Saa 2 zilizopitaAkutwa na hatia ya kutuma mtoto wake kumuua rapa PnB Rock
Akutwa na hatia ya kutuma mtoto wake kumuua rapa PnB Rock

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanaume mmoja amepatikana na hatia na mahakama ya Los Angeles Jumatano ya kumtuma mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 17 kumuua rapa PnB Rock.
Freddie Trone, 42, alipatikana na hatia ya mashtaka mengi, ikiwa ni pamoja na mauaji, makosa mawili ya wizi wa daraja la pili na shtaka moja la kula njama ya wizi, baada ya nyota huyo wa hip-hop wa Philadelphia kuuawa kwa kupigwa risasi Septemba 2022.
Rapa huyo alikuwa akila kwenye mgahawa wa Roscoe's Chicken and Waffles huko Los Angeles akiwa na mpenzi wake, ambaye ni mama wa mtoto wake wa miaka minne, wakati kijana huyo, aliyevaa barakoa aliingia kwenye mgahawa huo, na kudai vito vya msanii huyo na. kufyatua risasi.
Polisi walisema kijana huyo aliondoa vitu kutoka kwa muathiriwa kisha akakimbia kwa gari lililokuwa likisubiri, ambalo Trone alishutumiwa kuendesha, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
PnB alipata majeraha mengi ya risasi na alitangazwa kuwa amefariki katika hospitali ya eneo hilo chini ya saa moja baadaye.
Waendesha mashtaka wakati wa kesi hiyo walidai kuwa kijana huyo alikuwa akitekeleza agizo la baba yake huku timu ya utetezi ya Trone ikisema kuwa alikuwa msaidizi tu baada ya uhalifu.