Wanajeshi 25 wapatikana na hatia ya jaribio la mapinduzi Sierra Leone

 

Wanajeshi 25 wapatikana na hatia ya jaribio la mapinduzi Sierra Leone

Mwanajeshi mwenye silaha akishika doria katika mitaa ya Freetown kufuatia mfululizo wa mashambulizi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwanajeshi mwenye silaha akishika doria katika mitaa ya Freetown

Mahakama ya kijeshi ya katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown imewapata wanajeshi 25 na hatia ya mashtaka yote katika jaribio la mapinduzi lililotibuka Novemba 2023.

Lakini afisa mmoja, Sitta Dumbuya ameachiliwa huru kwa mujibu wa chombo cha habari cha Sierra Leone.

Baada ya mawakili wa utetezi kumaliza maombi yao, hatua inayofuata itakuwa hukumu yao.

Wanajeshi hao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na uasi, kushindwa kukandamiza uasi, mauaji, kusaidia adui na kuwasiliana na adui.

Novemba mwaka jana, watu wenye silaha walivamia ghala la kijeshi na magereza kadhaa huko Freetown, na kuwaachilia karibu wafungwa 2,000

Mamlaka ilielezea hatua yao kama jaribio la "kupindua" serikali.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024