Je, hatua ya ujasiri na ya hatari ya Ukraine kuivamia Urusi inaelekea wapi?

 

Je, hatua ya ujasiri na ya hatari ya Ukraine kuivamia Urusi inaelekea wapi?

.

Chanzo cha picha, Reuters


Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine imetangaza kuwa haina nia ya kushikilia kabisa eneo dogo la ardhi ya Urusi ambalo imeliteka wiki iliyopita.

Lakini inakabiliwa na chaguo gumu – ikiwa ibakize vikosi vyake huko ili kutoa shinikizo kwa Moscow au ijiondoe.

Wakati ikishambuliwa kila siku kwa makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi, vikosi vyake vilivyochoka vya mstari wa mbele vilikuwa vikirudi nyuma polepole huko Donba; Ukraine ilikuwa ikihitaji habari njema katika kipindi hiki cha joto.

Na kwa uvamizi huo wa kijasiri, wa ajabu na uliotekelezwa vyema katika eneo la Kursk la Urusi, imefanikiwa sasa kupata habari njema.

"Jambo la kushangaza zaidi kuhusu uvamizi huu," anasema afisa wa jeshi la Uingereza ambaye aliomba jina lake lisitajwe, "ni jinsi Ukraine ilivyoweza kumiliki vita –vita vya angani, ardhini hadi vita vya kieletroniki. Hilo linavutia."

Ukraine pia inaonekana kutumia baadhi ya silaha za kisasa zinazotolewa na nchi za Magharibi - kama vile vifaru vya Marder vya Ujerumani na magari mengine ya kivita.

Wamepata ufanisi zaidi kuliko mashambulizi ya mwaka jana ya majira ya joto yaliyoshindwa kulisukuma jeshi la Urusi nje ya majimbo ya kusini-mashariki ya Ukraine.

Uvamizi huo unakwenda wapi?

Kutakuwa na wale ambao watasema Ukraine tayari imeonyesha kuwa vita alivyochagua Putin, lazima sasa vilete maumivu kwa Warusi. Licha ya kurudi nyuma hivi karibuni kwenye uwanja wa vita huko Donbas, Ukraine imeonyesha ina uwezo wa kufanya mashambulizi yenye ufanisi.

Na watasema sasa Ukraine inapaswa ijiondoe mapema, baada ya kuipa Kremlin sababu ya kumwaga damu, kabla ya Urusi kuleta vikosi vya kutosha kuua au kukamata Waukraine walio vamia.

Lakini kujiondoa kunaweza kufifisha malengo mawili ya uvamizi wa Ukraine, ambayo ni kuweka shinikizo la kutosha kwa Urusi kwamba inalazimika kuondoa baadhi ya wanajeshi wake huko Donbas na pili kushikilia eneo la Urusi na kulitumia kama mtaji wa mazungumzo katika siku zijazo. Mazungumzo ya amani.

"Ikiwa Kyiv inashikilia eneo la Urusi," anasema Dk David Blagden wa Chuo Kikuu cha Exeter, "inaweza kufanya mazungumzo ya kurudisha eneo lake lililoshikiliwa na Urusi.

Kyiv pia itakuwa imejaribu kuharibu nguvu za serikali ya Putin na hisia za Warusi na kuihimiza Kremlin kutafuta suluhu isije ikawa hatari kwa Putin kuendelea kuwa madarakani.

Jambo moja liko wazi. Uwepo wa vikosi vya kigeni katika ardhi ya Urusi ni jambo ambalo Putin hawezi kamwe kulivumilia.

Atafanya kila awezalo kutatua uvamizi huu na kuweka shinikizo kwa Ukraine huko Donbas kwa kuwaadhibu raia wa Ukraine kwa mashambulizi zaidi ya droni na makombora.

Hasira yake katika runinga ya Urusi akiongoza mkutano wa dharura huko Moscow jana, ilikuwa iko wazi.

Kamari ya Ukraine imelipa?

Bado ni mapema sana kuwa na jawabu ya hilo. Ikiwa vikosi vyake vitakaa ndani ya ardhi ya Urusi, watatarajia kushambuliwa vikali kila wakati.

Dk Blagden anasema "wanajeshi na vifaa kuendelea kushikilia maeneo yaliyoivamia, litakuwa jambo muhimu, haswa ikiwa njia za usambazaji mahitaji zitapanuka."

Bila shaka ni hatua ya ujasiri zaidi ya Ukraine kwa mwaka huu. Pia ni hatua hatari zaidi.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China