Kiongozi wa Hamas Yahya Al-Sinwar auawa na vifaru baada ya kufanya makosa, IDF yaiambia BBC
Kiongozi wa Hamas Yahya Al-Sinwar auawa na vifaru baada ya kufanya makosa, IDF yaiambia BBC

Chanzo cha picha, Reuters
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) ametoa maelezo zaidi kuhusu jinsi Sinwar alivyouawa, katika mazungumzo na kipindi cha BBC cha Newshour.
Maj Doron Spielman anasema IDF imekuwa ikifanya kazi katika Rafah kwa lengo la kuwakamata "magaidi wakuu zaidi" - akiwemo Yahya Sinwar.
Spielman anasema katika operesheni zao, vikosi vya IDF vilifunga barabara, vililipua mahandaki na kudhibiti harakati zake katika "eneo dogo zaidi na dogo zaidi ", na kumlazimisha Sinwar "kutembea kama mkimbizi" na hatimaye "kufanya kosa".
"Kusema kweli, ni jana tu alifanya hivyo. Aliondoka kwenye handaki, akaenda kwenye jengo la ghorofa, na [Hamas] akawafyatulia risasi wanajeshi wa Israeli. Kifaru kilijibu mashambulizi, na akauawa katika shambulio hilo."