Mtaalamu wa mifugo wa Uingereza afungwa kwa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mbwa

 

Mtaalamu wa mifugo wa Uingereza afungwa kwa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mbwa

Adam Britton alikuwa mmoja wa watafiti wakuu wa mamba ulimwenguni

Chanzo cha picha, ABC News

Mtaalamu mashuhuri wa mamba wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela nchini Australia, baada ya kukiri kuwadhulumu mbwa kadhaa kingono, katika kesi ambayo ilitisha taifa hilo.

Onyo: Hadithi hii ina maelezo ya kuhuzunisha ya ukatili wa wanyama.

Adam Britton, mtaalamu wa elimu ya wanyama ambaye amewahi kufanya kazi katika BBC National Geographic, alikiri mashtaka 56 yanayohusiana na unyama na ukatili wa wanyama.

Pia alikiri makosa manne ya kupata vifaa vya unyanyasaji wa watoto.

Mahakama ya Juu ya Eneo la Kaskazini (NT) ilimsikiliza mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 53 alyeijirekodi akiwatesa wanyama hao hadi karibu wote wakafa, na kisha kuzichapisha video hizo mtandaoni kwa majina bandia.

Vitendo vyake vya unyanyasaji havikutambuliwa kwa miaka mingi, hadi kidokezo kilipopatikana katika moja ya video zake.

Britton alikamatwa Aprili 2022 baada ya upekuzi katika mali yake ya kijijini Darwin, ambayo pia iligundua vifaa vya unyanyasaji wa watoto kwenye kompyuta yake ndogo.

Sehemu kubwa ya maelezo ya uhalifu wa Britton ni ya wazi sana kuweza kuchapishwa, na kwa hivyo ni "ya kuchukiza" hakimu wakati fulani aliwaonya watu kuondoka kwenye chumba cha mahakama.

"Upotovu wako uko nje ya dhana yoyote ya kawaida ya mwanadamu," Jaji Mkuu Michael Grant alimwambia Britton, kiwa ni pamoja na muda ambao tayari umetumika, Britton anaweza kustahiki msamaha Aprili mwaka 2028.

Pia amepigwa marufuku kumiliki mamalia wowote katika maisha yake yote. Wakili wa Bw Britton alisema kosa lake lilitokana na ugonjwa usio wa kawaida unaosababisha mvuto wa kimapenzi usio wa kawaida.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024