktari wanatumai siku moja ya kuwekewa konea bandia inaweza kupunguza hitaji la michango ya konea ya binadamu.

Bw Farley, ambaye alisema alikuwa na matatizo ya jicho lake la kulia kwa takriban miaka 15, alifanyiwa upasuaji huo mwezi Februari.

Alisema alikuwa ameondokana na tatizo la kutoona hadi kurejea kuona taratibu.

Bw Farley alisema: "Inafanya maisha yako kukamilika wakati macho yako yanafanya kazi ipasavyo – hauwezi kutambui jinsi inavyoathiri hadi utakapokutana na tatizo hilo.

"Bado ninaweza kumuona mke wangu baada ya miaka 63 ya ndoa, tunaweza kuendelea tu na maisha yetu kama kawaida na kuishi maisha kikamilifu kadri tuwezavyo."

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo