Marekani kutenga dola milioni 425 za msaada wa kijeshi kwa Kyiv, huku Australia ikipeleka vifaru 49 vya Abrams
Marekani kutenga dola milioni 425 za msaada wa kijeshi kwa Kyiv, huku Australia ikipeleka vifaru 49 vya Abrams

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza kwa simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Jumatano na kutangaza kifurushi kipya cha msaada wa kijeshi cha dola milioni 425.
Kulingana na huduma ya vyombo vya habari vya White House, kifurushi hicho kitajumuisha, mifumo ya ulinzi wa anga, na magari ya kivita.
Wakati huo huo Australia itapeleka mizinga 49 ya Abrams ya mtindo wa zamani wa M1A1 nchini Ukraine, ripoti ya vyombo vya habari vya Australia ikimnukuu waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Pat Conroy.
Kwa mujibu wa shirka la utangazaji la Australia, wiki chache zilizopita Australia ilipokea kundi la kwanza la mizinga ya mtindo mpya wa M1A2.
Gharama ya jumla ya mizinga ambayo Ukraine itapokea inathamani ya dola Australia milioni 245 za Australia (sawa na dola za Marekani milioni 163.5).
Australia imeagiza mizinga 120 ya Abrams M1A2, gazeti la The Age limeandika.
Jeshi la Australia litahifadhi idadi fulani ya vifaru vya zamani kwa sasa hadi magari mapya yatakapowasili.
Uongozi wa Ukraine uliomba mizinga iliyotengenezwa na nchi za Magharibi katika majira ya baridi ya 2022-23, wakati ilionekana kuwa muhimu kwa ajili ya mashambulizi ya kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.
Biden alizungumza na Zelensky na kutangaza kifurushi kipya cha msaada cha $ 425 milioni.