Idara ya huduma za usalama ya Marekani ina 'dosari kubwa' na lazima ibadilishe uongozi, ripoti yanasema
Idara ya huduma za usalama ya Marekani ina 'dosari kubwa' na lazima ibadilishe uongozi, ripoti yanasema

Chanzo cha picha, EPA
Idara ya huduma za usalama ya Marekani (Secret services) ina "dosari kubwa" ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa haraka au majaribio zaidi ya mauaji kama yale yaliyofanyika mkutano wa hadhara wa Donald Trump yatatokea tena, ripoti iliyofichua kasoro yasema.
Jopo huru lililopewa jukumu la kuchunguza tukio la ufyatuaji risasi wa Julai 13 huko Butler, Pennsylvania, lilitoa matokeo yake siku ya Alhamisi, na kusema shirika hilo limekuwa "la urasimu, lenye kuridhika na halichukui maamuzi".
Katika ripoti hiyo ya kurasa 52 , ripoti hiyo ilitoa wito wa kufanyiwa marekebisho uongozi wake, na kusema " kushindwa kwa utekelezaji kazi wake " kuliwezesha kufanyika kwa mashambulizi dhidi ya mgombea urais wa Republican.
Tayari Idara ya huduma za usalama imekubali kushindwa kwa upande wake, na mkurugenzi wake alijiuzulu wiki chache baada ya kshambulio la risasi dhidi ya Trump.
Katika taarifa siku ya Alhamisi, kaimu mkurugenzi wake Ronald Rowe alisema shirika hilo litachunguza kwa makini ripoti hiyo mpya