Marekani yashambulia hifadhi za silaha za Wahouthi zilizofichwa chini ya ardhi
Marekani yashambulia hifadhi za silaha za Wahouthi zilizofichwa chini ya ardhi

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amethibitisha kuwa vikosi vya jeshi la taifa hilo zikiwemo ndege aina ya B-2 vimeshambulia hifadhi za silaha za chini ya ardhi za wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen.
Bw Austin amesema operesheni hiyo ilihusisha ulipuaji wa "usahihi" wa hifadhi tano "zilizoimarishwa" chini ya ardhi, zenye lengo la kupunguza uwezo wa kundi hilo kushambulia meli katika eneo hilo.
Amesema hifadhi hizo zina aina mbalimbali za silaha ambazo Wahouthi hutumia kulenga meli za raia na za kijeshi katika eneo lote.
"Hii ilikuwa hatua ya kipekee kuhusu uwezo wa Marekani kulenga vifaa ambavyo wapinzani wetu wanajaribu kuficha, bila kujali kina chake cha chini ya ardhi ," aliandika katika taarifa yake.