Zaidi ya watu 50 wauawa katika maandamano ya kupinga serikali nchini Bangladesh

 

Zaidi ya watu 50 wauawa katika maandamano ya kupinga serikali nchini Bangladesh

Maandamano yanaendelea licha ya ukandamizaji mkubwa ulioanza mwezi uliopita

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maandamano yanaendelea licha ya ukandamizaji mkubwa ulioanza mwezi uliopita

Takriban watu 50 wameuawa nchini Bangladesh huku makabiliano kati ya polisi na waandamanaji wanaopinga serikali yakizidi kuwa mabaya.

Machafuko hayo yanakuja huku viongozi wa wanafunzi wakitangaza kampeni ya kutotii raia kumtaka Waziri Mkuu Sheikh Hasina ajiuzulu.

Polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji katika maeneo kadhaa ya Bangladesh siku ya Jumapili.

Takriban watu 200 wamejeruhiwa. Amri ya kutotoka nje usiku imeanza kutekelezwa huku mamlaka ikijaribu kukomesha maandamano kote nchini.

Maandamano ya wanafunzi yalianza kwa kutaka kukomesha upendeleo katika kazi za utumishi wa umma mwezi uliopita, lakini sasa yamegeuka kuwa vuguvugu kubwa la kupinga serikali.

Siku ya Jumapili Waziri wa Sheria na Haki Anisul Huq aliambia kipindi cha Newshour cha BBC kwamba viongozi wamekuwa "wakijizuia".

“Laiti hatungejizuia kungekuwa na umwagaji damu. Nadhani uvumilivu wetu una mipaka,” aliongeza.

Katika mji mkuu, Dhaka, huduma za intaneti zimefungwa.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024