Uingereza: Zaidi ya 90 wakamatwa kufuatia maandamano ya mrengo mkali wa kulia
Uingereza: Zaidi ya 90 wakamatwa kufuatia maandamano ya mrengo mkali wa kulia

Chanzo cha picha, PA Media
Zaidi ya watu 90 wamekamatwa baada ya maandamano ya siasa kali za mrengo wa kulia kusababisha ghasia katika miji kadhaa nchini Uingereza siku ya Jumamosi.
Vurugu zilishuhudiwa katika miji ya Hull, Liverpool, Bristol, Manchester, Stoke-on-Trent, Blackpool na Belfast, huku mabomu ya machozi yakirushwa, maduka kuporwa na polisi kushambuliwa katika baadhi ya maeneo.
Waziri Mkuu Sir Keir Starmer ameahidi kuvipa vikosi vya polisi "msaada kamili" wa serikali kuchukua hatua dhidi ya "wenye msimamo mkali" wanaojaribu "kupanda mbegu ya chuki".
Mvutano umekuwa mkubwa baada ya mauaji ya wasichana watatu wadogo kwenye tamasha ya densi yenye mada ya Taylor Swift huko Southport, Merseyside, Jumatatu.