‘Israel haikabiliani tu na Hamas bali washirika wote wa Iran’- Netanyahu

 

‘Israel haikabiliani tu na Hamas bali washirika wote wa Iran’- Netanyahu

Netanyahu

Chanzo cha picha, Reuters

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameliambia jarida la Times kwamba nchi yake haikabiliani na Hamas pekee bali mapambano yake yanajumuisha mhimili mzima wa Iran.

Netanyahu alisisitiza kuwa lengo katika Ukanda wa Gaza ni kupata ushindi wa uhakika "dhidi ya Hamas, ili isiwe tishio kwa usalama wa Israel, na kuzuia uingizaji wa silaha kutoka Sinai hadi Gaza, akisisitiza juu ya udhibiti wa kudumu wa Ukanda huo."

Alieleza kuwa kuenea kwa vita vya Gaza na kuwa mzozo wa kikanda ni hatari ambayo anaifahamu, akisisitiza kuwa yuko "tayari kuikabili."

Netanyahu pia alisema vita hivyo vitamalizika endapo Hamas watajisalimisha, kuweka chini silaha zake na viongozi wake kuondoka Ukanda huo kuelekea uhamishoni.

Alielezea maono yake kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza baada ya vita kumalizika, ukiwakilishwa na utawala wa kiraia unaoendeshwa na wakazi wa Ukanda huo, kwa msaada wa washirika wa kikanda.

Matamshi ya Netanyahu yanakuja kabla ya kikao cha baraza la mawaziri la usalama na kisiasa la Israel kilichopangwa kufanyika jioni hii, huku nchi hiyo ikiwa katika hali ya tahadhari kwa mashambulizi ya Hezbollah kulipiza kisasi mauaji ya Fouad Shukr, mmoja wa viongozi wa kundi hilo, na hatua ya Iran kwa mauaji ya Ismail Haniyeh, aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa Hamas, aliuawa mjini Tehran.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024