Saa 1 iliyopitaYunus arejea Bangladesh kuongoza serikali ya mpito
Yunus arejea Bangladesh kuongoza serikali ya mpito

Chanzo cha picha, Reuters
Mshindi wa tuzo ya Nobel Muhammad Yunus amewasili nchini Bangladesh kabla ya kuapishwa kuwa kiongozi wa muda wa nchi hiyo.
Yunus mwenye umri wa miaka 84 anawasili siku chache baada ya Sheikh Hasina - mwanamke ambaye alitawala Bangladesh kwa mkono wa chuma kwa miaka 15 - kutorokea India.
Alijiuzulu baada ya wiki kadhaa za maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi - ambayo yalisababisha vifo vya mamia - yaliongezeka na kumalizika kwa wito wa kumtaka ajiuzulu
Lilikuwa ni moja ya matakwa ya wanafunzi kwamba Prof Yunus aongoze serikali ya mpito, wakitumai kwamba atarudisha demokrasia nchini Bangladesh baada ya miaka mingi ya utawala wa kiimla.